SIKUTEGEMEA SEHEMU YA 7



SIMULIZI : SIKUTEGEMEA

MTUNZI : MADAM YUSTAR

SEHEMU YA SABA

Tuendeleee..

Nilitoka kwa hasira hadi jikoni nilivyofika moyo wangu ulipiga shoti , ukweli sikuweza kufanya chochote nilisimama kama vile nimetekwa.

Akili yangu gafla ilianza kuwawaza watoto wangu, niliwaza wakifunga shule nitawaeleza nini kuhusu baba yao? Watanielewaje lakini nilimuwaza mwanangu ambaye bado alikuwa na mwaka mmoja tu , huyu ndo alinipa mawazo zaidi mwanangu kuiishi bila baba ooh..! Haikuwa rahisi kulipokea hili jambo, moyo wangu ulizidi kunisisitiza lazima nibaki hadi nione mwisho wa haya yote ni lini, nilitoka jikoni moja kwa moja hadi vyumba vya wageni niliingia na kujifungia kwa ndani.

Ninachoshukuru chumba hiki kilikuwa na bafu pamoja na choo chake hivyo kwangu ilikuwa raha sana.

Usku mzima sikuweza kupata usingizi, nilitafakari ni nini maana ya haya yote? Au sikuwahi kuwa na mvuto wowote kwa Peter.

Yawezekana hakuwahi kunipenda, au kaendewa kwa mganga lakini mbona siamini imani kama hizi?

Nilitafakari kwa mda mrefu mwisho nilipitiwa na usingizi.

       ***

Alfajiri na mapema nilishtushwa na kelele za mwanangu,  nilikumbuka mwanangu sijamuona toka jana ,  nilitoka haraka chumbani hadi sebleni,  nilivyofika nilishangaa dada wa kazi kabeba mtoto mwingine wangu yupo chini hana kofia wala soksi.

Wakati natafakari Irene alitokea ,  mkononi alikuwa kabeba funguo za gari aliniangalia juu hadi chini mwisho alisema;

"Mwangalie huyo nyani wako mwenyewe,  dada wa kazi atakuwa anahangaika na mwanangu.

Sikutegemeaa yale maneno kutoka kwenye kinywa cha rafiki angu,  sikuweza kumjibu kwa chochote nilimnyanyua mwanangu na kwenda nae chumbani.

Nilimfanyia usafi ,  nilimwangalia kwa macho ya huruma nikiwa kama mwanamke niliyekulia kwenye mazingira magumu sikuwa tayari kuona watoto wangu wanateseka.

Nilitoka na kwenda kumwandalia chochote mwanangu,  baada ya hapo nilisha mwangu alionekana kuwa na njaa sana.

Bado akili yangu iliwaza nitafanya nini ili niweze kutoka kwenye huu upweke,  nilikumbuka yupo Mungu asiyewahi wala kuchelewa kujibu maombi.

Nilinyanyua mwanangu na kwenda nae kanisani,  nilivyofika nilipiga magoti na kuongea na Mungu wangu.

" yawezekana yapo mambo mabaya nimetenda,  yawezekana sina meme hata moja mbele ya mume wangu na rafiki angu kipenzi ila wewe Mungu unajua haja ya moyo wangu. Baraka zako zikawe na mimi kila ninapoenda,  watoto wangu waongozwe na Roho Mtakatifu katika kila jambo,  maisha yangu nayakabizisha mikononi mwako" 

Baada ya kumaliza kuomba niliona moyo wangu u

naamani sana,  nilijiona mwepesi saana nilinyanyuka na mwanangu hadi nje.

Wakati nipo njee nilishangaa kijana Mtanashati anasigea karibu yangu,  uso wake ulijawa na tabasabu sana hata mwanangu alivyomuona alianza kumlilia yule kijana.

Alivyofika aliomba kumbeba mtoto wangu,  alivyombeba tu mwanangu alianza kutabasamu kama vile walishawahi kuonana kabla ya hapa kanisani.

Moyo wangu ulishtuka sana ,  gafla akili ilianza kujiuliza huyu mtu atakuwa ni nani?
Je! Huyu kijana ni nani???

      ITAENDELEA......

BAKI HAPA HAPA KWENYE APP YETU, MUITE NA MWINGINE.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: BINAMU 🔞 SEHEMU YA 11

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 1-5

CHOMBEZO: MASSAGE ROOM🔞 SEHEMU YA 21