ZOMBI WA DAR EPISODE 6
ZOMBI WA DAR
ABELUKA FILM (sika)
EPISODE 06
<>
TULIISHIA....
Mala ya mwisho tuliona Kuna ugeni mpya umeingia ndani ya kampuni ya mr hance. Wafanya kazi wote walibaki wameduaha haswahaswa linah alionekana kushangazwa zaidi baada ya kuona ule ugeni.enjoy alikuwa amesimama karibu zaidi na huyo mgeni na yeye akiwa ameshangazwa.
"Ayaaa huyu jamaa nilimwambia abaki nyumbani ona Sasa alichokifanya!!.." same aliongea bila kusikika pale kwenye meza yake ya kazi akiwa ameshika kichwa
TUENDELEE...
"we ni Nani na mbona umejipaka maunga usoni?.." aliuliza enjoy Ila zombi hakujibu alipeleka macho yake mpaka kwenye meza ya same.
"Huyu mtu ni chizi jamani mbona simuelewi kajipa kapaka maunga uso mzima Kama mtoto namuuliza hanijibu!. Walinziiiiiii...." Aliongea enjoy alafu akaita security.
"Enjoy subiri huyu ni mdogo wangu niliye mficha siku ile, anamatatizi ya akili kidogo ..." Aliongea same akiwa anasimama kwenye kiti chake na kuanza kutembea kuelekea mlangoni alipo zombi na enjoy.
"Kwa hiyo huyu ni mdogo wako uliyenificha siku ile?.."aliuliza enjoy alionekana Kama kuto amini hivi.
"Ndiyo ni dogo langu..."
"Hukumwambia kama Hapa ni sehemu ya kazi ona alivyo yani Kama kichaa unadhani baba akimkuta huyu dogo lako atafanyaje? uwe unajifikilia basi mpumbavu wewe hapa ni kazini.." Enjoy aliongea kwa kufoka Sana mbele ya same. Walinzi wakafika pale kuitikia wito wa enjoy
"Madam ulituita?.."aliuliza mlinzi mmoja kwa heshima Sana.
"Huyu kichaa ameingiaje humu?.."
Tusamehe madam hatukumuona anavyo ingia Ila ngoja tumtoe..."
"Muacheni atatolewa nje na Kaka yake nyie nendeni Ila siku nyingine muwe makini na hivi vishetani vinavyokuja kualibu hadhi ya kampuni..."
"Sawa madam .." security waliondoka pale.
"Nisamehe Mimi Enjoy nimekwambia anamatatizi ya akili kidogo, pia sikutegemea Kama ungenitukana namna hii. Asante kwa yote..." aliongea same akiwa na machungu mwanzo hakuwai kufokewa na enjoy, imekuwaje leo atukanwe mbele ya wafanyakazi wote.
"Toka nje haraka na takataka yako.." enjoy aliongea akiwa kwenye Hali ya hasira kali, same akamshika mshikaji wake na kutoka naye nje taratibu mpaka sehemu ya packing wakaingia ndani ya gari.
"Zombi ivi unamatatizo gani wewe? Umeona ujinga uliofanya hapo? nilikwambia ubaki nyumbani Sasa kilicho kuleta huku ni Nini? Aah mpaka najiraumu kwanini nilikutoa msituni yani!.."
SAA 4 ZILIZOPITA
Zombi alikuwa amelala kitandani mda huo same akiwa ameshaenda kazini. Zombi aliamini ndani ya jokofu Kuna nyama Kama alivyoambiwa na same hivyo alikuwa anasubiri njaa ianze aende kula msosi wake. Baada ya mda mfupi kukaa kitandani njaa ikaanza kumshika kwa umbali akaona ni Bora akale mapema kuliko kusubiri njaa kali imkumbe Pengine atashindwa kujicontor na kwenda kukiwasha huko kwa majirani. Aliinuka kitandani na kwenda kufungua jokofu, Alipigwa na butwaha kuona jokofu halina nyama.
"Inamaana jamaa amenidanganya?.."
kwa usalama wa majirani zombi aliamua kumfuata same kazini kabla njaa yenyewe haijakolea.
kabla hajaondoka alijipaka unga mwingi usoni ili ngozi yake halisi isionekane kwa watu. kupitia harufu anauwezo mkubwa wa kunusa na alikalili Sana harufu ya same hivyo alifika kirahisi pale ofisini kupitia harufu ya same.
SASA HIVI
"Huyu jamaa anielewi nimekuja huku njaa inaniuma, chakula sijakiona kwenye jokofu nitafutie nyama haraka kabla sijabadilika changamka Basi mi sitaki kudhuru watu!..." Zombi aliongea moyoni kwa msisitizo akimuonyesha same kwa vitendo alikuwa anashika shika tumbo kuonyesha njaa.
"Unataka kusema njaa inakuuma? Lakini nilikuachia chakula kama chote njaa inaanzaje tena Kama sio usumbufu..." Same alikuwa bado mgumu kumuelewa zombi,aliinamia usukani na kuendelea kufikiria Mambo mengine kuhusu enjoy.
