TWINS (MAPACHA) PART:02



TWINS (MAPACHA)

MTUNZI:OFFICIAL IBRAAH JUNIOR

PART:02

ILIPOISHIA....

Siku moja Kurwa alikaa sehemu na kumwangalia sana Majaliwa, ilikuwa ni siku za mapumziko, Majaliwa alikuwa akisafisha bustani ya kwao huku Kurwa akiwa anamwangalia kwa jicho regevu lenye mahaba ndani yake...

SONGA NAYO...
"vipi wewe tena, naona unataka kuimaliza pen kwa kuitafuna" Dorice Alitokea nyuma ya Dorine na kumkuta Dorine akiwa anatafuna pen tu huku akimwangalia Majaliwa

"Aah! Hana bana" Dorine alishituka kwenye dimbwi zito la huna kwa Majaliwa

"Hamna nini, na nakuona hapo sijui umefeli wapo usaidiwe" Dorice aliongea 

"Nawe ushaanza sasa, si kaendelee na mambo yako, mtu mwenyewe wa kidato cha kwanza, niache nina mawazo yangu ya pepa hapa" Dorine mfululizo na kumfanya Dorice agune tu 

"Mmhh!  Nawe haya, ila useme usaidiwe" Dorice aliongea na kufanya kuzuka kwa mjadala mzito wenye mabishano imradi tu, uitwe ugomvi 

"Haya nyinyi sura mbili mshaanza sasa, ndo tabu yenyewe hii kuwa na mapacha" Majaliwa ambae alimaliza shughuli zake, alisikia mjadala na fujo tu na kuingilia kati

"Si huyu nae sijui yupoje" Dorine aliongea kwa aibu

"Aahh! Acha niwaache, piganeni halafu mkimaliza mkakoge tuje tule"Majaliwa Aliongea na kuondoka, huku akifatiwa na Dorine. Siku zote mabinti hao mda mwengine walikuwa wanaelewana ila ukifika mda wa tafaruko ilikuwa ni balaa. Ilikuwa ni siku ya jumapili siku ya mapumziko siku iliyofata Majaliwa aliwasili shule mapema na kukaa mstasrini na baada ya dakika chache aliingia darasanii. Ilikuwa ni shule kubwa ya bweni, shule ilizungushiwa feni kubwa, Wakati Majaliwa anaingia Darasani alikuja binti mmoja na kumuulizia

"Majaliwa yumo humu" Binti huyo alikuwa anajuliakana kwa jina la Agnes 

"Nipo, vipi kuna tatizo" Majaliwa aliumuliza Agnes

"Hapana unaitwa ofisini na umeambiwa tuongozane" Agnes aliongea 

Majaliwa aliacha kazi yake ambayo kila kukicha ilikuwa ni destuli yake kufika na kusolve paper kama mwalimu wa zamu hajawasili darasani. Alinyanyuka na kuongozana na Agnes hadi nyuma ya shule yao kwenye madarasa

"Vipi huku ni wapi" Majaliwa aliuliza 

"Kwani nilimwambia wapi" Agnes nae aliuliza swali

"Si kwa mwalimu au"

"Ndio"

"Sasa huku kwa mwalimu,na kwanini aniite kwenye chochoro wakati sheria tunaenda ofisini?, usinisababishie matatizo" Majaliwa aliongea maneno mengi, lakini alisita baada ya kuangalia mbele na kumuona Dorine 

"Dorine"
Majaliwa alimwita Dorine ambae alikuwa anaona aibu tu huku akichezea vidole vyake 

"Beehh!"

