MGENI KUTOKA MJINI SEHEMU YA 2
SIMULIZI......MGENI KUTOKA MJINI
MTUNZI.........SHAX GOLD
NO..........002
Basi mzee mrisho na jeydan waliondoka uku wakiwa wanacheka ila juma akuwa sikia lakini alivyo tazama barabarani kwenye icho kinjia kidogo tu alimuona mtu akiwa amevaa kimjini mjini kabisa yani zilikuwa pigo za kisasa akiri ili mtuma kuwa yule ndio alie mfukuzia ndege wake.
Basi jeydan walifika adi kwa mzee nyange wakaomba ifadhi mzee nyange nae akuwa wanyima akawa wa kubalia mara kidogo aliingia juma mbavu uku akiwa amekasirika vibaya kwa kumkosa devota kwa stahili kama ile alivyo angalia pale kwao alimuona yule mgeni alievaa kimjini mjini ambae ni jeydan akiwa amekaa na babu yake kwenye beanch alafu baba yake mzee nyange akiwa amekaa kwenye kiti cha mbao apo chini ya mti.
“Afadhali nilivyo kuona baba angu kwema kwanza uko utokako...?” mzee mrisho alimuuliza juma mbavu alie kunja uso mda uwo kama vile kajambiwa na dondola.
”Kwema baba, shikamoo...” juma mbavu alisalimia uku ana mkata jicho jeydan la kushari shari.
”Marhabaa sasa mwanangu uyo unae muona apo ni mjukuu wangu anaitwa jeydan amekuja hapa ni mgeni ametokea mjini sasa tulikua tuna omba ifadhi kwenye chumba chako maana baba yako amesha kubali tayari kilicho baki ni idhini tu kutoka kwako....” aliongea mzee mrisho kwa sauti yenye ukalimu ndani yake.
“Usijari baba, nimesha kubali kwa moyo wote ata akikaa mwaka mzima. jeydan karibu kwetu...” juma aliongea uku akimpa jeydan mkono wa kinafki na kutoa mkono wake kwenye mkono wa mzee mrisho.
”Asante ndugu yangu nimesha karibia...”
Basi baada ya kupata hifadhi pale jeydan na babu yake walianza kuondoka taratibu kurudi nyumbani.
***************************
Kisimani alipokuwa devota na rafiki zake wanateka maji ilikuwa ni mida ya jioni jioni ivi kama kumi na moja basi devota alikuwa ana teka maji kwenye icho kisima rafiki yake mmoja anae julikana kwajina la grace alimuuliza.
“Devota mbona mda ule wakati una ongea na bwana mimbavu, ulikuwa una cheka cheka lakini baadae ulimkazia sura kama jambazi furani ivi ni tatizo lilikuwa nini shoga yangu...??” grace ali muuliza devota lakini devota akujibu kitu aliendelea kuchota maji yake mpaka amina akaingilia kati.
“Wewe devota mwenzako si amekuuliza mbona umjibu...?”
Amina ambae ni mcharuko wa hapo kijijini ali muuliza devita lakini na yeye vile vile akupewa jibu basi walikaa kimya tu devita alivyo maliza kuchota maji yake alimpisha irene ambae yeye ndo mpole kuliko wote pale wala aonge agi na mtu ovyo ovyo mda wote ni mkimya. Devota aliweka ndoo yake chini kisha akasema.
“Nyie nae yani mimi nachota maji mna nisemesha mnataka niingie kwenye kisima nini...!?” devota aliongea uku akiweka mikono yake kiunoni.
“Na unge ingia kweli ufe unajifanya kiziwi sikuizi..!!” Amina alimjibu devota kiukali mpaka devota akawa mpole.
“Sio kiziwi shoga yangu sema kuna kitu nilikuwa nawaza shoga zangu mnisamehe..” devota aliongea kiupole.
“Kitu gani tena icho unacho waza mtoto wa mzee kibara pumbu..?” amina aliongea.
“Shoga yangu wakati naongea na jumba mbavu pale sindo akapita bwana mzee mrisho na sijui mjukuu wake yule na anavyo onekana ni “MGENI KUTOKA MJINI” maana ule uvaaji wake sio wa hapa alafu ni mzuri huyo kaka sijawai kuona apa kijijini, ndo alie fanya mpaka nipate ujasiri wa kumtema juma mbavu pale...”
”Enheeeee!!! Usituambie...!!!” waliongea wote kwa pamoja isipo kiwa irene yeye alikuwa ana sikiliza tu wanacho ongea ila akuwa na time na I ho kitu kwanza yeye na wanaume ni vitu viwili tofauti toka atolewe bikra basi hana hamu nao tena.
“Akyamungu tena..!” devota aliongea ongea kwa kuwapa uku akipitia kidole chake cha shingoni kwake kama kuku anataka kunjiwa vile.
“Basi tukirudi tupitie kwa mzee mrisho tukamuone huyo kijana..”
Amina alitoa wazo na safari ikaanza ya kupita kwa mzee mrisho baada ya kumaliza kuteka maji.
************************
“Bibi naomba begi langu, kuna sola panel humo nataka ni wafungie hapa kabda sijaenda kulala ili kusudi na nyie mpate kamwanga japo jua ndo linazama ivyo..”
Bibi mrisho tena baada ya kusika mambo ya sola panel alizama ndani chapu akatoka na begi kisha akaingia tena ndani akatoka na ngazi akaitundika pale kwenye bati jeydan aliishika ile solar panel kisha akapanda juu chapu aka anza kufunga ile solar taratibu uku wazee wake wawili wakiwa chini wana mtazama.
“Kijana mwenyewe ndo yule pale juu sijui mme muona...?”
ITAENDELEA.........
TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.
Maoni
Chapisha Maoni