SHAIDA SEHEMU YA 10 MWISHO



SHAIDA: NO 10

"Eddy anakutaka kimapenzi? " swali la Sharif liliulaluwa moyo wa Shaida na kushindwa kujibu.

"Nimeona alivyokuvutia chumbani kwake, na wewe ulionekana kukataa em niweke wazi usinifiche maana unajuwa nakupenda na sihitaji Lolote mbaya likukumbe"

"Sharif... " Shaida alishindwa kuongea akaishia kulitaja jina lake.

"Don't worry, Hakuna kitakachotokea kwako. Kuja kwangu hapa si kwasababu ya mtu yeyote hapa.... Ni kwa ajili yako so! Niambie"

"Sharif ni marefu naomba niache tu"

"Yatakuwa marefu kiasi gani au yatachukuwa wiki ukiwa bado unanielezea? Nimeshakwambia I love you shaida. Nahitaji kuishi na wewe Shaida, ko sipendi kuona ukinyanyasika humu ndani na bwana shemeji"

"Naomba basi njoo kesho ntakwambia ukweli"

"Unaniahidi? "

"Nakuahidi"

Sharif alimtakia usiku mwema, kisha akaondoka. Shaida aliangua kilio ukija kuangalia yeye bado mdogo, na mambo anayoyapitia yapo juu ya uwezo wake, kulia kwake kulimpelekea na mtoto kuanza kulia. Upande wa sebuleni Eddy alikuwa ametulia akiangalia TV, ndipo alikuja Husna na kusema.

"Hey brother, kwanini Umy analia muda huu"

"Why unamjali sana"

"Nampenda like my daughter japo sijazaa"

Eddy alitabasamu tayari kunyanyuka kuelekea mtoto anakolilia.

"Kumwambia mtoto analia anaacha kila kitu, kweli wifi hajadanganya" aliongea Husna na kukaa kwa ajili ya kuangalia katuni.

Upande wa Eddy alifika na kuingia chumbani kwa Shaida bila kubisha hodi.

"Shaida kuna nini?" alihoji na kumfuata mtoto kisha kumnyanyua, Umy alikuwa ni mtoto anaependa kunyanyuliwa, hivo alitulia.

"Niambie nini kinakusibu" alihoji Eddy.

"Sharif alituona"

"Muda ule?"

"Ndio"

"Kwahiyo anasemaje"

"Ameniambia nimuweke wazi kuhusu wewe"

"Umemjibu vipi"

"Nimemwambia ntampa majibu kesho, kwahiyo hapa nimechanganyikiwa hata sijui ntamueleza nini"

"Na Anita kafanyaje au alikwambia nini maana ulitaka kusema hivo muda ule"

"Ameniambia niondoke humu ndani. Aa mi niache" aliongea Shaida na kuangua kilio, taratibu Eddy alimshika na kumlaza kifuani kwake.

"Yote haya uliyasababisha wewe, ulinitelekeza na bado hapa hutaki kunipa amani" alizidi kuongea Shaida.

"Kwasababu nakupenda"

Shaida aliinua uso wake na kumtazama Eddy usoni kisha akamwambia.

"Naomba kesho niondoke"

"huwezi kuondoka...kesho namfuata baba, ni siku mbili ntakuwa nimerudi. Mambo yote yatakaa sawa"

Muda huo kwa bahati Mbaya Husna aliigia na kushangaa.

"Nini shida" alihoji Eddy kwa msisitizo.

"I I I'm sorry" alijibu Husna na kutoka haraka.

"Tayari limekuwa tatizo Eddy" aliongea Shaida kwa hofu.

"Usiogope niko hapa"

"Uko hapa kitu gani... Najuta kuja mjini"

"Nimeshakwambia I'm here"

Majira ya asubuhi Eddy alijipanga kwa ajili ya safari. Kabla hajaondoka, alielekea chumbani kwa Shaida ilikujuwa kaamkaje maana hakuonekana sebuleni kabisa. Alipofika mlangoni alibisha hodi ndipo Shaida alifungua.

"Eddy unafuata nini tena? au Nia yako Anita atukute"

"Nisalimie kwanza"

"Ungeniachia nauli nikaondoka zangu ungekuwa umefanya vizuri zaidi" Shaida aliongea kinyonge na muda huo tayari Eddy alikuwa amezama chumbani.

Upande wa Anita, alikuwa kasimama sebuleni huku akiendelea kumsubiri Eddy ambae hakutokea.

