JUNE 17 EPISODE 7 MWISHO



JUNE 17

EP 7 Final

S.P. Owino

Judi alifumbua mdomo wake akawaambia Askari twende nikawaonyeshe hao watoto! Mchungaji alifurahi kwani Sasa Judi anaweza kuongea japo mdomo umejaa dam kwa vidonda.
Askari wengine walionywa wasitoe taarifa yoyote kuhusu watoto walio potea, kwani uchunguzi bado iwapo wale wazazi watarudi!! Waliingia ndani ya gari wakaanza Safari kuelekea tukio lilipo tokea Yani anapoishi Judi, Safari ilikua ndefu kidogo.
Ilikua saa 6:12 mchana
Hatimae walifika Judi alishushwa lakini getini alienda kugonga askari, hodi! Hodi! Baada ya mda kidogo mzee Mathias alifungua mlango Judi akiwa kwenye gari alimuona mzee yule, roho ilimuuma kwani alihisi anawasababishia matatizo! Askari walitengeneza mchezo wakidai wamemuokota Judi akiwa katika hali mbaya na amesema hapa ndo kwao, hivyo wanahitaji kuingia kukagua yawezekana yapo mazingira yalio mchochea yeye kuondoka nyumbani.
Mzee Mathias alikua haelewi chochote aliwaruhusu waingie, Ila alishangaa alipo muona Judi yupo katika hali mbaya anamajeraha yaajabu mdomoni. Alihitaji kumuuliza lakini alizuiliwa naaskari. Alipo hojiwa alidai yeye pamoja na mkewake walisafiri kidogo wakamuacha Judi nybani, kumbuka mzee Mathias amesahau Kama Alisha Wai kua na mtoto sijui kipi kilicho tokea labd huyu mama ndo kasababisha!!?
Mkewake aliingilia akadai labda Judi alirukwa naakili, Judi akafunguka kwamba yeye aliachwa nyumbani amlee mtoto mdogo walio mzaa lakini yule mtoto aliwaua wenzake wote waliokuja kumsalimia.
Polisi waliangaliana nahisi walidhani Judi amerukwa naakili, Ila waliitaji kuhakikisha Kama hii familia ilishawai kua na mtoto, waliwaomba mzee Mathias pamoja na mkewe wabaki nje.
Mule ndani waliingia Askari poja na Judi, Judi moja kwa moja aliwapeleka chumba alipo kua akilala mtoto chaajabu wanafungua wanakuta ni store Tena inaonekana store ya mda mrefu tu! Pastor alishangaa nae alianza kumtilia Shaka judi. Judi aliwahi sebleni aliifungua kabati akaitoa album inayo beba picha, pia alipo fungua yule mtoto haonekani!
Judi aliamua kukaa akaituliza akili yake alihisi atakua yupo ndotoni, polisi walikaa kwanza wapo wapioona Kama nimichezo wakiangaliana na kucheka.
Ile nyumba sio ghorofa Ila Kuna ngazi inayopanda Kama inaelekea juu ya Dari sijui ilijengwa kwaajili gani. Wakati pastor akiwa bado hajaridhika na kile alicho kiona aliiona ile ngazi, Ila pia pastor alikua bado anamaumivu ya ajali aliyo ipata. Alipanda pale kwa uangalifu rohoni alihisi kunakitu kule juu alipanda Ila kila alipo zidi kupanda alizidi kuingiwa na wasiwasi! Alipo fika juu, Yani ile ngazi ilipo ishia hapakuwepo kitu Ila dirisha dogo lililo kua wazi.
Pastor aliamua kurudi chini lakini aliingiwa na msukumo wakutazama chini kupitia lile dirisha, nandipo alipoamua kutazama. Alipo chungulia chini alikiona lile kisima ambacho kiliwai kuchimbwa Ila hakikutoa maji. Alipo tazama pembeni aliona Kama kiatu chamtoto mdogo!!
