TWINS (MAPACHA) PART:1
TWINS (MAPACHA)
MTUNZI:OFFICIAL IBRAAH JUNIOR
PART:01
TUANZE NAYO...
Ni katika shule ya High school inayopatika mtaa wa kinondoni jiji dar es salam, ilikuwa shule kubwa ya bweni (boding), anaoneka kijana majali, kijana ambae siku zote alijitahidi kupambana kimasomo ili aje aokee familia yake, licha ya familia yake ipo kijijini na hali ngumu ya kimaisha basi alipigana hapa na pale tu ili aokoee familia, siku moja akiwa shule hapo alitembelea wa mjomba wake, maana ilikuwa harusiwi kuondoka kutokana na shule ulikuwepo mbali na kijiji anachoishi ivyo ililazimika akae hapo shule mpaka likizo...
Siku moja, mjomba wa Majaliwa aliwasili shuleni hapo na kuonana ana majaliwa
"Mjomba wangu, usijali nitakulea mwanangu, nitakusomesha, na utafaulu vizuri"
"Mjomba kuna nini kwani mpaka unasema hivyo maana, maana si kawaida, na sikuelewi kwanini unasema hivyo"
Majaliwa alikuwa ni kijana wa miaka 19 ambae alikuwa nasoma kidato cha tatu katika za bweni, siku zote hakuzoea kumuona mjomba wake kwenye hali ile na kuongea maneno yale maana kama kusomeshwa huwa wanashirikiana na wazazi wake leo anamwambia maneno hayo ataweza kumsomesha peke ake
"Mbona sijakuelewa mjomba una maanisha nini"Majaliwa aliongea kwa hamaki
"Mjomba usijali, ila nafikiri twende kijijini"
Mjomba aliongea na kumfanya majaliwa ashangae
"Kijijini!, kuna nini kijijini anco, na wakati huu si wa likizo!"Majaliwa alishangaa sana na ikabidi amuulize Mjomba wake maswali mengi
Mjomba wa Majaliwa hakuwa na mazungumzo mengi aliamua kutumia cheo chake na kuondoka kwenda kijijini, wakati huo Majaliwa hakuelewa kabisa mjomba ake amekumbwa na nini, Safari ndefu ikaendelea mpaka kufika kijijini.
Majaliwa alishangaa sana baada ya kushuka gari na kupokelewa kwa kundi la watu, ilikuwa si kawaida yake Majaliwa ata akirudi likizo
"Mbona sijakuelewa mjomba mpaka sasa mnanipeleka peleka tu, kuna nini?"Majaliwa alizidi kuwa na wasi wasi
Hatimae walifika nyumbani kwao Majaliwa na kukutana na watu wengi sana ambao walitanda kwenye nyumba yao na wengine walikuwa nalia na Majaliwa akapelekwa ndani ndipo alipoona maiti mbili zikiwa zimelala kwenye sakafu, moyo ulimdunda na mapigo ya moyo kwenda mbio na kusema kwa kilio cha uchungu...
"Maa..mama! , Ba.. Baba!"Majaliwa aliita majina hayo na kupiga goti mbele ya maiti zile na kuanza kulia kwa uchungu
Hakika ni kilio, kilicho wafanya watu kumshika na kumtoa kwenye miili hiyo miwili, walikuwa ni wazazi wa majaliwa ambao walikufa kwa ajali gari, majaliwa alilia sana na kujiuliza tumaini lake limepitea nani atakae msaidia kuishi na kuendelea na shule, Majaliwa alizidi kulia sana sana. Baada ya masaa machache kupita Majaliwa alinyamaza na mipango ya mazishi ikapangwa kesho yake, huku majaliwa akiwa amebaki peke ake maana katika uzao wa wazazi wake yupo yeye pekee. Mazishi yalipangwa na wanafunzi wachache pamoja na Madam ambaye alikuwa mwalimu wa Majaliwa nae aliwasili kwenye msiba huo mzito
"Baada ya msiba, Inabidi Majaliwa arudi shule"Madam aliongea kwa sauti ya upole
"Madam Deborah, sasa nani atakae msomesha majaliwa shule ya kulipia kwa sasa, maana hao wazazi wake tu walikuwa wanajinyima mengi sana na walikuwa na uwezo kidogo"Mjomba wa majaliwa aliongea kwa huzuni na kumfanya majaliwa ajinamie tu
"Daahh!, ila mimi nitajitolea kumsomesha Majaliwa, maana ni kijana Muelewa"Madam Deborah aliongea na Majaliwa kupata tumaini na kunyanyua kichwa
"Kweli madam!" Majaliwa alitakia kumuuliza madam kwa sauti ya kufarijika na jambo alilosikia
"Ndio" Madam alijibu kwa kutabasamu
"Sawa, tumekubali bila shaka ila majaliwa ukasome tu"Mjomba alikubali na kumsisitiza Majaliwa juu ya elimu
"Sawa mjomba"
Baada ya siku tatu, Majaliwa na Madam waliaga kijijini na kwenda mjini dar es salam kwaajili ya kuendelea na masomo, Majaliwa hakupelekwa tena bweni kwaajili ya kuishi shule, kwasababu Madam alikuwa akiishi karibu na shule hiyo hivyo akampeleka hadi kwake
Madam Deborah,alikuwa mwalimu mkuu wa shule ya High school, alikuwa ni mtu mzima ambaye alikuwa na watoto wawili mapacha, yaani Dorice ambae alikuwa ndo Dotto, na mwengine kurwa ambae alikuwa anaitwa Dorine.
Walikuwa mabinti ambao wanasoma madarasa tofauti tofauti kwa sababu Dotto yeye alipatwa na maradhi na badae kurejeshwa darasa baada ya kukaa sana kwao alikuwa kidato cha kwanzo na Dorine alikuwa kidato cha pili. Madam baada ya kufika aliwatambukisha watoto wake kwa Majaliwa na majaliwa akatambulishwa, hayo ndo yakawa mwanzo wa maisha ya Majaliwa. Asubuhi mapema, Majaliwa alimka kitandani mara baada ya usingizi wa mda mrefu, kutoka saa 2 usiku mpaka asubuhi hiyo, alishuka kitandani na kuchukua mswaki ili akajisafishe mwili kwa lengo la kwenda shule. Upande wa Dorine na Dorice nao walizidi kujiandaa kuwahi shule. Ilikuwa ni jumatatu tulivu kabisa, siku ambayo kila mmoja aliamka kwa furaha
"Majaliwa, Majaliwa, weee majaliwa..!" Ilisika sauti ya Madam Irene akimwita majaliwa ambae alikuws bafuni mwake akikoga
"Naam anti, nipo bafuni"Majaliwa ajibu
"Nikajua umelala, maana unanupenda usingizi" Madam alimtania Majaliwa
"Nakuja Mama nawe"
Hayo ndo yakawa maisha ya furaha na siku zote madam Irene alijitahidi kumlea Majaliwa kama aliyemzaa ilimradi tu asije akajisikia vibaya kutokana na kufa kwa wazazi wake Majaliwa. Majaliwa alikuwa vizuri kielimu na huku akiwa na dada zake Kurwa na Doto. Siku moja Kurwa alikaa sehemu na kumwangalia sana Majaliwa, ilikuwa ni siku za mapumziko, Majaliwa alikuwa akisafisha bustani ya kwao huku Kurwa akiwa anamwangalia kwa jicho regevu lenye mahaba ndani yake...
ITAENDELEAA......
BAKI HAPA HAPA KWENYE APP YETU, MUITE NA MWINGINE.
Maoni
Chapisha Maoni