ROHO YA KUZIMU SEHEMU YA 1
STORY:-ROHO YA KUZIMU
PAGE YA:-1
MWANDISHI:-AMANI KUYELA
Karibu sana katika mfululizo mpya wa simulizi hii iliyojaa mpangilio wa mikasa na matukio ya kutisha katika ulimwengu wa roho, kwa wanao amini uwepo wa ulimwengu huu basi nakuja kukujuza elimu dunia katika mtindo wa sanaa ya fasihi andishi nakusafirisha hadi ndani ya ulimwengu huu wa roho kujulikanako kama kuzimu usioweza kuonekana kwa macho ya kawaida ya kibinadamu.
Naam, ambatana nami mwandishi wako AMANI KUYELA niweze kukusogezea yale usiyoyaona katika hadithi zingine, story ndo kwanza bado mbichi kabisaa.
Baada ya utangulizi huo, sasa twende mzigoni.
Ikiwa ni siku nzuri sana ya al hamisi, katika mitaa ya soko kuu la manispaa ya kahama mjini anaonekana mwanadada akiwa amevalia mtoko maridadi kabisa. Mwanadada huyo aliyepanda hewani futi kadhaa zenye ujazo huku umbo lake likiwa lakuvutia lenye muundo wa aina yake, na sura yake ikiwa ni ya kumvuta bwana shitete kutoka huko pangoni, mwanadada huyo akiwa na mchanganyiko wa udongo wa mjini kigali rwanda pamoja na udongo wa kirangi kutoka makao makuu ya nchi mjini chamwino.
Mwanadada huyo akiwa amevalia nguo nadhwifu zenye rangi nyekundu huku zikiwa zimebana na kuzidi kuonyesha mchoro wa umbile lake namna mola alivyompa mvuto wanamna yake, kutokana na nguo zake kuwa zimebana kwa nyuma na kupelekea matamanio kwa kila mwanaume aliyejikuta akitupa jicho lake kutizama umbile la mwanadada na sasa watu wengi waliokuwepo mule sokoni wakazidi kuonekana wakikodolea macho kwa umakini kuona ni wapi mwanadada huyo anaenda kuishia.
Baada ya muda kidogo, mwanadada akaonekana akiingia ndani ya soko kuu la manispaa ya kahama, alipoingia ndani ya soko, basi kila mwanaume aliyemtupia jicho alijikuta akirudia rudia kumuangalia namna nyuma umbo lilivyochorwa likachoreka, basi mwanadada akafika hadi katika meza moja ambapo palikuwapo msichana mdogo mwenye miaka 13 akiwa anauza genge la mama yake kwa kua siku hiyo mama yake hakufika sokoni.
Yule mwanadada mwenye asili ya kinyarwanda akawa anaulizia vitu vilivyokuwa pale juu ya meza, akanunua samaki mkubwa wa kukaangwa kisha akafungashiwa na mazaga zaga mengine ikiwa ni pamoja na nyanya,hoho,karoti pamoka na limao kadhaa.
Wakati bado yule mwanadada akiwa amesimama pale kwenye ile meza akijaribu kununua kila alichohisi ni muhimu kwake, wakati anaendelea kuchagua mara akaonekana mwanaume mmoja aliye na urefu wa futi kadhaa kwenda hewani akiwa anaingia ndani ya soko la manispaa ya kahama, alipoingia ndani ya soko, akaonekana kuwatia wasiwasi watu wengi kwa namna alivyovalia mavazi, kwa kuwa alikua amevaa suruali nyeusi aina ya kadeti huku akiambatanisha na viatu supar black vyenye muundo wa American boot, alikua pia kavaa koti jeusi refu sana lenye kufika usawa wa magoti akiwa amelifungua zipu wazi upande wa mbele, na kwa juu alikua amevalia miwani supar black pamoja na kofia cape nyeusi.
Kwa hakika alionekana kunukia harufu nzuri sana ya marashi ambayo yalimfanya, kila meza anayopita mule sokoni basi watu wanaduwaa kumuangalia yeye
Sasa wakati yule mwanaume anatembea taratibu katika njia finyu zilizojaa watu wanaopishana pishana mule sokoni, alipotupa jicho upande wa pili akamuona yule ,mwanadada akiwa amesimama kwenye ile meza akifanya mahemezi yake.
