SHAIDA SEHEMU YA 9



SHAIDA: NO 09

"Ndio madame, eti umeniita"

"Shaida I'm sorry kwa hili, kiukweli naanza kuona tatizo kwenye ndoa yangu. Eddy anamapenzi ya dhati na mwanao mpaka nashindwa kuelewa, na si yeye tu Bali sote kwa ujumla tunampenda mwanao Sana.... Siku Ile tumegombana na Eddy kwasababu ya Umy na kuna maneno aliongea nikaona hakupendezwa wewe kuishi humu ndani bila kufanya kazi. Tafadhali nimeshaongea na Sharif, nataka nikupe hela, kuna nyumba nzuri Sharif amekutafutia kwa ajili ya kuishi wewe na Umy. Na ntakupatia pesa kwa ajili ya mtaji, si kusema undugu wetu utaishia hapa, Hapana! wewe ni zaidi ya ndugu kwangu, tutakuwa tukitembeleana na tutazidi kusaidiana, ambacho nahitaji kukiepusha hapa ni hii ya kila mtu ndani anachanganyikiwa kuhusu mtoto. Na Mimi hapa mjamzito. Naomba tafadhali nielewe mpenzi" maneno ya Anita yalimuingia Shaida ikambidi kukubali.

"Usijali dada Anita, naelewa tena naelewa sana, pia hongera kwa ujauzito"

Anita alivuta pochi yake na kutoa pesa kisha kumkabidhisha Shaida. Kwa bahati mbaya Eddy aliingia na kuona wanavyokabidhishana pesa. Shaida aliamua kunyanyuka na kutoka haraka.

"Nini kinaendelea" aliuliza Eddy.

"Hakuna baby" Anita alijibu kwa wasi wasi.

"OK jiandae unasubiriwa nje"

"Kina Frank wameshafika? "

"ndiyo" alijibu Eddy nakutoka huku akiwa anajiuliza pesa nyingi Kama zile amemkabidhi ili iweje. Na kwanini walipomuona walishtuka. Haraka alielekea chumbani kwa Shaida.

"Mbona unaingia bila kubisha hodi" aliuliza Shaida huku akifuta machozi.

"unalia?" Eddy alimuuliza kwa mshangao baada ya kumkuta akipanga nguo kwenye begi.

"Ungenikuta uchi?" aliuliza Shaida ili kuzuga.

"Nini kinakuliza? "

"Vituko vyako nimevichoka"

"nini kinaendelea Kati yako na Anita"

"Hakuna"

Eddy alisogea na kukaa kitandani.

"Niambie"

"Nimeshakwambia Hakuna kitu"

"Unanidanganya mimi"

"Kwanini uniulize Mimi? Si ukamuulize mkeo"

"Aaah jeuri"

"Jeuri kitu gani? Si unaona Mimi mzigo kukaa hapa bila kufanya kazi... Ila Mimi Hakuna niliyemwambia atafute mfanyakazi mwingine na istoshe kazi zote nilikuwa nafanya"

"Aaah naona Kuna kitu mmekizalisha hapa, wait" Eddy alinyanyuka na kumshika mkono kisha kumtoa chumbani. Moja kwa moja mpaka chumbani kwake alipo Anita.

"Hey baby nini shida?" aliuliza Anita kwa mshangao.

"Naomba mnijibu, nini kinaendelea Kati yenu? " aliuliza Eddy kwa upole na kuwafanya watazamane kwa mashaka.

Be.... " Anita aliishia hapo baada ya kunyamanzishwa na Eddy.

"Mlikuwa mnakabidhiana pesa ili iweje? "

"Eddy Mimi ntakujibu. Mkeo hahusiki, Mimi ndo nimemuomba pesa ili nirudi nyumbani" Shaida aliongea kwa upole huku akilia.

"Not, Anita you lie to me?" Eddy alimjohi mkewe.

"No dear ukweli ni kwamba" Anita aliamua kumueleza ukweli mumewe ili kuepusha balaa.

"Aaah kumbe naonekana mjinga humu ndani? OK Shaida hamna kutoka humu, aliemruhusu kuishi hapa ni baba. Na yeye ndie atajuwa nini cha kufanya, halafu Shaida suala la wewe kutokufanya kazi nililidhibitisha Mimi sijui tunaelewana?" aliongea Eddy kwa upole.

"Lakini baby Sharif alitaka akaishi nae"

"Akaishi nae kwasababu gani?"

"Kwasababu ni wapenzi"

"Shaida unamahusiano gani na Sharif?" Eddy alihoji kwa msisitizo.

Shaida alikosa jibu la kujibu akaishia kupepesa kope.

