SIKUSTAHILI SEHEMU YA 17



SIKUSTAHILI”

Na:Anold Machavo

Mbeya—Tanzania

Sehemu ipatayo ya 17
★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★
««Ilipokomea...
Kuonana naye ilikuwa ni mpaka kazini tuu na kwa kuwa ulikuwa ni wakati wa kazi hawakuweza kuwa jirani zaidi kuhofia kupunguza ufanisi katika utendaji kazi. Baada ya siku kadhaa Cara alishawishiwa na rafiki zake kutomuacha kijana mwenye muonekano na tabia zinazomkosha, Cara alikuja na mbinu ndogo yenye ujanja zaidi. Alithibitisha kuwa Edison ni ndege mjanja anakwenda kunaswa katika tundu bovu...

TEREMKA NAYO...»»
Siku mojawapo Edison alipokuwa dukani akiendelea na kazi ya kuwaonyesha nguo mpya kwa wateja wa jumla. Kwa bahati nzuri au mbaya siku hiyo alikuwa na mambo mengi hali iliyomfanya akasahau simu yake mezani katika chumba chake kule. Wateja walikuwa wengi na walihitaji muda mrefu kiasi ili kuchagua aina zote watakazozipenda na kuhitaji kununua. Edison akisaidiana na Issa pamoja na Mariam kwa zile za kike walihakikisha kila mteja anakamilisha mahitaji yake pale siyo nusunusu yaani fullu pakeji. Siku hiyo Cara aliiona simu ya Edison ikizubaa mezani wakati akipita jirani na chumba kile.
Cara aliinyanyua simu ya Edison na bila kupoteza muda alipitiliza kukagua jumbe kadhaa kwenye simu hiyo ndipo alikutana na namba iliyojionyesha kwa jina tuu lililohifadhiwa lilijieleza kila kitu si wajua tena yale majina yetu yaani. Alipokagua baadhi ya jumbe kwenye namba hiyo pekee alikutana na faraja ya moyo wa Edison, mahali anapojidai napo kila anapoona mwanamke mwingine sijui kama hakuona wengine au ndiyo alikuwa akifanya kuvunga.
Alipekua na rekodi za namba zilizopigwa na kupokelewa, huko alikuta namba ya Bahati ndiyo imeshamiri na kutawala pote. Ndiyo namba hiyohiyo iliyojaa kwenye upande wa jumbe/meseji. Mpaka hapo alifahamu ya kuwa huyu ndiye anayempa kiburi Edison hadi anamzungusha ilihali yupo jirani naye zaidi kuliko huyo mhusika. Aliinyanyua simu hiyo na kuipiga namba ya Bahati. Hazikupita sekunde tano tayari simu ilikuwa imepokelewa.
“Habari ya kazi Eddy wangu?” Sauti nzuri yenye bashasha na kuchombeza kutoka upande wa pili ilisikika simuni mara tuu simu ilipopokelewa.
“Eddy wako tangu lini?” Cara aliuliza kwa jazba.
“Mbona unanichanganya dada, kwani wewe nani na simu hiyo ni ya Eddy?.”
“Nakuambia kistaarabu tuu niachie Eddy wangu sikufahamu kumbe ndiyo maana siku hizi amekuwa makini sana na simu mpaka ananisahau miye kisa wewe.”
“Kumbe alishapata wa huko mjini siku nyingi halafu hajaniambia Eddy kwanini kanifanyia hivi lakini jamani...” Sauti yenye kigugumizi ilitoka kwa Bahati aliyeonyesha kushangazwa vilevile kuumizwa baada ya kusikia jabari hilo.
“Ndiyo hivyo dada yangu nakuambia kistaarabu tuu, simu nimemnunulia mimi halafu anajifanya mjanja, hebu niachie Eddy wangu kabla hatujaonyeshana utabe.”
“Yote sawa nilijua tuu ipo siku atakuja kunisaliti na kunitupa namna hii mwambie nampenda sana na namtakia maisha mema huko alipo sikustahili kufanyiwa hivi mimi bora angekuwa mkweli tuu.” Bahati alijibu kwa sauti iliyogubikwa na kilio chenye kwikwi na maumivu ya mtu mzima yaliyomaanisha machungu mazito.
Cara alicheka kwa dharau na kumwambia “tena uifute namba yake na umkome kabisa Eddy wangu.”
Bahati alipatwa na ganzi mwili mzima, alijihisi mwili kuchoka kwani hakuamini kama kweli Edison ameamua kumtuma mwanamke wake amtukane na kumchamba kwa maneno ya dharau na fedheha kupitia simu ya Edison.
Lakini hakuwa na namna, ukikubali kuolewa ni lazima ukubali kulala mtupu, Bahati alikubali kumpenda Edison hivyo hakuwa na namna yoyote ya kuyakwepa maumivu endapo akiachwa kwa kishindo ama kuumizwa hivi.
Hakufurahia kwa kitendo cha kuachwa kiasi hicho tena bila kosa. Hapa alikumbuka kuwa mara nyingi wenye roho nzuri na kila kutenda wema wao hutendewa ubaya kama malipo. Siku hiyo ikawa imevurugika kwa upande wa Bahati alizima simu yake na kulala ingawa ilikuwa ni mchana kupooza machungu ingawa hata usingizi haukuwepo. Kwa mliyowahi kuachwa mnaweza kushuhudia eti huwa inakuwaje, nasikia hata kuku wa kuchomwa hapandi usingizi hakuna au ni wachache tuu wanakutwa na hayo ma-ovyoovyo.😃😃
Cara alifurahi baada ya kuona Bahati amekata simu yake kwa hasira na machungu baada ya kukitwa na kisu kikali katika eneo la moyo wake lililokuwa dhaifu kwa Edison. Alifuta rekodi ya mwisho aliyompigia simu Bahati endapo Edison akija kukagua ili ashindwe kugundua kirahisi. Cara alisubiri kujua yajayo kwani tayari ameshafanya kazi yake kiutaalamu zaidi na kilichosalia ni kusubiri dawa iingie vizuri.