"Unahisi atakuja sasa hivi?" aliongea Husna.

"Unamaana gani?"

"Nenda kamwangalie chumbani kwa Shaida"

"Ati nini?" Anita alihoji kwa mshangao na tayari mashaka yakaanza kumuingia, bila kupoteza muda alielekea chumbani kwa Shaida haraka haraka. Alipofika mlangoni alishusha pumzi huku akiwa anajiuliza Kama kweli Eddy yupo ndani atafanya nini Kama mke ndani ya ndoa. Kabla hajakishika kitasa kwa ajili ya kufungua, muda huo mlango ulifunguliwa, na mfunguwaji alikuwa ni Eddy. hivo uso kwa uso na mkewe.

"Eddy...." sauti ya mshangao ya Anita ilimshtua Shaida aliyoko chumbani.

"Em twende" Eddy alimshika mkono na kumtoa eneo hilo. Kiukweli upande wa Anita alishindwa kuuliza swali lingine ukija kuangalia na Hali aliyonayo ya ujauzito. Eddy aliamua kuondoka bila kumpatia mkewe nafasi ya kujadili swala lile, na alivyowaajabu aliacha moto kauwasha kisha akaondoka bila kuuzima ama kuupoza. Anita akiwa haelewi hili wala lile, alianza kuunganisha matukio siku ya kwanza wanamuona Shaida Hali ya Eddy ilibadirika na tokea hapo maisha ya furaha kwenye ndoa yake yalipungua.

"Wii umeona sasa" aliongea Husna baada ya kumkuta nje.

"Kwanza kaka yangu yuko wapi" alihoji Anita.

"I think atakuwa mazowezini"

"Wifi mwenzio ntakufa"

"dah! Sasa kaka amekuwaje"

"Sielewi chochote, hii ni Mara ya pili namkuta Eddy chumbani kwa Shaida"

"Na Mimi nilitaka umuone kwa macho yako, maana Jana nilivyoingia chumbani kwa ajili ya kuchukuwa mtoto... Mmmmhh wifi huwezi kuamini nimemkuta kaka kamkumbatia Shaida huku Shaida akiwa analia"

"What" alihoji Anita kwa presha ya Hali ya juu.

"Eee sasa sijui nini kinaendelea"

"I'm crazy and you know that"

"I know"

Haraka Anita alielekea ndani kisha Husna akamfuata nyuma. Alipofika sebuleni alimwita Shaida kwa uchungu mpaka machozi yakaanza kumtiririka, Shaida Haraka alifika akiwa amembeba mwanae mgongoni, huku hofu ikiwa imemtawala. Kabla hajauliza alizabwa kibao na Anita, kabla hajakaa sawa alipigwa kingine na kudondoka chini. Nyamisi kwa mbali alikuwa anashangaa.

"Nyanyuka haraka" aliongea Anita kwa hasira huku Shaida na mwanae wakiwa wameanza kulia. Taratibu Shaida alinyanyuka na kuanza kuficha uso wake kutokana na kuogopa kibao.

"Naomba niambie nini kinaendelea Kati yako na mume wangu, I swear Shaida usiponiambia ukweli nakukata Kata vipande vipande" maneno makali ya Anita yalizidi kumpa hofu Shaida.

"Nisamehe" Shaida alishuka chini na kupiga Magoti.

"Staki kusikia, nyanyuka haraka" Anita alianza kumpiga vibao huku na Yeye akiwa analia kwa uchungu.

"Wii basi nimchukuwe mtoto mtamuumiza" aliongea Husna kwa upole.

"Staki na wewe kaa pembeni kabisa, nyote njama moja na kaka yako. Shaida tell me ntakupasua mimi" Anita alivuta chupa ya soda iliyoko pembeni kisha akamnyooshea ishara akizingua anamuua.

"Ntasema ukweli" maskini Shaida alijikuta akitaka kusema ukweli kwa kuyahofia maisha yake na mwanae.

" yes sema ukweli"

"Ukweli ni kwamba Umy ni mtoto wa Eddy" aliongea kwa sauti ya upole na hapo ndipo Anita alichanganyiwa na kutaka kumpiga chupa ya kichwa, ila Nyamisi aliwahi na kumzuwia. Ikawa fujo mtindo mmoja, hofu Kubwa ya Shaida ilikuwa kwa mwanae, Nyamisi alijitahidi kumnyang'anya chupa Ile. Ila kwa bahati Mbaya Anita alimrusha pembeni na kudondoka huku chupa ikapasuka na kumchana kiganjani. Ndipo Anita alimrukia Shaida tayari kuanza kumnyonga bila kujali kilio cha Umy. Husna muda wote alikuwa pembeni bila kusaidia Huku akiruka ruka na kumkanya wifi yake aache.

