HUKUMU YANGU SEHEMU YA 5



STORI: HUKUMU YANGU

MTUNZI: JrLukoo ✊🏿

SEHEMU YA TANO (05)

Ilipoishia sehemu ya nne

"Achana na mwanangu, acha kabisa yule ni mke wa mtu nishakula na kifunga uchumba"

Baada ya mkwara huo mzito mzee Matata aliondoka.
Kichwani mwa Hakimu kulitawaliwa na mambo mengi yaliyomchanganya akili yake.
Kwanza harufu ya kifo alichokikwepa dakika chache zilizopita lakini pia suala la kukutana na Jesca kabla hajaondoka.

Songa nayo.......

Kwa unyonge huku moyo wake ukitawaliwa na hofu kuu.
Hakimu alijizoa zoa chini pale na kunyanyuka kuelekea alipoweka nguo zake.

Alijikaza kiume na kuendelea kufua nguo chache zilizobaki. Umuhimu wa kuzitakatisha nguo zile haukuwepo tena, hamu yake kwa wakati ule ilikua ni kumaliza tu kuzipakaza maji nguo zile na kuanza safari ya kurudi nyumbani.

Siku ile Hakimu hakuzianika nguo zile kule kule mtoni kama alivyozoea bali kwani moyo wake haukua na amani tena na eneo lile.
 Baada ya kumaliza haraka Hakimu alibeba ndoo iliyokua na nguo ndani yake na mkono mwingine akishika begi na viatu alivyovifua.

Muda mfupi baadae Hakimu alishafika nyumbani, alimkuta bibi yake ambae tayari alishamuandalia chakula cha mchana.

"Kulikoni mume wangu mbona umechelewa sana kurud leo? Na kama haupo sawa kunani tena mume wangu?" 

Bibi alimpokea Hakimu na mfululizo wa maswali mawili ya kumdadisi yakifungaman na utani ndani yake.
"Mmmmh unawivu nawe mke! Yaani hata nisicheze huko mtoni!

Na kwa wivu huo nitakuongezea bi mdogo awe anakusaidia majukumu maana si unaona mbavu inavyotanuka".

Yalikua ni maneno ya mzaha ya Hakimu kwenda kwa bibi yake.
 Hayo ndio maisha ya Hakimu na bibi yake siku zote, utani na mizaha ya hapa na pale. Imechuka sehemu kubwa ya maisha yao ili kuing'arisha furaha yao.

"Hahahahha ebu toka hapa nisije nikakivunja kibinti cha mtu na ole wako nikusikie. Nitawategua kiuno wewe na hicho kibinti chako"

 Kicheko cha bibi kilipokea maelezo ya Hakimu.

"Hahahaa sawa tu mie sina usemi. Enhe chakula umeniwekea? Hakimu aliuliza mara baada ya kukubaliana utani wa bibi yake.

"Ndio tena enhe nilitaka kusahau, nenda kachukue chakula uje ule hapa  kuna maswali nataka kukuuliza hapa" 

bibi Hakimu alisema.

"Mmmh sawa"
 Hakimu alikubaliana na maneno ya bibi yake.

Baada ya muda mfupi Hakimu tayari alishaketi kando ya bibi yake kwenye mkeka chini ya mti wa mwembe ulikokua kwenye uwanja wa nyumba yao.

"Enhe kitu gani tena hicho?"
Hakimu alimuuliza bibi yake.

Bibi yake Hakimu alianza kueleza
"Mjukuu wangu umekaa nami hapa kijijini kwa muda sasa. Kwa muda wote huo rafiki yako mkubwa amekua yule binti wa mzee Matata. Na tayari nishaanza kusikia sikia huko mtaani. Sasa naomba unambie ukweli kama ndio tayari sisi tuandae mahari".

"Hapana bibi hakuna kitu ni utafiki tu" 
Haraka Hakimu alikinzana na mawazo ya bibi yake.

"Aya sawa wewe wasema lakini kama ni kweli na unanificha ni kheri ukae kando nae, maana mzee Matata nimjue mimi hapa kijijini haingiliki. Tena ukicheza na binti yake mmmh ni kheri hata ucheze na kitoto cha chatu. Yule mzee puuuu! Ni Mtata kama lilivyojina lake"

Bibi Hakimu alimtahadharisha mjukuu wake kiasi cha kutema mate chini (puuu!) kama ishara ya kutilia mkazo maneno yake.

Maneno ya bibi yalizichukua fikra za Hakimu na kuzirudisha tena mtoni kule tayari taswira ya vitosho vyote vya mzee Matata ilitawala ndani ya akili yake.

Alijikaza kiume ili bibi yake asiweze kugundua hofu aliyonayo moyoni mwake.

Hakimu hakua tayari kabisa kuondoka bila ya kuonana na Jesca licha ya hatari aliyokwisha kuionja.

Dakika zilizonga masaa yakakatika hatimae saa 12 jioni muda wa Hakimu kukutana kama walivyoahidiana ulikaribia.
 Haraka Hakimu alimuaga bibi yake kuwa anaenda kucheza na asingekawia kurudi.

Baada ya baraka za bibi yake
 Hakimu alitoka nyumbani na kuelekea kwenye njia ya kuelekea bombani kwa kina Jesca.

Alijitega kando ya mwembwe ili hata akipita mtu asimuone na kumtilia shaka juu ya uwepo wake eneo lile.
Baada ya dakika tano Hakimu alisikia vishindo vya miguu kuashiria kuwa kulikua na mtu aliyekua anakaribia eneo alilopo.

Hakimu aliangaza macho njiani na kumuona Jesca aliyekua na ndoo ndogo ya maji.

