MCHUNGAJI MCHAWI EPISODE:20



Story: MCHUNGAJI MCHAWI.

Mtunzi: Nellove

Episode: 20

Ilipoishia...

"Msaadaaa!!! Nisaidieeeeee" aliendelea kupiga kelele zisizofua dafu ila alitulia ghafla baada ya macho yake kuona kitu kama uso wa mtu kwenye mbao ya juu ya jeneza ukimuangalia.

Songa nayo...

"Umefuata nini hapa????" ilikuwa sauti kali kutoka kwenye uso ule uliokuwa ukimuangalia. Mchungaji alitetemeka.
"Hii ni himaya yangu mimi peke yangu, kwanini wataka uniingilie??"
Mchungaji joshua aliendelea kutetemeka,, cha kujibu alikosa. Alibaki kujiuliza.
"Nani huyu? Je sio miongoni mwa wale wa ufalme wa kuzimu?"
Joto liliendelea kupanda nayo pumzi ilianza kukatika kwani hewa ya oksijeni haikuwepo.
"Ni mazoea yenu binadamu kuingia hata mahali ambapo hapakuhusu. Umetumia mazoea ya asili yenu ila fahamu kwamba hapa umekosea na hakika utajuta"
"Mimi sina kosa" yalikuwa maneno ya mchungaji ambayo yaliishia kwenye fikra na mawazo tu,, sauti haikutoka.

Lile joto lililokuwepo lilipanda mara mbili zaidi yani Mchungaji alihisi kama amechovywa ndani ya jiko lenye moto mkali,,, alipaza sauti kuomba msaada lakini hapakuwa na mafanikio yoyote kwani sauti haikutoka na hata wa kumsaidia hakuwepo. Machozi yalianza kutoka yenyewe baada ya kuona mchungaji anachelewa kulia.
"Nisaidie" alijitahidi kutamka ila kwa sasa mdomo ulikuwa mzito kabisa,, ilikuwa ngumu kunyanyuka.
Damu zilianza kuchuruzika kutoka masikioni mwake baada ya sauti kali mithili ya radi kupasua ngoma za masikio yake. Macho yake yaliyoyanza kumulikwa na mwanga mkali yalianza kuona kama israeli mtoa roho anamfuata kwani hali iliyokuwa inamkabili ilikuwa nzito haswaa.

Bado hakufahamu kosa lake ni lipi, na yule aliyekuwa anamuadhibu ni nani na kwanini waliompeleka hawampi msaada wowote katika kipindi kigumu kama hicho.
"Nimezikwa mzima mzima. Nakufa huku najiona" yalikuwa mawazo yaliyopita kichwani mwake. Macho yalipoteza nguvu ya kuona, giza likatawala maradufu machoni mwake na moyo wake uliacha kufanya kazi kwani hewa ilikosekana kabisa. Mchungaji Joshua alitulia kama maiti.

  †

"Baba David!!! Baba David!!" aliita Mama David huku akimtikisa mumewe.
"Sikutaka kukuamsha mapema kwasababu najua ulichelewa kulala lakini ni saa 5 hii bado umelala,,, hakika hauko sawa Baba si bure" alilalamika Mama David huku akiendelea kumtikisa Mchungaji Joshua.
"Tangu jana asubuhi hutaki kula, nakuuliza unasema hauna tatizo. Haya hii ya leo si kawaida yako kulala hadi muda huu. Una shida gani lakini???"
Mama David aliendelea kulalamika hadi machozi yalimtoka,, ule upole wa Umama Mchungaji ulitoweka,,, alikuwa anaongea kwa kufoka kudhihirisha uchungu na wasiwasi uliopo ndani yake.
"Jamani humu ndani kuna usalama?" aliuliza Mama yake Mchungaji Joshua. Mama david hakujibu chochote, zaidi aliongeza kilio tu.
Mama yake mchungaji hakuwa na mazoea ya kuingia chumbani kwa mwanae lakini sasa angefanyaje katika hali kama hii? Aliingia.

Kama ilivyokuwa kwa Mama David, Mama yake mchungaji Joshua naye alipata wasiwasi na mashaka, hakujua nini kinaendelea kwa mwanae.
"Amka Baba yangu" aliita na kumtikisa mwanae lakini hapakuwa na mabadiliko yoyote.
"Kwani hii hali imemkuta sangapi?"
"Mimi nimeshtukia asubuhi hii tu maana hata hapo jana alichelewa kulala. Ila nahisi kuna kitu hakipo sawa" alieleza Mama David.
"Sasa ni heri tumpeleke hospitali kuliko kuendelea kujiuliza hapa"
"Sawa Mama"
"Basi ngoja nikajiandae" alisema Mama yake Mchungaji Joshua na kutoka haraka.
Mama David aliamua kujipumzisha kwa kukaa kitandani huku mkono wake wa kulia akiutupa shavuni mwake,,, alishika tama.
"Mamaaaaaaaaaaaa!!!!" alipiga kelele Mama David na kukimbia mara baada ya kushikwa begani ghafla.
Hakujua kama ni Mume wake ndiye aliyekuwa amemgusa baada ya kuamka muda mfupi tu.
"Mbona unanikimbia!!"
"Aaah! Umenishitua" alisema Mama David huku anahema.
Alitulia kidogo na kurudi kitandani alipokuwepo wakati huo sio muda mrefu Mama yake mchungaji Joshua aliingia.