Alishuka haraka bila kuongea na mtu mpaka pale kilipo kile kisima, aliitaji kuchungulia mule ndani kwani aliona kiatu cha mtoto kwa pembeni kabla hajachungulia yule mama aliingia akamwambia "hapana tumewapa Uhuru kukagua ndani hukunje kunanini" yule mama alikua mkali kweli. Alimuondoa pastor eneo lile, pastor alionyesha Kama hakuna alicho gundua akamwambia hapana mimi nimemaliza uchunguzi ndomana nipo huku nje napunga upepo. Yule mama alionekana kupumua kwani alihisi pastor kagundua chochote!
Ila pale chini pastor kaona kiatu cha mtoto mdogo Ila pia kunakitu amehisi kimo ndani ya kisima aliondoka bila kunionyesha chochote, yule mama alibaki eneo lile.
Pastor alirudi ndani akamuita Judi pembeni, mdahuo polisi walikua wakiongea na mzee Mathias wakijaribu kumuomba radhi kwa usbufu ulio jitokeza. Pastor alimwambia Judi humu ndani ya hii nyumba kuna kitu kinaendelea, na hata Mimi nimekiona. Alimuomba Judi aondoke arudi kwao kabla mambo hayajawa mabaya. Judi alisema narudi vipi nyumbani? Pastor alimuuliza huyu mtoto baada ya huyu mama kujifungua alimtaarifu mtu yoyote?
Judi alijibu hapana aliomba iwe Siri mpaka ipite miaka mitatu, na hakuitajika mtu yoyote kumuona sura wageni walipo ingia walimficha mtoto sikunzima! Yule pastor alimwambia Sasa Leo usiku jiandae kesho huyu mama ataamka mapema akiamka nitumie sms nitakwambia chakufanya. Judi alishangaa Yale anayo ambiwa na pastor!
Polisi, pastor waliaga wakaondoka, hapohapo kwa haraka yule mama akizunguka nyuma ya nyumba yake akakichukua like kiatu akakisukumia kisimani!!
Ilikua saa 12:45 jioni!!!
Pale nyumbani kulikua kimya mama na mzee Mathias walionekana hawana furaha namimi, nilipo ingia jikoni kuandaa chakula mama alinizuia alisema ntaanda mwenyewe.
Ile siku ilikua ngumu Sana kwangu, tulilala
kweli ilipo fika mida ya saa 10 alfajiri sio kawaida mama aliamka alionekana akiwa na haraka kilikuwepo gari aina ya pickup aliliwasha, hapo nami nikamtumia sms mchungaji kwamba mama ameamka. Mchungaji aliniambia nakuja Sasa ivi wewe jiandae Ila panda ile ngazi ukachungulelie kwa dirishani anafanya Nini pale kisimani.
Kamavile pastor alikua amesha ielewa akili ya mama, kwelinilipaanda haraka nikafungua lile dirisha taratiibu nikijitahidi asinione. Mama aliisogeza ile pickup mpaka eneo lile la kisima alitoa Yale yalio ziba kisima naalionekana Kama kunakitu anavuta, looo sikuamini nilicho kiona alikua akivuta miili ya watoto wadogo kumbe inavyo onekana Wana ndoa Hawa Kuna kitu walifanya ili kuufucha ukweli kuhusu kile kilicho tokea.
Du! Kumbe mmewake pia analifaham ili swala "mzee Mathias" alileta madiaba makubwa yakuwekea maji yakiwa na mifuniko, waliingiza ile miili ya watoto mule ndani wakafunga Kisha wakasaidiana kubeba Yale madiaba na kuyapakia ndani ya pickup!!
Sikujua wanapo elekea Ila nilihitaji kupiga sim polisi japo mchungaji alinizuia!!
Mchungaji alikimbiza gari kuwai pale nyumbani, geti lilifunguliwa mzee Mathias pamoja na mkewake wakiwa ndani ya pickup nyuma yakiwepo madiaba makubwa mawili waliya funika kwa mashuka ili watu wasishtilukie!
