ROHO YA KUZIMU SEHEMU YA 1

STORY:-ROHO YA KUZIMU PAGE YA:-1 MWANDISHI:-AMANI KUYELA Karibu sana katika mfululizo mpya wa simulizi hii iliyojaa mpangilio wa mikasa na matukio ya kutisha katika ulimwengu wa roho, kwa wanao amini uwepo wa ulimwengu huu basi nakuja kukujuza elimu dunia katika mtindo wa sanaa ya fasihi andishi nakusafirisha hadi ndani ya ulimwengu huu wa roho kujulikanako kama kuzimu usioweza kuonekana kwa macho ya kawaida ya kibinadamu. Naam, ambatana nami mwandishi wako AMANI KUYELA niweze kukusogezea yale usiyoyaona katika hadithi zingine, story ndo kwanza bado mbichi kabisaa. Baada ya utangulizi huo, sasa twende mzigoni. Ikiwa ni siku nzuri sana ya al hamisi, katika mitaa ya soko kuu la manispaa ya kahama mjini anaonekana mwanadada akiwa amevalia mtoko maridadi kabisa. Mwanadada huyo aliyepanda hewani futi kadhaa zenye ujazo huku umbo lake likiwa lakuvutia lenye muundo wa aina yake, na sura yake ikiwa ni ya kumvuta bwana shitete kutoka huko pangoni, mwanadada huyo akiwa na mchanganyiko wa udongo...