ZOMBI WA DAR EPISODE 7
ZOMBI WA DAR
ABEKUKA FILM
EPISODE YA 07
«LEO ZOMBI KAONGEA»
TULIISHIA HAPA....
"Suzi nenda tutakutana baadae.." Mr hance alimwambia yule binti aliye kaa nae baada ya kumuona linah amefika pale hotelini. Suzi alisimama mezani akambusu Mr hance mdomoni na kuondoka.
Linah akafika pale na kukaa kile kiti alichotaka suzi.
"Samahani bosi kwa usumbufu..'
"Ongea haraka kilicho kuleta hapa.."aliongea Mr hance akiwa ameshika grass ya maji anataka anywe.
"Bosi ni kwamba.."
Ni kwamba nini ebu ongea haraka?.."
"Rajah hajafa ni mzima.." aliongea Linah Mr hance akadondodha grass ya maji.
ENDELEA....
"linah umesemaje?.."
"Bosi nimemuona rajah kwa macho yangu mawili hajafa!.."aliongea linah kwa wenge Sana
"Umemuona wapi wakati ni marehemu yule? ."
" Alikuja ofisini inaonekana anakaa nyumba moja na same maana same alisema yule Ni mdogo wake amemtoa Kijijini lakini yule ni rajah bosi.."
"Tuliza mapepe linah kwa Sasa mi nitajua Nini Cha kufanya.."aliongea mr hance akasimama pale na kuondoka.
"Ee mungu nisaidie Mimi.." aliongea linah alafu akajilaza kwenye ile meza ya chakula akiwa na mawazo.
BAHARINI
Mida hiyo maeneo hayo ya baharini walipo kuwa same na zombi kulikuwa Kuna utulivu mkubwa, hakuonekana mtu yeyote zaidi yao.
same na zombi walikuwa wanatembea taratibu wakiyaelekea maji.
"Zombi unajua Kwanini nimekuleta huku? Okay we twende mbele utajua mda sio mrefu.." aliongea same akiwa amemshika zombi mkono wanasogea taratibu mwanzo wa maji ya bahari.
"Huyu jamaa bado simuelewi anataka kunifanya nini? Ngoja tuone.." zombi alifikilia kimoyo moyo akiendelea kusogea na same mpaka wakagusa maji. Zombi akasimama
"Acha uoga twende mbele zaidi..." Same alimshika zombi mkono na kuendelea kutembea wakielekea mbele zaidi.
Walitembea mpaka wanafika kina Cha maji yaliyowafika kifuani same akasimama maana pale mbele palikuwa na mawimbi makali Sana alafu maji yanazunguka kwa Kasi kukionekana kuwa na kina kirefu Cha maji.
"Zombi naomba unisamehe kwa ninachoweza kufanya." Aliongea same kisha kwa haraka san anamsukuma zombi pale mbele kulipo kuwa na kina kirefu Sana cha maji alafu yeye akarudi nchi kavu.
Zombi hakutegemea lile jambo halilo tendewa alibaki kuangaika kutoka ndano ya maji lakini viungo vya zombi vipo taratibu Sana hivyo ilikuwa ni ngumu yeye kutoka pale alijikuta anazidi kupelekwa na mawimbi mbele zaidi kulipokuwa na kina kirefu.aliunguruma tu akiwa anatapatapa ndani ya maji.
"Nisamehe zombi nimefanya hivi ili nisipoteze kazi na watu wangu wa karibu sikuwa na namna zaidi ya kufanya hivi samahani sana ." aliongea same kwa uchungu akiwa amesimama kando ya bahari anamtazama zombi akiteseka.
Waswahili wanasema ukitaka kujua spidi ya kinyonga choma msitu kwa tafsiri nyingine nasema tatizo linaweza likaonyesha picha nyingine ya mtu iliyojificha huwezi kuamini zombi akiwa anazama aliita kwa sauti ya kujirazimamisha mapaka ikasika kwa maneno yanano eleweka
"Same njoo unitoe nazama.." ilikuwa Ni sauti ya zombi mala hii ilisikika kwenye masikio ya same, iliyomfanya same abaki anashangaa tu.
"Inamaana leo ameongea.."same aliongea taratibu akiwa anatokwa na machozi ya furaha.
"Niokoe same.."zombi aliongea tena mwisho akazama
"Nakuja zombi.." same alianza kurudi ndani ya maji mbiombio, akapiga mbizi mpaka alipozama zombi kwenye kile kina kirefu zaidi, akamshika mkono na kuanza kumvuta kumbe same na yeye hawezi kuogelea hilo swala hakuyumba kabla.akiwa anaendelea kumvuata zombi kwenye kile kina, maji yalimvuta na yeye wakajikuta wote wanarudisha nyuma mpaka ndani ya kina kirefu zaidi.
"Mamaaaaa tusaidieni..." Same alipiga ukunga akiita msaada, hakukuwa na mtu yoyote eneo hilo wa kutoa msaada kwa hawa jamaa. Walianza kuzama taratibu kuelekea chini wakitazamana kwa kutabasam wakijua hiyo ndiyo hatima yao.