Kama bahati nzuri aliingia Aisha akiwa na shangazi Kaja iliyomo nguo zake. Baada ya kushuhudia tukio lile alipaza sauti kibabe na kumshtua kila mmoja.

"Achaaaaaaa!!"

Anita ambae macho yalikuwa yamemtoka Kama mlusi aliyebananishwa na mlango, alimuachia Shaida na kugeuka kumtazama Aisha ambae alimfikia na kumuinua juu.

"Wewe ni muuwaji? " Aisha aliuliza. Kabla Anita hajajibu chochote, alizabwa makofi mawili na kudondoka chini.

"Wifi jamani" aliongea Husna ndipo Aisha alimfuata na kumzaba nae pia vibayo viwili.

Haraka Aisha alimfuata mdogo wake Shaida ambae alikuwa anakohoa kwa maumivu kisha akamtoa Umy na kuanza kumbembeleza.

"Dada asante kwakuja" aliongea Shaida baada ya moyo wake kupata faraja.

"Naomba nyote mkae na mnieleze mmoja mmoja shida nini mpaka mnataka kuuwana" aliongea Aisha ndipo Anita aliamka na kukaa kitako huku akilia.

"Niambie, mnahisi kupigana ndio kutafuta suruhu?"

"Siyo hivo Aisha. Mdogo wako muulize nimemthamini kiasi gani? Nimempa kila atakacho mpaka nimemuomba mume wangu amlete mfanyakazi mpya ili apate muda mzuri wa kumlea mwanae..muulize nini amekosa humu? Mwanae anamnyanyua Mara ngapi? Hata Kabla sijajuwa kuwa Mimi mjamzito nimempenda mwanae mpaka sasa sikukata upendo kwa Umy. ..muulize mdogo wako kwanini anataka kunivunjia ndoa yangu" aliongea Anita kwa uchungu, ndipo akaendelea kusema.

"Kumbe anatembea na mume wangu... Hali hii nimeiona kwa muda mrefu, Mara Eddy kumtazama Shaida Mara amvute jamani na Mimi ni mwanamke na nina moyo vilevile"

"Shai jikaze uongee" Aisha aliongea.

"Nisamehe dada Anita, kiukweli sikuja hapa kwa ajili ya Eddy ila Eddy ndie anapenda kunisumbua na simpendi wallah"

"Mbona nimesikia unasema Umy ni mwanae umenidanganya? " aliongea Anita.

"Ndio ni Mwanae"

Muda huo Sharif alikuwa pembeni anaskia, kiukweli moyo ulimuuma ikambidi kusogea.

"Nini kinaendelea dada" aliongea Sharif na kumfanya Anita aangue kilio kwa uchungu.

"Mpigie shemeji aje hapa"

Anita alipewa simu akampigia mumewe ila hakupokea, watu wote walijaribu kumpigia bado hakupokea kitendo kilichozidi kumchanganya Anita.

"Jamani, sote ni watu wazima hapa. Na kila kinachoendelea tunaelewa ningeomba tujipe muda wa kusubiri mwenyewe aje kutatuwa suala hili " aliongea Aisha na Muda huo Husna alimpigia baba yake akapokea.

"Dad huku kuna tatizo.... Kaka nampigia hapokei sim na watu wanataka kuuwana kwa ajili yake kiukweli Fanya uje" Husna alikata simu na kuwaambia.

"Baba kasema yeye yupo njiani na hayupo na Eddy sasa sijui kaka kaelekea wapi"

Walikaa wakimsubiri mpaka majira ya jioni ndipo mzee alitokea na muda wote Eddy hakupokea simu kabisa.

"Dad I miss you" aliongea Husna baada ya kumpokea.

"Mbona mpo kwenye Hali hii nini shida" aliongea mzee na kukaa kwenye sofa. Muda huo aliingia Eddy bila wasi wasi, mkewe alipomuona aliangua kilio.

"Nini kinaendelea hapa" alihoji mzee kwa Mara nyingine. Na hapo Eddy alikuwa amekaa.

"Eddy aongee na ahakikishe ananiandikia talaka" aliongea Anita kwa uchungu.

"Eddy Kuna nini?" mzee wake alimhoji ila bado majibu hayakutolewa.