Aliirudisha simu ya Edison mezani na kuondoka kwenye kichumba hicho kimyakimya bila kuonwa na mtu kwani chumba chenyewe kimejificha jirani na stoo. Wakati huo bado Edison alikuwa makini kufuatilia wateja wake huko waliokuwa wanachagua mzigo huu mara wanaacha halafu wanahamia mwingine lakini yote kwa yote mteja ni mfalme licha ya kumkaribisha kwa taadhima pia unatakiwa kumvumilia katika kero nyinginezo ndogondogo kama hizi anazozionyesha. Walichukua muda mrefu mpaka wateja wale walipokamilisha kuchukua bidhaa zao za jumla kisha wakasaidiwa kubebewa hadi nje kwa ajili ya safari ziendako. Edison alifunga stoo kama ilivyo jadi na kurudi kwenye chumba chake. Ilikuwa jioni tayari kwa wakati huo. Aliendelea kuperuzi kwenye simu yake katika mitandao ya kijamii bila ya kumtafuta Bahati. Edison hakufikiria chochote juu ya kumtafuta Bahati kwa wakati ule.
Siku iliisha pasi na kumtafuta Bahati hadi yalipofika majira ya usiku kabla ya kulala. Edison alinyanyua simu na kumtafuta Bahati lakini simu haikupatikana kwa usiku ule. Edison asielewe chochote alihisi labda simu haina chaji ukilinganisha na kutokuwa na umeme wa uhakika zaidi ya kutegemea umeme wa sola kule kijijini ingawa hakuna siku ambayo Bahati hakuwahi kutopatikana. Edison alijisemea labda ni mambo ya kawaida bila kujua kinachoendelea tena alipata usingizi mwanana kuitafuta asubuhi awahi kibaruani.
Siku ya pili aliwahi kibaruani na alipojaribu kumtafuta Bahati bado majibu yalikuwa vilevile haikupatikana. Hapa ndipo alipata wasiwasi labda huenda simu yake ina matatizo. Baada ya kashikashi zote za siku hiyo kuisha ulifika wakati wa kuondoka ndipo alimpigia simu mama yake kumjulia hali baada ya kutoongea naye siku nyingi. Alifanikiwa pia kuongea na dogo lake ambaye kabla ya Bahati kuwa na simu alitumika kama mjumbe huru. Alimuachia maagizo dogo na kumwambia kuwa akipata mrejesho amletee madini. Dogo hakuwa na shida ingawa siyo nzuri hii wanakuwaga wabaya baadaye hawa maana kila kona wanazijua vizuri.
Edison aliendelea kujaribu kumtafuta Bahati bila mafanikio yoyote hadi siku hiyo pia iliyoisha.
Siku iliyofuata dogo alipokuwa akirudi kutoka shule kama bahati nasibu alifanikiwa kukutana na Bahati mwenyewe sasa. Alitoa salanu kama ilivyo ada na kuongea machache sana.
“Hajaniagiza chochote mimi kasema tuu muongee naye.” Dogo aliongea.
“Weeee tena mnikome na kaka yako sitaki kuwaona.” Bahati alijibu kwa jazba kidogo.
“Mimi nina kosa gani mfano?” Dogo aliuliza kwa mshangao ingawa tayari alijua tayari jungu la mboga limeshanyewa na mtoto.
“Ondoka dogo halafu namshangaa sana kaka yako anakupoteza tuu wewe unaacha kuwa makini na shule unafanya umbea huu.” Bahati bado alikuwa na hasira alitamani hadi kumdunda mang'wenzi dogo.
“Sasa shule imetoka wapi tena miye sina kosa nimefikisha taarifa naondoka.” Dogo alitumia busara zaidi.
“Ukija mitaa hii utanitambua unaacha kusoma unafanya uzinzi...”
“Naondoka basi hayo maneno mwambie mdogo wako maana kila siku namburuza darasani pamoja na kujifanya mtu wa elimu sana huu mchezo hautaki hasira.” Dogo aliongea maneno hayo na kutimua vumbi pasi na kusikiliza neno lolote kutoka kwa Bahati. Alijua tayari hakuna jipya hapa zaidi ya kuzungushana.
Bahati alibaki akisindikiza kwa macho tuu huku akiwa amesimama palepale kama mti...😃😃🌠

Tukutane sehemu inayofuata...

ITAENDELEA...

BAKI HAPA HAPA KWENYE APP YETU, MUITE NA MWINGINE.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: BINAMU 🔞 SEHEMU YA 11

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 1-5

CHOMBEZO: MASSAGE ROOM🔞 SEHEMU YA 21