Baada ya kufika eneo lile walilokubaliana Jesca alipepesa macho pande zote ili kumtia machoni Hakimu.

Hakimu nae alivyogundua kuwa macho ya Jesca yalikua yakimtafuta yeye alizunguka kwa upande wa nyuma wa Jesca.

Kwa mwendo wa kunyata Hakimu alimsogelea Jesca na alipomfikia  alimsogezea mikono yake kutokea upande wak wa nyuma na kufanikiwa kumziba macho yake.

Jesca alishtuka kwani hakugundua kama alikua ni Hakimu

"enhe otea ni nani  mimi?"
 Hakimu alimuuliza Jesca

"Niiiachie bhana Hakimu unaniumiza macho mie" 
Sauti nyororo ya Jesca iliitikia maneno ya Hakimu.

"Daaah leo ningekufa mimi"
maneno ya Hakimu kwenda kwa Jesca.

Kwa shauku Jesca alimuuliza Hakimu

"Enheee kulikoni tena mwenzangu?

Hakimu alimweleza mawashimu yote aliyokutana nayo siku ile kutoka kwa Baba Jesca.

Jesca alidakia

"Mhh poule ebu potezea hizo habari za baba, natakiwa kuwahi kurudi nyumbani" .

Haraka Jesca alimuamuru Hakimu wasogee pembeni kidogo kwani pale palikua njiani.

Hakimu bila kipingamizi alitii amri ile na kumfuata Jesca kwa nyuma ambae tayari alishaongoza njia kuelekea kwenye kichaka kidogo kilichokuawepo maeneo yale.
Jesca alipohisi kufika eneo lenye usalama zaidi alimgeukia Hakimu na kumkumbatia Hakimu kwa nguvu saana. Huku kichwa chake akiwa amekilaza kwenye bega la Hakimu.

" Samahan kama nitakuuzi au haukutegemea hichi kitachotokea. Kiukwel hata sikuwa na jambo la kutisha saana kama ambavyo nilikueleza jana. Ila nilitumia mbinu ile ili uone umuhimu wa kuonana na mimi kabla hujaenda mjini" 

Jesca aliweka kituo na kisha kuendelea.

"Siwezi kuficha tena hisia zangu kwako, naona moyo wangu umekua mzito saana. Na hii yote inasababishwa na kitu kizito nilichokibeba ndani yake. Ni kheri niufanye moyo wangu uwe mwepesi leo nimeamua kuutua huu mzigo. Naomba sana Hakimu nikubalie niutue huu mzigo".

"Hakimu nakupenda saana, natamani siku moja uje kuwa baba wa wanetu tutaojaliwa mimi na wewe.
Siwezi tena kuendelea kubaki na huu mzigo wa maneno ndani ya moyo wangu"

 Maneno mazito ya Jesca yalipenya vilivyo kwenye moyo wa Hakimu.

Bila kupoteza muda Jesca hakutaka kumpa Hakimu nafasi ya kujieleza.
Alivamia mwili wa Hakimu mithili ya mbwa mwenye hamu ya kitoweo.

"Hakimu sijawahi kukutana na mwanaume tokea nizaliwe, japo wengi wananitaka lakini msimamo wangu siku zote ni hapana. Kwako nimeamua kukutunuku uwe mwanaume wa kunitoa usichana wangu"

Maneno ya mahaba ya Jesca ambaye kwa sasa sauti tu ilionyesha ameshatawaliwa na tamaa za mwili.

Hakimu hakua mbali mwili ulimtuma kucheza kulingana na biti.
Akajikuta anaanza kuitikia tamaa za mwili zilizoshamiri kwenye mwili wake.

Wakati hayo yote yanaendelea giza lilishaanza kutanda. Ghafra walihisi sauti ya Mzee Matata akiwa anafoka pekeyake huku akishika njia ya kwenda kisimani.

"Atanieleza vizuri huyu mpumbavu kama hayo maji anachimba chini au anasubiri mvua inyeshe akinge".

Jesca na Hakimu waliyasikia vizuri maneno yale ya Mzee Matata.

Kwa kasi mzee Matata alielekea kisimani. Huku maneno makali na ya hasira yakimtoka kinywani mwake.

Wakati huo wote Hakimu na Jesca walikua kwenye hofu isiyo kifani. Lakini wote wawili hawakua tayari kupingana na hisia za miili yao.

Punde si punde sauti ya Mzee Matata ilisikika tena kuashiria kuwa alikua anarejea kutokea kisimani.

"Huyu mpumbavu ndie atakae kuwa anamvuruga binti yangu walai nitamkata miguu safari hii kabla hata hajatoroka kwenda mjini.

Hapa ni mguu wangu moja kwa moja kuelekea kwa bibi yake. Akanieleze vizuri mjukuu wake amemuweka wapi mwanangu. Na nisipopata majibu ya uhakika nitamzaba vibao na huyo bibi yake"

Mzee Matata alifoka  akiwa amesimama kando ya njia kidogo walipo Hakimu na Jesca. Huku akiifakamia bange kwa pupa kupitia kinywa na pua yake.

Jesca na Hakimu walitulia kwa muda kila mmoja akijikaza walau hata mapigo yake ya moyo  yasidunde kwa kasi sana.

Je wataweza kupambana na tamaa za miili yao kukatisha walichokua wanaanza kukifanya? ❤️😋

Jesca afanyaje ikumbukwe hata kisimani kwenyewe hajaenda bado.

Hukumu ya Hakimu ni kama inanukia hivi.

    ITAENDELEA....

BAKI HAPA HAPA KWENYE APP YETU, MUITE NA MWINGINE.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: BINAMU 🔞 SEHEMU YA 11

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 1-5

CHOMBEZO: MASSAGE ROOM🔞 SEHEMU YA 21