"Dad sijui kwanini Eddy ameamua kuniaibisha hivi. Kila kitu nimejitolea kwake ila huwezi kuamini anamtaka Shaida" maneno ya Anita yalimfanya mzee ashangae na kugeuka kumtazama Shaida ambae alikuwa ameshusha macho chini.

"Eddy..." mzee alimwita.

"Nam"

"Nini kinaendelea? Eti unamtaka Shaida?"

"No dad, Shaida ni mke Wangu"

Maneno ya Eddy yalimshtua kila alieyekuwa hajui.

"Unamaana gani?" alihoji mzee.

Eddy alianza kutoa mkasa wa mambo yote toka Zanzibar mpaka kufikia hapo mambo yalipofikia.

"Inawezekana vipi mbona sielewi" alihoji mzee.

"Nyie wawili ndugu? " mzee aliwageukia kina Shaida ndipo Anita alinyanyuka na kusema.

"Ulivyonichumbia mpaka kunioa hukuniambia kuwa unamke na mtoto. Eddy chagua Kati yangu na shaida nani unabaki nae kwasababu Mimi siwezi ukewenza" maneno ya Anita yalimshtua kila mmoja ndipo Shaida alijikaza na kusema.

"Anita nakupenda Sana na siwezi kupata amani endapo ntavunja ndoa yako, wewe ndie unaependwa na istoshe Eddy ndani ya moyo wangu hayupo... Nikuombe uwe na amani ntamlea mwanangu peke yangu"

"Naomba niongee" aliongea Eddy na tayari kila mtu kumpa masikio.

"Mimi ni mwanaume, na nyote wawili ni wake zangu tena wandoa. Hakuna Kati yenu anaeweza kunipangia Nani nimuache na Nani niendelee nae, Mimi ndie wakusema namtaka nani abaki humu ndani.... Naomba nisikilizeni kuoa mke zaidi ya mmoja ni sunnah na mwenyezimungu amehalalisha, sasa kwanini mnataka kupingana na maneno ya mwenyezimungu"

"Ongea point Nani abaki na Nani aondoke" aliongea Anita na kuangalia pembeni.

"Usiongee hivo mbele yangu ntakupiga sasa hivi.... OK Hakuna atakaetoka humu ndani"

"ati nini?. Eddy ni hakili zako kweli? Kabisa Mimi nichangie mume na mfanyakazi wangu" aliongea Anita.

"Eddy usijisumbue kwasababu dada amekuja kunichukuwa mi staki ndoa tena" aliongea Shaida.

"Weee ishia hapo Mimi sijaja kukuchukuwa, nimekuja kutafuta maisha" aliongea Aisha na kumfanya kila mmoja acheke.

"Naomba tusikilizane" mzee aliongea na kila mmoja akawa tayari kumsikiliza.

"Eddy ameshaongea kuwa nyote anawapenda, kikubwa Mimi Kama mzazi wenu nyote naomba msimvunje ndoa zenu kisa hasira... Eddy ni mwanangu kaenda huko kaoa bila kunitaarifu, Leo hii mimi ndo kujuwa why sijalalamika Kama mazazi, ni kwasababu najuwa ni Haki yake kuoa kwahiyo naomba muelewe yeye ni mwanaume anauwezo wa Kuoa hata sasa hivi wengine wanawake wawili na msimfanye kitu, so naomba mtulie"

"Nikweli baba ukija kuangalia dada wewe unampenda Shaida kubalini tu iwe hivo" aliongea Sharif.

"Siyo wewe ulikuwa unampenda Shaida, Kwanza siwezi kuchangia mwanaume na mwanamke anaetembea na kaka yangu" maneno ya Anita yalimshangaza kila mmoja.

"Sijawahi kuwa na mahusiano na Shaida hata siku moja ukitaka muulize, sema mimi nampenda ila yeye hanipendi"

Maneno ndani yalizidi ila mwisho wa siku walielewana, Eddy akamuomba msamaha mkewe Anita vile vile na Shaida. Kilichofanyika Eddy alimnunulia nyumba Shaida ya kifahari pamoja na gari ili kuepusha msongamano. Maisha ya furaha yaliendelea mpaka mzee wao huko Zanzibar alikuja kuishi na binti zake.

Huu ndiyo Mwisho wa kastory ketu kafupi. Kametungwa na Aisha khan.

                      MWISHO


TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: BINAMU 🔞 SEHEMU YA 11

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 1-5

CHOMBEZO: MASSAGE ROOM🔞 SEHEMU YA 21