"Mwambie usiogope" aliongea Anita.

"Usimlazimishe kuongea. Shaida nenda chumbani kwako" Eddy alimuomba Shaida kuelekea chumbani kwake ili kuepusha maneno.

Baada ya muda walijiandaa na kuelekea chini kwa ajili ya kuongea na wageni.

"Oohh shemela huyo" aliongea Dan Ambae alikuwa amekaa kwenye sofu huku kinywaji kikiwa mbele yake.

"Unanianza shem" Anita alijibu na kukaa.

"Ni muda toka kwenye harusi yenu sijakuona"

"Hukutaka kuniona ndo maana"

"Upo salama lakini?"

"Yeah nipo sawa"

Wakiwa wanaendelea kupiga story za hapa na pale, alifika Shaida akiwa amembemba Umy mgongoni, pamoja na Nyamisi Akiwa na kikapo. Kina Dan walipomuona Shaida walishtuka mno na kuishia kumtazama, upande wa Shaida haikumshtua maana Kama ni ubaya walishaga ufanya.

"Ha ha habari ya ya yako Shem" Dan Alitoa salam na kumshangaza Anita ambae aliangua kicheko.

"Aah Shem bhana, huoni kizuri kikakupita, yaani hapo unataka uambiwa hajaolewa ili upate gia ya kuanza nayo" maneno ya Anita yaliwashangaza Sana kina Dan maana Shaida wanamjua vizuri Kama shemeji yao.

"Shaida mnaelekea wapi?" Anita alihoji.

"Tunafika gengeni Mara moja"

"Mtoto muacheni" Eddy aliongea bila wasi wasi huku akibonyeza simu, na hapo ndipo alizidi kuwachanganya marafiki zake. Upande wa Anita alianza kupatwa na wivu kutokana na Eddy kuonekana kumjali Sana mtoto.

Shaida alimtoa Umy mgongoni na kumkabidhisha Anita ambae alimpokea kinyonge tofauti na siku zote.

"Mlete kwanza" Dan alimfuata Umy na kurudi nae kukaa.

"Mmmhhh Aisee ni mtoto wa Eddy kabisa, ila mbona sielewi kinachoendelea" Dan alijisemea Moyoni baada ya kumtazama Umy kwa muda.

"Shem tumboni kukoje? " aliuliza Frank .

"Mi mniache"

"Kwanza hataki kufanya mazowezi" aliongea Eddy kiutani.

"Mwaya mazowezi yake hata sijawahi kuyaona" maneno ya Anita yalimchekesha kila mtu.

Baada ya muda Eddy na wenzie walikuwa wamekaa nje huku wakipata soda taratibu.

"Yaani sijakuelewa, how" aliongea Dan.

"How nini? Mambo ndo hivo hata Mimi mwenyewe nashindwa nichukue uamzi gani" alijibu Eddy.

"Em imagine siku mkeo akalijuwa hili"

"I don't care"

"Dah! Kidogo nilisanue muda ule"

"Hata ungesanua. unahisi naogopa? Anita ni mke wangu vile vile na Shaida pia"

"Hayo mapenzi kwa Shaida yametokea wapi? Siyo wewe ulimtelekeza na ukasema haja yako imekwisha " Frank aliongea.

"Nikweli, sema nilipigwa na butwaa Sana ila she's different na ukija kuangalia ana mwanangu why niendelee kuutesa moyo wake"

"Hilo nikweli kabisa" aliongea Dan na muda huo Shaida pamoja na Nyamisi walirudi. Dan alipowaona alimuomba Shaida amletee maji ya kunywa.

"Kuna kitu chochote unataka kumuuliza" alihoji Eddy.

"Yeah"

Kama dakika kadhaa alifika Shaida akiwa na maji.

"Shem za siku" Dan Alitoa salam.

"Safi"

"Vipi Yule ni mwanetu?"

"Sijaelewa swali lako"

Muda huo Sharif alifika.

"Hey guys mambo vipi"

"Saf Inakuwaje" walimjibu kwa pamoja.

"Balida, huyu ni mke wangu mtarajiwa" aliongea Sharif akiwa amemshika begani Shaida, jambo lililowashangaza kina Dan huku Eddy akijifanya kupotezea.

"Aaahh" Dan aliishia kukubali, ndipo Sharif alimshika mkono na kutoka nae.

"Inawezekana vipi" aliongea Dan.

"Imewezekana, unaniuliza nini tena" alijibu Eddy.

"Sometimes maamuzi yako siyaelewi, hivi huoni Kama hili litakuwa tatizo mbeleni"

"Nikweli kwasababu Kama Sharif atatembea nae sizani Kama utakuwa na nafasi tena" aliongea Frank na kumjengea wivu Eddy.