Waliwasha gari wakaondoka sikujua walikua wakielekea wapi Ila nilihisi walikua walienda kuizika ile miili ili kuficha ushahidi! Niliwai getini kutazama walipo elekea
Ilikua saa 11: 15 alfajiri
Mda kidogo polisi walifika nawalionekana kuniamini waliniuliza wameelekea wapi nikawaambia, waliondoka kuwafuata. Mdakidogo pastor alifika, kumbe alikua amenikatia ticket ya kwenda nyumbani aliniomba nikafuate mabegi yangu ndani nakuchukia Kila kilichokua changu. Akinisiaitiza pale ni hatari Sana, alinisindikiza mpaka stendi nikapanda Basi lakwenda mikoani!! Nilimuaga pastor Ila hakujua Kama nilisha waita polisi, ilibidi pastor awashe gari kurudi walipo elekea mzee Mathias pamoja na mkewe.
Nikiwa ndani ya Basi nilijua lazima pastor atanitafuta kunilaumu kwanini niliwaita polisi, niivunja ile laini na sim niitupa nikiwa safarini!
Hatimae mzee Mathias pamoja na mkewake walifika eneo la mtoni wakasimamisha gari waliyashusha Yale madiaba makubwa mawili wakaitoa ile miili ya watoto nakuanza kuitupa majini walifanya vile kwa haraka ili pasi kuche wakakutwa pale.
Waliyaish ayale madiaba ohoo za mwizi ni arobaini polisi walikua wakitazama Yale yote..
Pastor anachelewa kufika anakuta tayari wamesha kamatwa na ile miili polisi waaliitoa Kama ushahidi, mahakamani. Alipo jaribu kupiga namba ya Judi haipatikani...,.....,
Zilipita wiki mbili pastor aliwatembelea mzee Mathias pamoja na mkewake mahabusu wakisubiria hukumu! Alipo fika walionekana kua dhaifu sijui pastor alikua nampango gani na Hawa watu kwani hakutaka polisi walijue like jambo.
Alimuuliza mama alimpataje yule mtoto yule mama alimuelezea kwamba alipo olewa familia ya mme wangu ilinikataa baada ya miaka miwili ya ndoa bila mtoto, hivyo niliamua kusafiri Kama mwezi haikujulikana nilipoelekea lakini nilipo rudi baada ya mwezi mmoja niipata mimba!
Alisema huko alipo kwenda alipewa masharti kwamba atapata mimba lakini huyo mtoto asione Kane mpaka afikishe miaka Saba!! Pastor alikua sababu ya yule mama kuyafanya yote yale!
Kule mahabusu walikuwepo wazazi wawanandoa wale wengi walikua wakilia tu! Pastor alimuuliza yule mama akimuomba aukubali wokovu yule mama akitoa machozi alisema anahisi hatia na haoni Kama Mungu anaweza kumsamehe! Ila mchungaji Ali mwambia hakika utaupata wokovu na hakika roho yako haitapotea!!
Wiki moja baadae hukumu ilitoka na mzee Mathias pamoja na mkewake walihukumiwa kifo!!!!
Ile ilikua taarifa nzuri kwa wale wazazi walio wapoteza watoto wao Ila sio kwa wale wazazi wa mzee Mathias pamoja na mkewake!!
12/9/2008 mzee Mathias alinyongwa mpaka kufa Ila mkewake alisubirishwa na mahakama kwani alionekana ni mjamzito, lilikua Jambo la furaha japo alijua baada ya kujifungua ata nyongwa mpaka kufa, Ila moyoni mwake akiamini Mungu amemsamehe!!!!!
Miezi 9 baadae, mama alijifungua na yule mtoto alivhukuliwa na familia ya mzee Mathias.
Tarehe 23/7/2009 mama alinyongwa mpaka kufa.....

********END********


TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: BINAMU 🔞 SEHEMU YA 11

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 1-5

CHOMBEZO: MASSAGE ROOM🔞 SEHEMU YA 21