"Huyo ndo alikuita" Agnes aliongea kwa tabasamu 

"Yaani wewe ndo uliyenita, sasa ndo mpaka huku hujui ni hatari, na wewe kwanini umenidanganya?" Majaliwa aliongea sana bila kituo 

"Agnes asante sana unaweza ukaenda, na Majaliwa wala usimlaumu Agnes mimi ndo niliyemtuma" Dorine aliongea huku Agnes akiondoka kwa mwendo waadaha na kuifanya siketi fupi na mirinda kutikisika tu. Zikapita dakika nyingi bila Dorine kuongea chochote alibaki kuchezea vidole tu, ndipo Majaliwa alipoamua kuvunja ukimya

"Mbona kimya, haya niambie ulichoniitia basi" Majaliwa aliongea 

"Aahh!  Hata sijui nikwambie nini?" Dorine aliongea huku akiwa anaendelea kuchezea vidole vyake

"Mmhh!  Ushaanza, toka juzi unaniita kama hivi halafu huongei" 

"Badae bana nitamwambia"

"Mmhh! Sawa, acha niwahi darasani, maana kuna kipindi saivi" Majaliwa aliongea 

"Haya sawa"
Dorine alijibu huku bado anachezea vidole vyake. Majaliwa akatoka eneo hilo mbio kuarakia darasani, wakati huo Dorine alikuwa anajilaumu tu kushindwa kumueleza ukweli wa moyo wake, alitoka katika eneo hilo na kuelekea moja kwa moja kwenye bweni za wasichana

"Vipi Dorine, umemueleza au, naona mnyonge sana" Agnes aliongea baada ya kumuona Dorine alikuwa mnyonge 

Dorine alikaa kimya tu, ndipo Agnes akaongea tena "kwani umefanya  nini, niambie basii" 

"Aahh!  Shoga weee" Dorine aliongea na kusita 

"Shoga nini au hajakubali" 

"Bora angekuwa hajakubali, ingekuwa afadhali" 

"Kumbe Kafanya nini" 

"Nimeshindwa kuongea" 
Dorine alijibu na kumfanya Agnes achukue 

"Nawe kila siku, ndo unabaki kutoa lawama tu, ngoja aje achukuliwe na wengine ndo utajifunza"

"Heehh!  Punguza Basi maneno makali shoga angu niambie nifanye nini" Dorine alisita  kongea na kuvuta pumzi juu na kusema tena "Au nifanye ile plan B niliyokwambia"

"Plan gani? Ile ya kupeleka barua?"
Agnes alimuliza Dorine 

"Ndio"

"Haya sawa maana kuongea ndo huwezi"

"Ndio hivyo shoga, pia naomba unaisaidie kuipeleka kwa Majaliwa" 

"Mimi tena huyo, aahh!  Siendi wewe nenda tu" 

"Naomba"

"Mmhh!  Sawa ikishindikana basi"

"Sawa"
Agnes alichua barua na kumpeleka Majaliwa ambae aliipokea. Mda ulipomaliza walirudi nyumbani ndipo akakumbuka maneno ya Agnes "Soma barua hii ukifika kwenu ndo utajua nani aliyekuandikia". Majaliwa alikuwa na shauku ya kuisoma barua ile, aliacha buku ambalo alilokuwa anasoma na kuanza kuitafuta barua ile kwenye mkoba wake, alipata na kuifungua, alistaajabu baada ya kuanza kuisoma... 

'WAKO DORINE, NATUMAINI UMZIMA WA AFYA, MAJALIWA SAMAHANI KWA NITAKACHOKUELEZA, PIA HUWA NAONA AIBU KUKUELEZA NIKIKWITA, MARA ZOTE NILITAKA NIKWAMBIE NAKUPENDA SANA, NAHITAJI UWE MUME WANGU, MTU PEKEE WA MAISHA YANGU..!'

Majaliwa alisita na kusoma barua ile na kuanza kujiuliza mengi kichwani mwake, alichukua tena barua na kuendelea kuisoma 

'NAOMBA UNISIKILIZE WALAU KILIO CHANGU, MOYO WANGU HAUNA AMANI KWA AJLI YAKO, ASANTE SANA NATUMAINI OMBI NZURI KUTOKA KWAKO'

Majaliwa alimaliza kuisoma barua na kushusha pumzi nzito... 

ITAENDELEAA....

BAKI HAPA HAPA KWENYE APP YETU, MUITE NA MWINGINE.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: BINAMU 🔞 SEHEMU YA 11

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 1-5

CHOMBEZO: MASSAGE ROOM🔞 SEHEMU YA 21