MPENZI CLARA EPISODE 7
MPÉNZĪ CLĀRÁ
EPISODE (07) ✓
!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
ILIPOISHIA
:::::::::::::::::::
nikaona labla ni wenge langu tu nikaweka pozi tena sasa round hii sijui alikuja mama yake yule maana kalikua ni kabibi sana ila nilipo geuka kucheki sikuweza muona mtu nikajua tu sasa hapa kumekucha tena maana wakulungwa nao wanataka wauze sura kwenye camera nilisimama na kuanza kusepa modogo mdogo kama kinyonga
:::::ENDELEA NAYO SASA :::::
nilitembea kama hatua 3 hivi mala nikasikia sauti wewe kijana una kwenda wapi?! ilikua ni sauti ya bibi kizee yani hata matamshi yake yalikua yana toka kwa kubabaika
nilishtuka kidogo kisha nikasimama ila nikaona nikiendelea kusimama pale itakua jau nikaendelea kutembea sasa ile nakilibia kwenye mlango mala naona kono likapita na kwenda kufunga ule mlango kisha likatoka na funguo heeeh!! jamani!! niliongea kwa mshangao sana
niligeuka nyuma nikakiona kile kibibi kimesimama tu etiiih kina nichekea chekea
anha kwaiyo leo ndo wamekuma wewe au sio alafu jamani mbona mnapenda kunipa kesi mchana wote huu alafu mimi sitaki kesi wala mada kesi mjue sasa wewe kizee ngoja nikuonyeshe umafya leo wewe si ndo unajifanya kontawa eehe?! sasa ngoja nikupe dawa yako paka wewe maana nishachoka niliongea kwa ujasiri kweli kweli nilitembea kwa speed kukifata kile kizee ila kabla sijakifikia nilichezea bonge la mkofi aseeh wa paji la uso yani ileeeeh (bampuuuuh!!!) mkofi wa kufunika si mnaujua wazee ghafla niliona kiza mbele yangu na nikaanza kusema (siludii tena siludii tena siludii tena siludii tenaaaah) kwa sauti ya kulia)
mala nikasikia vicheko vingi vingi
(Ahahahah!!! ahahahah!!!! ahahah! ahahahah!!! Ahahahah!!! Ahahah!!! Ahahahah!!! Ahahahah!!! ahahaha!!)
Jamani sasa mbona mnanicheka tena kwani me makosa yangu yako wapi?! jamani eeehe?! alafu kumbe mko wengi kiasi hiki jamani bimdashi naomba unisamehee niliongea kwa uwoga maana nilikua nasikia tu vicheko ila sioni kitu mala kidogo alitokea CLARA kwenye sofa (mamaaah nilishituka sana)
(CLARA- Ahahahah!!!! Ahahah!!! Ahahah!!! sikia JOH wewe unajitesa mwenye sasa unawezaje kumkimbia mkeo?!!!)
Mmmh!!! Akuuuh!!! wakati mimi nilikua naenda kuchota maji ya kunywa pale ndaniiiiiiiih kwenye friji niliongea kwa uwoga huku niking'ata kola ya shati langu
(CLARA- Ahahahah!!! muongo wakati ulikua unataka kukimbia sasa sikia ukitaka uishi kwa amani lazima unioe mimi yani lazima ufunge ndoa na mimi sawaaah?!!! ila kama utaleta ubishi basi chamoto utakiona kwa heri nakupenda sana baby wangu) kisha akayeyuka Yayuuuuuh
Mh!!! kampenda mama ako mzazi niliongea kwa uwoga kidogo kisha nikasimama nakwenda kuokota simu maana nilipopigwa ule mkofi mpaka nilidondosha simu sio poa aseeh usiombe ukutane na mkofi wa jini
niliokota simu yangu lakini niliangalia mlango niliona funguo ikiwa ipo pale pale ila mlango ulikua bado umefunga (hiiiiiih mamaaah wameludisha funguo) niliongea kwa mshangao basi nikafungua mlango kisha nikasepa zangu pale ndani
hapa sasa nishatoka njee na Leo siludi tena mle ndani ma boya wale etiiih lazima unioe nakupenda sana mpenzi wangu alafu kile kijini kiboya kweli ahahah!!! na hamnipati tena humo ndani nyie ma boya hasa wewe kizee saizi nenda kampige baba ako mzazi ule mkofi wako
Ahahah!!! Ahahah!!! kisha nika push zangu (D) nakusepa kabisa maeneo yale maana nilikua nimesimama njee ya lile ghetto langu nilitoka moja kwa moja mpaka (SHISHI FOOD) ili nikale msosi wa mchana nilipofika pale nilimkuta mchizi wangu DELVICK amesha wai mapema sanaaah
Aaaah!!! mzee niaje naona mapema tu kaka au unatoka na shishi Nini?! nilimtania kidogo mchizi wangu
(DELVICK- Daaah!!! we acha tu bro asubuhi sijala kabisa alafu si unajua leo friday kwaiyo birian kama kawa vipi lakini mtoto Clara anasemaje maana naona saizi uko bize sana na Ghetto lako ahahah!!!! Alionge mchzi
emu chana na hizo mada basi sema dada namimi niletee birian na juice ya matunda baada ya dakika chache yule mdada alileta chakula sasa tukawa tunakula mdogo mdogo huku story zikiendela ila mala nikaona juice kwenye grass haipo mh!!! niliguna kidogo oya jamaa juice yangu hapa mbona haipo kuna mtu yoyote amefika hapa nilimuuliza DELVICK kwa mshago kidogo
(DELVICK- aaah!!! jamaa sasa wote si tumekaa hapa alafu unaniuliza sema juice upiga fundo moja tu umemaliza yote inaoneka ulikua una kiu sana kaka Ahahahah!!! Alicheka sana mchizi
ITAENDELEA.......
haya (JOH) amefanikiwa kutoka mle ndani na ameeleka mpaka shishi food ili apate chakula cha mchana lakini wakati ameagiza Brian na juice ya matunda ghafla akiangalia kwenye grass juice hakuna je ni yapi yatafata usikose sehemu ijayo
TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.
Maoni
Chapisha Maoni