"Ooooooh!" Alishtuka na kuongeza.
"Jamani MUNGU ni mkuu"
"Kwanini Mama na kuna nini kinaendelea?"
"Baba tangu jana ulivyoingia kulala ndo unaamka sahivi. Saa tano dakika 50 hii" alizungumza Mama David.
Mchungaji alishituka kidogo kusikia hivi,,, na si kwamba alishtuka kwa sababu ya taarifa ya kutoamka tangu alale,, hapana. 
Ni hivi ile hali ya pale ndani ilimkumbusha kwamba alikuwa na mtihani wa kufanya na anakumbuka mara ya mwisho alikuwa eneo la kufanyia mtihani wake na tayari alishauanza mtihani ule aliotakiwa kuufanya kwa takribani siku tatu. Sasa kilichomshangaza nikuhadithiwa na mke wake kwamba tangu alale JANA.
"Kwahiyo ule mtihani nimeufanya kwa usiku mmoja badala ya siku tatu kama nilivyoambiwa?? Kwanini?" alijiuliza kichwani mwake hata hivyo hakupata muda wa Kujijibu ama kujiuliza zaidi,, Mama yake alivuruga mawazo yake.
"Tangu jana asubuhi haukula,, vipi una tatizo gani mwanangu?"
"Mama mimi sina tatizo lolote ila pia naomba kwa sasa mniache nipumzike kidogo"
"Basi uoge ndo upumzike" aliongea Mama David
"Sawa Mama"

Mchungaji joshua alijilaza kitandani na kuruhusu hili na lile kupita kichwani mwake.
"Hili linawezekanaje? Inawezekana vipi ufalme wa kuzimu ukaahirisha ama kubadili walichopanga? Lakini pia kama haiwezekani kubadili sasa mbona nimerudi kabla ya siku tatu kutimia!!" Mchungaji Joshua aliendelea kujiuliza swali lile la mara ya kwanza. Jibu lilikosekana,,, aliamua kupotezea hili suala.
"Yule niliyemuona makaburini na kunitesa ni nani? Ni kutoka himaya gani na kwanini anifanyie vile?" Mchungaji alijiuliza maswali hayo huku akiendelea kukumbuka mateso aliyoyapata akiwa kule. Kitu kimoja kilimshangaza na kumuumiza sana,,, kwanini waliompeleka kwenye mtihani huo hawakutaka kumsaidia ikiwa nguvu na uwezo wanazo?
"Hawajali kuhusu mimi kwa maana hiyo siku moja wanaweza kuniacha nife kabisa" alizungumza peke yake na baada ya kuwaza sana basi alifikia maamuzi yake mwenyewe,, waswahili huita maamuzi magumu.

"Maji ya kuoga yapo tayari,,, Jiandae Baba" alikuwa Mama David
"Nashukuru sana" 

                                             †

Mchungaji alichoka sana hivyo hakutaka kuchelewa kulala. Majira ya saa nne nyumba nzima walilala ila ilipofika saa 7 usiku Mchungaji Joshua aliamka akihitaji kwenda kujisaidia. Sasa bwana,,,,
Lilikuwa jambo la kushangaza sana kwa mchungaji wakati anainuka,,, alishangaa anainuka kutoka ndani ya jeneza na si kitandani. #OMG
Alikurupuka haraka na kutoka mle ndani akiwa na wasiwasi mkubwa kwamba labda yupo kulekule makaburini,, moyo ulidunda kwa kasi tena bila mpangilio.
Lile giza lilimuogopesha Mchungaji Joshua,,, sasa katika tembea yake ya hovyo hovyo alijikuta akiparamia ukuta na kubonyeza swichi,, taa ziliwaka. Looh! kumbe alikuwa ndani ya nyumba yake katika chumba kile cha siri,, moyo wake ulipata amani kidogo.
"Hongera sana. Wewe ni mwanafunzi bora kwetu" ilisikika sauti nzito. Mchungaji joshua aligeuka kwa wenge alitazama huku na huku ila mzungumzaji hakuonekana.
Hakutulia,, alizungusha macho yake pande zote mwisho aliona kivuli kilichokuwa kikitembea ukutani taratibu. Alishtuka kidogo ila alijikaza na kuuliza.
"Kwanini?" aliuliza Mchungaji huku akiyatembeza macho yake kila upande kile kivuli kilipojongea.