Kidume alipoona toto limenona na kukata kila idara, bila kusita akaanza kujipenyeza katika njia njia za mule sokoni huku akiwa ameweka mikono yake katika mifuko ya lile koti lake jeusi akitembea kwa kujiamini utazani watu wasiojulikana.
Kidume akamsogelea yule mwanadada, kabla hajamfikia basi yule bidada akajikuta akigeuka nyuma kutizama ni nani haswaa anapita na harufu nzuri kiasi kile kwa kua yale marashi yalipenya moja kwa moja hadi katika kuta za kingo ya moyo wa mwanadada, akajikuta anaingiwa na hisia za ajabu za upendo.
Mwanadada akamuona kidume akiwa anajongea taratibu kabisa mithiri ya kamanda mwandamizi wa jeshi la urusi,
Alipomuona tu pale pale bidada akajawa na hofu kubwa moyoni mwake kwa namna jamaa alivyokuwa anatembea kama afisa flani wa usalama wa taifa, basi kidume akamsogelea kabisa bidada kisha akasema
"Mambo vipi sister"
Bidada kwa woga na kitete ndani ya nafsi yake akaitikia huku sauti yake ikiwa na mitetemo ya hofu akasema
"Safi tu, habari yako bro"
Kidume akajibu
"Niko njema sana sister, naona uko unachukua mazaga ukaandae msosi"
Bidada akiwa bado na hofu huku akimuangalia kwa jicho la sitaki nataka akasema
"Eeee, bro si unajua tena mambo ya madiko diko"
Kidume akatabasamu kisha akawa anamungalia machoni yule dada, lakini dada naye akajitahidi kadri anavyoweza kurudisha taswira ya muonekano wa kupokea japokuwa ndani ya nafsi yake alikua bado anajiuliza maswali mengi sana juu ya yule mwanaume kwa kua alionekana kua na asili ya kisomali akawa anahisi labda anaweza kuwa jambazi ama gaidi na kutokana na namna alivyovaa ilikuwa ikizidi kumtia wasi wasi mwingi sana yule bidada.
Ikapita kama dakika moja ya ukimya huku kila mmoja akijaribu kumsoma mwenzake, basi yule bidada akamuuliza yule muuzaji iwapo anamdai kiasi gani, muuzaji akamjibu ametumia elfu kumi na mbili na mia saba, basi bila kupoteza muda bidada akazamisha mkono wake ndani ya pochi yake ndogo yenye rangi ya pink aliayokua ameishikilia mkononi, akatoa shilingi elfu kumi na tano kwa ajiri ya kumpatia yule muuzaji.
Lakini wakati tu anataka kulipia, pale pale yule jamaa kamzuia na kumuambia asilipe chochote yeye ndiye atagharamia kile anachodaiwa,.
Mwanaume akazama ndani ya mfuko wake akatoa waleti kisha akachomoa noti tatu za elfu kumi kumi zikiwa zimenyooka utazani zimepigwa pasi, yani unaweza hata ukakatia nyanya kwa namna zilivyokua mpya yule kidume akampatia yule mmuzaji shiling elfu 30 , yule bint muuzaji akapokea na kumuuliza iwapo anahitaji kununua kitu kingine lakini kidume akamjibu, anahitaji ndizi za elfu mbili tu na chenji inayosalia atabaki nayo muuzaji.
Walipomaliza kufanya malipo, mwanadada akataka kumuaga yule jamaa kwa kumshukuru sana kutokana na alivyomsaidia kumlipia, lakini yule mwanaume akawa bado anashauku ya kutaka kuambatana na bidada watoke wote ndani ya soko, bila kusita mwanadada akamkubalia wakaanza kutoka ndani ya soko huku wakiongea mawili matatu, walipofika nje ya soko bidada akamuaga kisha akataka kuita bajaji ili apande na kuelekea nyumbani, lakini jamaa akamuambia asiite atampakiza katika gari yake na kumpeleka hadi anapotaka. Bidada aliposikia vile akauliza.
"Kumbe upo vizuri eeee, unagari kabisa"
Yule mwanaume akamjibu akiongea kiswahili chenye mchanganyiko wa rahaja ya kisomali,
"Yes sister, niko namchuma wangu ule pale"
Bint akatabasamu kisha akakubali lakini rohoni mwake akawa bado hamuamini amini yule mwanaume, ikambidi tu akubali kishingo upande, jamaa akasoge hadi alipopaki gari yake yenye mvuto na hadhi ya kitajiri, ilikua ni gari nyekundu ambayo kila aliyeiona pale parking alijiuliza ni mtu wa hadhi gani anayemiliki gari ya thamani kiasi kile.