"We jamaa Nitafutie chakula haraka Hali yangu inaweza kubadilika Sasa hivi mbona hunielewi.."zombi aliendelea kusisitiza kimoyoni same hakuelewa hata kimoja alikuwa kwenye strees zake za mapenzi mpaka macho ya zombi yakaanza kubadilika na kuwa mekundu mda huo wakiwa ndani ya gari. Mala hii same strees za mapenzi zikapotea baada ya kusikia muungurumo wa Zombi Kama amepandisha kichaa hivi.
"Ohoooo inamaana mshikaji njaa ilikuwa inakuuma live?.." same aliongea akiwa anarudi nyuma taratibu alipoona macho ya zombi yameiva rangi .
Same akafungua mlango wa gari haraka haraka na kutoka alafu akamfungia zombi ndani ili asitoke. Sama akaanzidha mbio kwenda mpaka hotel Moja iliyokuwa karibu na pale kununua nyama.
Huku ndani ya gari zombi amepandisha mzuka mkali anapiga piga kioo mpaka kinaachia nyufa na kuanguka, anasukuma mlango wa gari unaenda chini moja kwa moja(paaaa) alafu Zombi sasa NDO anatoka akiwa na njaa kali.
Walinzi waliokiwa maeneo Yale wakamuona
"Nini kile?.." walinzi wakaandaa bastora zao baada ya kuona Zombi amechomoa mlango wa gari alafu anaelekea walipo wao.
"Tufyatue risasi kabla hajatufikia anaonekana sio binadamu huyu..."
"Tulieniiiiiiii..."same Alitokea kwa kukimbia mkononi akiwa na kifungashio Cha nyama akaenda kusimama mbele ya zombi.
"Nyama hii apa mshikaji twende kwenye gari ukale.." aliongea same kwa woga kidogo akimuonyesha zombi kifungashio Cha nyama. Zombi akakivuta kile kifungashio na kuila nyama kwa fujo mbele ya umati wa walinzi na baadhi watu waliokuwa nje ya kampuni.
"Ayaaaa anafanya nini huyu mjinga!!.." same hakuwa na kitu Cha kufanya alijikuta anatazama tu namna nyama mbichi zinavyo liwa.
"Same huyo ni binadamu kweli?.." aliuliza mlinzi mmoja akiwa amesimama na wenzake wakiwa bado wameshika siraha
"Huyu ni chizi alafu nimemtoa Kijijini kwa hiyo kula nyama mbichi kawaida kwake msijali shusheni siraha zenu..." Same alijitetea hadharani Tena aliongea kwa ujasili akiwa anamsubili zpmbi amalize kula.
Zombi alimaliza nyama akili zikamrudi akainuka taratibu akiwa anatazama kushoto kulia namna watu wanavyo mshangaa
"Inamaana nimeharibi tena?.."
"Naona akili zimekurudi Sasa. twende kwenye gari Watu wanakushangaa.." same alimbeba zombi na kuelekea ndani ya gari.
"Huu sio ustaharabu kabisa kwa hiyo ameamua uvunje na mlango wa gari!..." Same aliongea akiwa anainua mlango wa gari na kuweka nyuma ya buti. Hakuwa na namna aliacha gari pale na kusimamisha taxi. Wakaingia pamoja na zombi ndani ya taxi.
"Kaka mnaelekea wapi?.." aliuliza dreva kabla hajaondoa gari.
"Tupeleke baharini..."
"Huyu jamaa anataka twende baharini kufanya nini tena? .." zombi alijiuliza moyoni. Taxi ikaanza safari kuelekea beach.
NDANI YA KAMPUNI
"Nyie wadada kumbe same anaishi na kichaa hahahaha nayeye MDA sio mrefu akili zitamruka .." aliongea sadiki jamaa ambaye hapendi same mda huo linah alikuwa pembeni ametulia kimya akionekana kuwa mwenye mawazo sana baada ya kumuona zombi
"Linah unatatizo gani mbona sio kawaida yako kukaa kimya?.." aliuliza sadikiakini linah hakujibu kitu alitoka nje na kupiga simu..
"Hallo bosi hance naitaji kukutana na wewe Sasa hivi..."
"Sawa njoo hapa hotel nipo napata lunch.." aliongea Mr hance na kukata simu.
Linah bila kupoteza mda alichukua gari lake na kwenda hiyo hotel aliyoambiwa. Hotel haikuwa mbali na pale alifika haraka sana na kuingia ndani ya hotel. na kweli alipoingia kwa mbali alimuona Mr hance akiwa mezani na binti mmoja mdogo mrembo.
"Suzi nenda tutakutana baadae.." Mr hance alimwambia yule binti aliye kaa nae baada ya kumuona linah amefika. Suzi alisimama mezani akambusu Mr hance mdomoni na kuondoka.
Linah akafika pale na kukaa kile kiti alichotaka suzi.
"Samahani bosi kwa usumbufu..'
"Ongea haraka kilicho kuleta hapa.."aliongea Mr hance akiwa ameshika grass ya maji anataka anywe.
"Bosi ni kwamba.."
Ni kwamba nini?.."
"Rajah hajafa ni mzima.." aliongea Linah Mr hance akadondodha grass ya maji.
ITAENDELEA....
Mpaka hapa mambo ni fire moto!!! Huyu Linah maneno mengi anamjua Zombi!! tena amelitaja jina la Zombi mbele ya bosi wake!!! Hawa Watu wawili wanasiri yao....tutaijua tu hakuna siri chini ya jua..
TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO
Maoni
Chapisha Maoni