"Umeufanya mtihani wako kwa viwango na uaminifu wa juu sana,, siku tatu zimetimia hivyo lazima upate tuzo ya matokeo ya Kile ulichofanya" 
Mchungaji alichanganyikiwa kidogo kusikia kumbe hata hizo siku tatu zimetimia,, sasa zimetimiaje??? Hili swali lilikula nguvu ya ubongo wa mchungaji joshua. Angeuliza wapi haya maswali kama sio hapa hapa ambapo majibu lazima yapatikane tu.
"Nina maswali" mchungaji alizungumza.
"Ahahahahahahah! Najua unachotaka kuuliza,, ni kwa sababu ya uchanga wako. Ukikua utakuwa na nguvu ubongoni mwako itakayochakata mambo mbalimbali na kuyapatia majibu yake. Hata haina haja ya kuuliza juu ya kilichotokea,, sasa kaa tayari kufahamu na kuelewa "

Mchungaji Joshua alitulia kimya huku moyo wake ukiripuka kwa hamu na shauku kubwa ya kufahamu haya.
"Ingia ndani ya jeneza lako"
Mchungaji alifanya kama alivyoambiwa na baada ya dakika kadhaa lile jeneza lilianza kupaa. 
Ni mfano wa Mchawi arukaye na ungo ndivyo mchungaji Joshua alivyokuwa akipaa akiwa ndani ya jeneza,, kile kivuli kilikuwa kinaelea nyuma yake.
"Sasa utaoneshwa kila kilichokuwa kikiendelea" sauti ya kile kivuli na iliposikika tu ulitokea mwanga mkubwa zaidi ya ule wa mbalamwezi. Ule mwanga uliangaza pande zote na walipofika maeneo ya makaburini kule Kola lile jeneza lilishuka karibia na kutua aridhini.
Mwanga ule ulimulika eneo kubwa na sekunde chache tu macho ya Mchungaji Joshua yalishuhudia idadi ya watu watano eneo lile.

"Unaowaona pale ni mzee wa mitihani, mzee Jangala, mzee Makusi na mzee Lunde."
"Na yule mwingine ni nani?" Aliuliza Mchungaji
"Yule mwingine aliyevalishwa sanda ndio wewe mwenyewe"
Mchungaji alishtuka kidogo,,, maelekezo yaliendelea.
Mchungaji Joshua aliendelea kuoneshwa matukio yote yalivyokuwa, tangu wanafika kaburini hadi anaachwa kisha zinatokea maiti, Zinamkamata na kumzika.

"Hizo kelele zinazosikika ni zako ukiomba msaada."
"Mmh!" Mchungaji aliguna 
"Najua pia una maswali mengi juu ya ule uso uliouona. Unahitaji kufahamu ni nani na kwa nini amefanya vile na pengine imewezekanaje kutoka kule. Sasa angalia mwenyewe"
Mchungaji alikaza macho kuangalia. Macho yake yalimuona mtu mmoja akitembea hapo makaburini huku mikononi mwake akiwa ameshika mguu wa maiti fulani akiiburuza kuelekea kwenye kaburi fulani na kuanza kufukua taratibu.
"Hilo kaburi analofukua ndio hilo ulilokuwa umezikwa Wewe. 
"Wakati anafanya hayo mimi nilikuwa wapi?" Aliuliza Joshua
"Ulikuwa mlemle ndani ya kaburi."  Sauti kutoka kwenye kivuli kile.
Mchungaji Joshua aligeuka tena na kuendelea kuangalia matukio yale.
Walimuona Yule mtu akiendelea kufukua kaburi hadi alipofanikiwa kulikuta jeneza ila katika hali isiyo ya kawaida alishangaa kuukuta mwili wa mtu mwingine ambaye ndiye mchungaji Joshua sasa aliyekuwa amezikwa humo.

"Hizo kelele za hasira ni za yule mtu na hicho kilio ni cha kwako wakati anakutesa" yalikuwa maelezo kutoka kwa kile kivuli ambacho kwa sasa kilianza kuonekana fuvu.💀
"Kwanini sasa mlikuwa hamnipi msaada?" Aliuliza huku akiendelea kutazama  alivyokuwa anateseka,,, akajionea huruma.

    †

HAYA Mchungaji Joshua anaendelea kuoneshwa matukio yaliyomkuta.

BILA SHAKA ANACHOONESHWA KITAJIBU MASWALI YAKE 
HAYA👇

👉Yule aliyekuwa anamtesa ni nani haswa?

👉 Mchungaji Joshua aliwezaje kutoka kwenye mateso yale?

👉Je siku tatu zimetimia kweli?

👉Ikiwa Mchungaji Joshua alikuwa makaburini,, nini kilikuwa kinaendelea hadi nyumbani wakawa wanamuona bila tatizo?
        

      ITAENDELEA.......

BAKI HAPA HAPA KWENYE APP YETU, MUITE NA MWINGINE.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: BINAMU 🔞 SEHEMU YA 11

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 1-5

CHOMBEZO: MASSAGE ROOM🔞 SEHEMU YA 21