Jamaa akafungua akaingia ndani ya gari kisha bidada naye akafungua upande wa pili nakuingia wakaanza kutoka sokoni, wakati wanaenda njiani mwanadada akawa anamuangalia yule jamaa kwa jicho la nataka sitaki huku akifurahia harufu nzuri ya marashi ya kipekee yaliyokua yameshamiri ndani ya gari, yule mwanaume akamuuliza bidada
"Sorry sister ni vyema tukifahamiana japo kwa uchache, unaitwa nani na unastay mitaa gani?"
Bidada akiwa anatabasam akajibu
"Naitwa Zehera naishi mitaa ya kule chini chini uswahilini panaitwa mtaa wa mtakuja,".
Jamaa akasema
"Ooohh well, sipafahamu kabisa since mimi huja huku kufanya connection za biashara ila sana sana huishi mombasa kule kenya, na this time nilikuja kwa hapa kuna mission nafatilia".
Bidada akauliza
"Woooow, kumbe huishi tanzania?, mimi pia mama yangu ni mnyarwanda ila baba alikua akiishi dodoma bahati mbaya alifariki nikiwa mdogo sana, na isitoshe mama naye alipatwa na matatizo ya presha na stroke kwa hiyo mimi ndiye nikabaki kutafuta riziki kumsaidia, na kwa sasa yeye yupo nyumbani dodoma nawadogo zangu watatu"
Yule mwanaume akajibu
"Polee sana Zehera nadhani, huu utakua mwanzo mzuri wa kujuana, mimi naitwa Hashiru nimkurugenzi katika kampuni ya ST general enterprises ipo huko kenya na tunafanya biashara tanzania kenya na somali, so nafurahi kukutana na mrembo kama wewe na ningependa tuwe wote umenivutia sana Zehera kwa kweli unauzuri na umbo halisi la kinyarwanda,".
Zehera akajibu
"Kwa sasa siwezi kusema lolote, ila nitakupatia mawasiliano tutaongea nikifika nyumbani, usijari kaka angu tuko pamoja"
Hashiru akauliza
"Sawa zehera, vipi kwa sasa unajishughulisha na job gani hapa tanzania??"
Zehera kwa sura ya haya na aibu akajibu
"Mhhhhh,,, kwa kweli hadi sasa nimeajiriwa kwenye hotel moja hapa mjini, ila kipato ni kidogo sana hakinikidhi kabisa, kwani mama na wadogo zangu wananitegemea halafu nacholipwa ni mshahara wa chini sana, ndio maana nikaamua kupanga chumba huko uswahilini angalau kidogo huko kodi ni ya chini".
Hashiru akajibu
"Sasa kwanini usingejiajiri mwenyewe ukajisimamia na kuendesha mambo yako??".
Zehera akajibu
"Hilo wazo hua lipo, lakini kiukweli kuipata hela ya kuanza kujitegemea kujiajiri ni suala la ndoto isiyowezekana kwani kila napo pokea najikuta natuma mahitaji kwa mama pia bado namimi mwenyewe kujikimu inafail kabisa"
Hashiru akauliza
"Lakini mbona sister kwa muonekano wako unaonekana ni mtu fulani mwenye uwezo, ulivyo dress umbo lako lilivyo zuri moja kwa moja unapata taswira wewe ni mtu fulani maisha mazuri"
Zehera akajibu
"Wahenga walisema umaridadi huficha umaskini, kupendeza haimanishi una maisha mazuri, ukweli unabaki kuwa ndani yangu na napoishi, we twende utajionea mwenyewe mitaa nayokaa".
Basi baada ya kupita takrbani nusu saa wakawa tayari wameingia katika barabara inayoingia hadi mtaa wa mtakuja, hashiru akawa anafikiri jinsi gani atapitisha gari lake la kifahari kwenye njia finyu iliyotapakaa maji machafu yanayotiririshwa na mifereji inayotoka kwenye nyumba nyingi zilizobanana banana. Hashiru aka.........
ITAENDELEA......
TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.
Maoni
Chapisha Maoni