MUDRICK AND JABIR SEHEMU YA 21



HADITHI- MUDRICK AND JABIR

SEHEMU YA 21

MTUNZI- LISSA WA MARIAM

"Sasa unanikatia simu na kunizimia ili iweje? Unajua nataka kukwambia nini?" Nawal alisema na kujilaza alichukia sana,

Baada ya nusu saa kupita, Mudrick alirudi na kumuomba atoe vyombo kama amemaliza, aliita sana akiwa mlangoni lakini Nawal hakuitikia ikabidi afungue mlango kwa kuogopa asije kumkuta labda hajavaa, alichungulia na kumuona amelala na kugeukia upande mwingine

Mudrick aliingia na kukuta chakula vile vile kama kilivyo, alianza kumuita taratibu kwa kujua huenda yupo kwenye usingizi, lakini Nawal alikuwa macho na kila kitu alisikia alipomgeuza alimuona akitokwa machozi

"Nawal umezidiwa sana au? Mbona unalia jamani"
"Nipo sawa"
"Sasa mbona hujala, kwani unatatizo gani? Embu niambie kwasasa mimi ndo nipo hapa na wewe, mama amechelewa leo naomba niambie pleasee, au unahisi mimi sitokuwa na msaada kwako? Embu niambie"

"Mudrick?" Nawal aliita kwa upole na kuinuka akakaa

"Naam"
"Kwani unanichukia mimi?"
"Nikuchukie kwasababu gani?"
"Kwasababu nilikataa ombi lako na kukwambia nina mahusiano na Jabir?"

"Hapana siwezi kukuchukia kabisa, nawezaje kufanya haya yote kwa mtu ambae namchukia! mimi nikishampenda mtu huwa kumchukia siwezi, je kweli wewe na Jabir mna mahusiano au umeniambia vile ili tu unikatae mimi?

"Ndio kweli tuna mahusiano, wala sioni sababu ya kudanganya, wewe umechelewa Mudrick hivyo hupaswi kunichukia mimi wala Jabir"

"Mmhhh! Ok nimekuelewa mimi sitofanya hivyo sawa, wote nawapenda ila mbona Jabir kasema hana mahusiano na wewe?"

"Amesema hivyo?" Nawal akishtuka
"Ndio ameniambia kuwa nyinyi sio wapenzi"

"Hapana amedanganya na hilo jambo ndo linanifanya niumie sana, mimi siumwi kabisa sina homa wala malaria, isipokuwa leo nimeongea na Jabir amenisema sana kwanini nilikwambia mimi na yeye ni wapenzi, pia hataki kuongea na mimi kasema mpaka nitakapokanusha kwako kuwa sisi hatuna mahusiano, kila nikimpigia hataki kupokea kwanini mnaamua kunifanyia hivyo" Nawal alilalamika

"Hee! Sasa mimi au yeye ndo anakufanyia hivyo? ukweli sielewi kwanini hili jambo nafichwa fichwa, basi nisikilize Nawal wewe si unampenda Jabir? Basi hakuna shida kuwa nae tu, mimi nitabaki kama shemeji yako au ukijisikia kuniita kaka basi pia ni sawa, naomba hili jambo leo liwe mwisho, nitachofanya kukusaidia kuongea na Jabir ili muweze kuwa sawa, naomba ule chakula sasa nitoe hivi vyombo" Mudrick alisema akimaanisha

"Sawa nitakula tu na nikimaliza nitatoa"

"Hapana kula nikiwa hapa hapa, hayo ni mambo yakawaida mdogo wangu yasikupe shida" Mudrick alimbembeleza na kuchukua kijiko akawa anataka kumlisha

Nawal kabla hajafungua mdomo alibaki kumuangalia Mudrick asiamini kile anachotaka kufanya.

ITAENDELEA.....

BAKI HAPA HAPA KWENYE APP YETU, MUITE NA MWINGINE


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: BINAMU 🔞 SEHEMU YA 11

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 1-5

CHOMBEZO: MASSAGE ROOM🔞 SEHEMU YA 21