SIKUSTAHILI SEHEMU YA 17

“ SIKUSTAHILI” Na:Anold Machavo Mbeya—Tanzania Sehemu ipatayo ya 17 ★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★ ««Ilipokomea... Kuonana naye ilikuwa ni mpaka kazini tuu na kwa kuwa ulikuwa ni wakati wa kazi hawakuweza kuwa jirani zaidi kuhofia kupunguza ufanisi katika utendaji kazi. Baada ya siku kadhaa Cara alishawishiwa na rafiki zake kutomuacha kijana mwenye muonekano na tabia zinazomkosha, Cara alikuja na mbinu ndogo yenye ujanja zaidi. Alithibitisha kuwa Edison ni ndege mjanja anakwenda kunaswa katika tundu bovu... TEREMKA NAYO...»» Siku mojawapo Edison alipokuwa dukani akiendelea na kazi ya kuwaonyesha nguo mpya kwa wateja wa jumla. Kwa bahati nzuri au mbaya siku hiyo alikuwa na mambo mengi hali iliyomfanya akasahau simu yake mezani katika chumba chake kule. Wateja walikuwa wengi na walihitaji muda mrefu kiasi ili kuchagua aina zote watakazozipenda na kuhitaji kununua. Edison akisaidiana na Issa pamoja na Mariam kwa zile za kike walihakikisha kila mteja anakamilisha mahitaji yake pale siyo nusunusu y...