MGENI KUTOKA MJINI SEHEMU YA 1
SIMULIZI:MGENI KUTOKA MJINI
MTUNZI:SHAX GOLD
NO :.001
Simulizi yetu ina anzia morogoro katika kituo kidogo cha mabasi alishuka bwana mdogo mmoja wa kama miaka 23 ivi alishuka kwenye basi uku mgongoni akiwa kavalia begi lake la nguo tu kama yale ya wanafunzi wa shule ali tazama mbele akamuona dereva wa boda boda akiwa amepaki boda boda kivulini na yeye akiwa amelala kwenye gogo.
“Daaaaaah!! Yani watu wanatoka kijijini wana enda mjini kuta futa maisha mimi natoka mjini nakuja kijijini kuta futa ama kweli..”
Bwana mdogo uyo alijisonya mwenyewe pale Kisha akaenda adi pale Alipo kuwa yule dereva wa boda boda kisha aka muelekeza mpaka anapo taka kwenda basi wali tembea kama nusu saa ivi wakawa wamefika kisha bwana mdogo alizamisha mkono wake mfukoni na kumpa yule dereva wa boda boda hela yake akawa sasa ana tazama wapi pa kwenda.
“Sasa nyumba yenyewe ndo ipo wapi.? Maana kitambo Sana daah!!!”
Wakati bwana mdogo ana jiuliza maswali bila ya majibu kumbe kwa nyuma yake alikuwepo mama wa kama miaka 60 naa yani tuseme ni mbibi tu ila wa makamo maana bado ana nguvu zake. Basi yule bibi alivyo muona yule kijana alipiga vigelele ile Mbaya.
“Heeee alluuuuu wee! Mzee mrisho mzukuru wako kaja uku....!”
basi yule bibi alitupa jembe lake na kwenda kumu wai mjuu wake na mjukuu wake alivyo sikia tu vile aligeuka ile ana geuka tu bibi yake huyu apa amesha mkombatia uku akifurahi na kumsalimia basi kijana alifurahi vibaya mno maana angepotea kabisa maeneo yale basi bibi alipokea lile begi na kwenda nae sasa kwenye mji wake maana pale walipo kuwa wamesimama apa kuwa kwake basi mzee mrisho nae alitoka ndani uku akivuta sigara yake alitoa kwanza sigara yake kisha akamsalimia mjuu ake.
“Ujambo mjukuu wangu..?” mzee mrisho alimsalia mjukuu wake uku akiwa amesimama mlangoni.
“Sijambo babu shikamoo...!”
“Marhabaa bibi mrisho nenda basi kalete stuli...”
Basi mzee mrisho alimpisha mkewe pale mlangoni aka ingia na lile begi ndani kisha akatoka na stuli aka zitenga pale njee moja kwajiri ya mjukuu wake na nyengine ya mume wake kisha yeye akaingia zake ndani.
“Karibu sana mjukuu wangu...”
“Asante sana babu nimesha karibia..”
Wakati wakiwa wana endelea kupiga pale story mbili tatu kidogo bibi mrisho akatoka na sinia limejaa ubwabwa na maharage akatenga pale kwenye ndoo aliyo toka nayo kisha akaenda kuchukua na maji kwenye jagi akatenga pale kisha akarudi zake ndani baada ya kuwa karibisha chakura.
“Mjukuu wangu we kura kwanza Mimi ngoja nimalizie sigara yangu apa japo nimesha kura tayari ila nita kusaidia kidogo japo matonge mawili...”
“Amna shida babu usijari..” basi mzee mrisho alivuta sigara alivyo maliza aka anza kura na mjukuu wake ambae mpaka sasa atuja mjua jina lake baada ya kumaliza kura pale mzee mrisho ali mwambia mjukuu wake.
“Mjukuu wangu jeydan, apa sasa kwakuwa tumesha kura itabidi twende hapo kwa rafiki yangu mmoja mzee nyange akupe hifadhi angalau siku kazaa ili nikujegee banda lako uwe unalala hapa..” mzee mrisho aliongea uku akimtazama mjukuu ambae anaitwa jeydan.
”Sawa babu aina shida..”
Basi mzee mrisho aliinuka pale waka muaga bi mrisho kisha waka anza safari ya kwenda uko kwa mzee nyange uku wakipiga story mbili tatu. Sasa njiani walipo kuwa wanapita alikuwepo mshikaji furahi ivi anae julikana kwajina la juma mbavu alikuwa amesimama na mtoto mzuri anae julikana kwajina la devota. Basi juma alikuwa ana saundisha uku akigeuza mgongo barabarani alafu devota alikuwa ana tazama kwenye barabara basi juma alikuwa anatema swaga mda uwo devota akingata kucha mara achume maji uku ana tazama chini kwa aibu kama unavyo jua tena wanawake wakijijini wakiwa wana tongozwa jeydan na babu yake walipita hapo hapo uwezi amini devota alivyo muona tu jeydan alijikuta kapata ujasiri wakufa mtu maana alitokea kumpenda gafra tu jeydan alivyo muona.
“Juma sikia ni kwambie sikupendi na sikuitaji..!! Kisa na kungatia kucha hapa usijue na kupenda sana tena na kwambia unikome..!!”
Devota aliongea kwasauti adi babu yake jeydan na jeydan waka sikia wakawa wanacheka devota alichukua ndoo yake aka ishika vizuri ngata yake kisha akaondoka akimuacha juma akimuita tu kwa nyuma lakini asigeuke devota alienda walipo kuwa marafiki zake kama watatu ivi na yeye wanne wakaondoka zao..
ITAENDELEA.......
TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.
Maoni
Chapisha Maoni