Upande wa ndani, Shaida pamoja Nyamisi walikuwa wanachambua mchicha huku wakipiga story.

"Familia hii inakupenda Sana" aliongea nyamisi na kumfanya shaida atabasamu.

"Kwanini?"

"Wewe huoni? Halafu shoga yangu, boss anakupenda"

"Sharif?"

"Hapana Eddy"

"Weeee, nani kakwambia"

"Namuona ona, mfano juzi nimemuacha Umy sebuleni mwenyewe. Basi alivyofika akamuona, weee niliulizwa maswali wewe"

"Kwahiyo unataka kusema napendwa. umy ndie anapendwa"

"Hata wewe"

Muda huo aliingia Anita akiwa amemnyanyua Umy.

"Nyamisi naomba tupishe kidogo" aliongea Anita kwa upole ndipo Nyamisi alitoka.

"Shaida"

"Abee boss"

"Nataka nikupe nauli urudi kwenu" maneno ya Anita yalimshtua Shaida.

"Kwanini? Au kazi sifanyi vizuri"

"Siyo hivo, tatizo ni Eddy"

"Kafanyaje" alihoji kwa hofu huku akihisi huwende Siri tayari imegundulika.

"Eddy simuelewi kabisa. Mapenzi aliyonayo kwa Umy siyo ya kawaida, tafadhali naomba usikatae kuondoka"

"Sawa ntaondoka" Shaida alijibu kinyonge, ndipo Anita aliondoka na kumuachia mawazo.

Majira ya usiku Shaida alianza kumtafuta Anita maana ndie alikuwa na Umy toka mchana hivo alitaka akalale maana tayari walikuwa wameshakula. Kila kona aliyomtaftia alimkosa ikambidi kuelekea kunako chumba chake. Alipofika alibisha hodi ndipo Eddy alimuuliza.

"Unagonga huku?"

Shaida alipoisikia sauti ya Eddy, hakutaka kujibu ilimbidi kuanza kurudi nyuma.

"Shaida"

Shaida alishtushwa na Sauti ya Eddy, ndipo alisimama na kugeuka kumtazama.

"Njoo" Eddy alimwita ndipo Shaida alisogea taratibu.

"Kuna nini?" alihoji Eddy.

"Anita yupo?"

"Kwanini ulikuwa unaondoka, na Anita wa nini?"

"Namtaka Umy nikamuoshe"

"Sijui kaenda wapi, ila upo sawa?"

"Ndio" alijibu kinyonge.

"No! Haupo sawa njoo uniambia" Eddy aliongea na kumshika mkono Tayari kumvutia chumbani kwake.

Kama bahati mbaya tukio hilo Sharif alilishuhudia na kubaki mdomo wazi.

"Mungu wangu, Eddy mbona hivo"

"Niambie unanini"

"Hivi Anita atukute hapa jamani. .. Mimi mnyonge ntafanya nini Kama siyo kuuwawa"

"Usijali nataka kujuwa nini kimekusibu hata mezani nimekuona ulivyokuwa unakula"

"Hakuna"

"Mbona mudi ulitoweka"

"Anita anataka.... " kabla hajamalizia kuongea, mlango uligongwa na ikasikika sauti ya Anita akicheka Kama mwenye kuongea na simu.

"Toba, nafanya nini Mimi" aliongea Shaida kwa hofu, huku Eddy akionekana kutokushtushwa na jambo lolote.

Upande wa Anita, Sharif alimfuata na kuomba kuongea nae ili kuepusha balaa.

"Iwe habari nzuri" aliongea Anita baada ya kufika sebuleni.

"Don't worry my sister, nilitakakukwambia kuwa. Nahitaji kurudi nyumbani hivi karibuni"

"Ooh na vipi kuhusu Shaida?"

"Hilo tutalizungumzia baadae"

Upande wa Eddy, Shaida hakutaka mjadala tena, aliamua kuelekea chumbani kwake. Akiwa yupo chumbani huku akijiuliza balaa litakalotokea siku Anita akijuwa Kuwa Umy ni mtoto wa Eddy,

muda huo Sharif aliingia akiwa na Umy.

"I'm sorry kuingia bila kubisha hodi" aliongea Sharif kinyonge huku akikaa kitandani.

"Haina shida" alijibu Shaida bila wasi wasi.

"Naomba kukuuliza"

"Niulize"

ITAENDELEA.....


TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: BINAMU 🔞 SEHEMU YA 11

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 1-5

CHOMBEZO: MASSAGE ROOM🔞 SEHEMU YA 21