"Kumbe na huyu jamaa kichwani hakuna kitu alikuja kunisaidia akiwa hajui kuoga ndani ya maji !.." aliongea zombi kimoyomoyo mda huo same pumzi ikiwa inakata akifumba macho yake taratibu. Zombi hakuweza kusaidia chochote maana hata yeye ndani ya maji hana ujanja.
hazikupita sekunde nyingi mala kunamzee mmoja anazamia kwenye maji na kwenda chini kabisa kina alichotaka Zombi na same.
Yule mzee alimuona Zombi akazamia zaidi na kumshika zombi ili amsaidie kutoka. Zombi hataki kusaidiwa anaonyesha hishara ya kukataa kabisa na kunyoosha kidole alipo same akiwa na maana msaada uanze kutolewa kwa same kwanza. Mzee akaenda haraka kumsaidia same na kurudi naye nchi kavu. Kisha akarudi kumsaidia na zombi.alishangaa kuona zombi hajakata pumzi licha ya kuwa alikaa muda mrefu zaidi ndani ya maji.
Mzee akaanza kutoa maji kwenye mapafu ya same aliyekuwa amepoteza fahamu mda huo.baada ya mda mchache same alitapika maji mengi na kukohowa, macho yake yakafunguka.
"Asante mungu kijana umeamka.." aliongea yule mzee aliyetoa msaada same akasimama akiwa anakohowa kohowa.
"Asante Sana mzee wangu kwa kutusaidia sijui hata nikulipe kitu gani?daah.."
"Hakuna tatizo kijana Mimi Ni mvuvi haya maeneo na nijukumu langu kusaidia watu wanao hitaji msaada nilisikia sauti ikiomba msaada nikaja haraka.ila huyu mwenzako ananitisha jinsi alivyo! .."
"Huyo jamaa anamatatizo ya ngozi usimuogope.Asante Sana mzee ukipenda twende nyumbani kwangu tukapata hata chakula cha pamoja .." aliongea same mda huo zombi ametulia tu pembeni anawasikilizia
"Hapana kijana ngoja mi niende, nina kazi nyingi.."yule mzee aliondoka pele, same anageuza macho akamtazama zombi alafu akacheka
"Aya tusepe tukapande taxi.."
zombi alisimama wakaanza kuelekea balabalani.
Walifika ilipo balabala kuu wakachukua taxi na kuanza kurudi kuelekea nyumbani.
Haikuchuka mda mrefu walifika wakashuka mbali kidogo na nyumba. Same akalipia nauli kwa dreva lakini dereva alikuwa mgumu kupokea ile nauli
"Kiongozi hii ela yako imelowa Sana naomba nibadilishie.." aliongea yule dereva kwa unyenyekevu kidogo.
"Zombi toka nje tusepe. We jamaa kaianike alafu nimekupa teni yote usinirudishie chenchi.. Zombi changamka Basi toka.." aliongea same akiwa nje ya taxi anasubiri zombi atoke. Zombi alitoka wakaanza kutembea kuelekea maskani.
Sasa wakiwa wanakatiza kwenye chocho za majirani same akasimama
"Haraka Zombi Chukua mavumbi ujichafue chafue usoni mama tony na wenzake wale pale.." aliongea seme alipoona Kuna kagenge ka wamama kamekaa ubarazani kwa mama tony wanasukana. Zombi akachota vumbi na kujipaka usoni.
Sasa ile wanakatiza tu pale alipo mama tony na wapambe wenzake
"Hallooo hehehe mfuga majini na jini wake huyo.." ilipigwa ile kelele ya umbea na mama tony.
"Habari za saizi mama tony.." same alisalimia licha kwamba alizalilishwa
"Sitaki salamu ya wachawi Mimi piteni tu.." aliongea mama tony kwa dharau Sana akaendelea kumsukia shosti wake
"Okay uwe na siku njema na usiku .." same alipita na Zombi akionekana kitopendezwa na kile kitendo
"Ety uwe na siku njema ila wachawi bwana kenzake kamejipaka mavumbi kama kajini, hahahahah.." aliongea mama tony wenzake wote wakacheka ila Zombi na same hawakua mbali sana walisikia yale maneno na vicheko.
"Yule mama hana heshima kabisa nitamfundisha namna ya kuheshimu watu.." aliongea zombi mala hii alisikika vyema kabisa kwa sauti yake nzito kidogo kidogo yenye hasira.
"Zombi naona umeongea tena hahahaha. utamfanya Nini Sasa yule mama maana hata Mimi kanike..." Aliongea same hata hakumaliza sentensi akatulia na kusimama chap akabaki anashangaa kuona gari la Mr Hance likiwa nimepack nje ya nyumba yake.
"Gari la nani lile mkuu?.."aliuliza zombi
"La bosi wangu..." Same alijibu mala mlango wa lile gari unafunguliwa akatoka Mr hance akiwa ndani ya suti yake nyeusi akageuka na kumtazama same akiwa yupo na zombi.
"Zo
ITAENDELEA.....
TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.
Maoni
Chapisha Maoni