SAA ZA MWISHO EPISODE 6



SAA ZA MWISHO

EP 6

S.P Owino

Hii nisiku ya nne katika familia yangu hakuna Alie fahamu kwamba ifikapo siku ya tano, kwamujibu wa yule nesi anae nitokea usiku nitafariki! Niliamka asubuhi sikuhi nilikua nauwezo wa kutembea hivyo niliwaomba madaktari waniruhusu niweze kutoka nje! Lakini nilikumbuka sharti alilo nipa yule nesi! Kwamba sitakiwi kuuvuka lango wa hospitali!
Waaaa! Nilijisikia raha Sana nipo nje namwanga wajua ulikua mzuri asubuhi ile nilitamani kuishi nje, kwakweli haliyahewa ilikua nzuri. Niliamini Yale yote niliyo ambiwa na yule nesi yalikua uongo! Niliona Kama ndoto tu! Ilikua furaha kwangu machozi ya furaha yalinitoka nikikumbuka hata ugonjwa niliokua nikiugua walipo upima haukupatikana! Nilitamani niondoke pale hospitali mdaule!
Kuna familia moja ilikua ipo ndani ya gari ilionekana ikielekea kule kijijini, ilionekana Kama familia yakitajiri ndani ya gari alikuwepo alieonekana Kama baba wa familia mama watoto wa wili pamoja na dereva, wakati wapo jiani Yale mazingira yalionekana kua mapya kwao.
Walipishana na mwanamama Alie vaa hovyo na miguuni alikua peku kidogo wgonge kwani alionekana Kama anaongozwa na mtu au watu!! Waliendesha gari walipofika mbele kidogo njia walio izoea ilikua imeota kichaka, walisimama ilibidi baba ashuke alipo jaribu kutazama hakuona njia nyingine lakini walikumbuka walimuona mtu nyuma ilibidi warudi kumuuliza Kama anaifaham njia mpya!
Apa kijijini watu waliamua kurudi walikusanyika baada ya kumkosa mamdogo walipo fika nyumbani lile eneo walilo fukua kaburi la Bibi pamejifunika Kama hakujawai hata kukwaruzwa! Kila MTU alishika mdomo wapo walio ogopa wakaamua kurudi makwao, Sasa mama baada ya vitu kutulia kidogo, mama alimrudia Kaka kwanini amewaita polisi! Aligombana na Kaka lakini Kaka aliomba samahani.
Baadae Kaka alipoona kelele zimezidi aliamua kuingia ndani!! Alijifungia kwenye chumba cha store akijaribu kuwaza Nini kinaendelea. Ali Anza kusikia mitikisiko aliamka kuufuata alipo toka alisikia sauti chumba kile kilicho fungwa, alijaribu kufungua aingie lakini alishindwa alianza kuupiga teke ule mlango mama wajomba waliingia wakamuuliza Nini shida alisema hiki chumba Kuna mtu!
Aliwaomba watulie walipo tulia kweli waliisikia sauti kama aliyo isikia Kaka waliamua kufungua mlango, duh!!
Wanakutana na mwili wa Bibi umeharibika upo juu ya kitanda wakaanza kushangaa ninihiki kinaikuta familia hii! Waliusogelea ule mwili taratibu wakaugeuza kwani ulikua umelala kifudifudi! Walimgeuza chali! Harufu ilikua Kali Kaka aliupiga picha ule mwili! Watu walitoka kwasababu ya harufu Ila ilibaki Siri kwa Wanafamilia, baada ya mda mfupi mama alianza kulia kwani ile hali ilimkumbusha Mama yake mzazi!
Aliamua kurudi chumbani alipofika anaukuta mwili upo kifudifudi!! Alipiga kelele!
Hii familia iliamua kurudi kumuuliza yule mama walie pishana nae barabarani kuhusu njia ili waende kijijini walimfukuzia kwamda hatimae walimuona kwa mbele kidogo akitembea vilevile akiwa ameangalia chini, walimaogelea Ila dereva alionekana kuogopa Sana walipo mkaribia dereva alisimamisha gari sijui Nini kilicho mstua!
Baba wa ile familia alishuka akaanza kumuita "we dada! We dada! Lakini alikua hasikii huyu baba alikua Hana wazo, mama wa familia alimuuliza dereva upo sawa dereva alimwambia hapana aka muuliza shida Nini, dereva alimjibu tazama nyayo za huyu dada kila akipiga hatua zinatokea nyayo zaidi ya kumi na nne!! Chini!! Yule mama kweli alipo shuka chini ya gari anakuta nyaro nyingi lakini anae onekana ni mmoja.
Alipiga yowe kumuita mmewake arudi haraka!!



ITAENDELEA.......



TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: BINAMU 🔞 SEHEMU YA 11

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 1-5

CHOMBEZO: MASSAGE ROOM🔞 SEHEMU YA 21