KIPOOZEO SEHEMU YA 3
SIMULIZI : KIPOOZEO
SEHEMU YA TATU
MTUNZI : MADAM YUSTAR.
Tuendeleee.....
Wakati natembea gafla niliguswa bega na mtu ambaye sikutegemea uwepo wake pale.
"Yustar mambo! " aliongea kwa tabasamu huku anacheka.
"Poa za kwako..!" Niliitikia nikiwa mkavu sana bila aibu, nilikuwa na hasira nae sana hivyo nilitamani asimbue namshobokea.
"Oooh... Samahani naitwa Jacob, ujue kuna siku uliomba namba zangu ila kwa bahati mbay nilishindwa kukuandikia kutokana na khali niliyokuwa nayo, nisamehe mama ile siku nilikuwa naumwa hivyo nilikuwa nawah duka la dawa."
Maneno yake ya upole yalinivutia sana, wala sikuona sababu ya kuendelea kumnunia wakati ameshaomba samahani.
"Aaah... Usijali sana pole kwa kuumwa, unaendeleaje sahivi?"
"Naendelea vizuri" aliongea huku anatabasamu, nilifarijika sana kumuona anavyofurahi.
"Nafurahia kusikia hivyo, mmmh umemaliza dozi lakini?!"
"Yeah.. Mama nimemaliza asante kwa kujali, hata hivyo naomba uniandikie namba zako hapa" alitoa simu yake na kunipa niandike namba zangu, haraka haraka niliandika namba bila kusita. Baada ya kuandika namba kila mmoja aliondoka na kuweza kwenda kwake.
Nilivyofika kwangu kila mda nilikuwa naangalia simu yangu kama ameweza kunitafuta, lakini haikuwa hivyo Issa alikuwa mtu pekee sana anaenijali sio asubuh wala jioni alihakikisha nakuwa sawa kwa namna yoyote ile.
Zilipita kama siku nne bila kutafutwa na Jacob, nilijiona mwenye kihere here sana lakini haikunifanya niache kusubiri meseji yake.
Kwelii alifanikiwa kunitafuta japo kwa kuchelewa, ukaribu wangu na wake ulipamba moto sana nilifurahia zaidi kuwasiliana nae kuliko Issa, hata hivyo mimi ndo nilionekana kumtafuta yeye kuliko mimi.
Haukupita hata mwezi Jacob aliweza kuniita kwake na kwa vile nilikuwa nampenda sikukwepesha chochote, nilienda bila kuogopa, nilivyofika alikuwa anachezea simu huku yupo kifua wazi alikuwa anachezea simu yake kwa dharau.
"Oooh! Umefika " aliongea huku anatoka kitandani na baada ya mda alisogea na kuweza kuzima taa, kitendo cha yeye kuzima taa kulinikosesha amani sana. Kufumba na kufumbua tayari mwanaume alishanivua nguo zote, hakuishia hapo alianza kufanya mapenzi na mimi bila hata maandalizi ya aina yoyote ile kile kitendo kilinikwaza sana, nilionanimejidhalilisha mwenyewe.
Baada ya kumaliza kufanya unyama wake, aliwasha taa na kuniamuru nivae nguo niondoke wakati tunazidi kuongea gafla simu yake iliita.
"Oooh... Mungu wangu ee my girl anapiga" aliongea huku anachukua simu yake.
"Yes.. Mama mbona hujalal hadi mda huu?"
Sikuweza kusikia sauti upande wa pili ila maongezi ya Jacob yalionyesha kabsa ni kiasi gani alikuwa anafurahia kuongea na mwanamke wake.
Machozi ya uchungu yalianza kunitoka ila nilihisi moyo wangu unauma zaidi, sikuweza kuendelea kusikiliza yale maongezi zaidi sana nilibeba kila kulicho changu na kurudi kwangu kuugulia maumivu.
Nilivyofika tu kwangu niliingia bafuni na kuweza kufungulia majii ilii niwezee kulia kwa nguvu, ujanja wangu wote leo hii nimetumika kwa dharau, lakini kilichokuwa kinaniuma zaidi ni kitendo cha Jacob kuniona kama taka taka. Wakati nazidi kulia gafla mlango wangu uligongwa......
Itaendeleaaa...
Unazani Yustar kakosea wapii? Unazani Jacob anamakosa ya aina yoyote ile? Tukutane sehrmu ya nne.
SIMULIZI : KIPOOZEO
MTUNZI : MADAM YUSTAR
SEHEMU YA NNE
Wakati nazidi kulia gafla mlangu wangu uligongwa, nilitoka kwa jaziba kwenda kuangalia anaegonga mlango usku wote ule.
"Hey..! Nani wewe unasumbua watu usku huu" niliongea huku nafungua mlango wangu mkubwa wa sebleni.
"Ooh pole kwa usumbufu mama, nimetoka huko kuonja kidogo nimeona sio sawa nikakubebea matunda enjoy!" Issa huyo aliongea kwa sauti ya kilevi, baada ya kunipa mfuko wenye matunda aliondoka zake taratibu.
"Hivi huyu chizi ananitafutia nini mimi lakini? Kwanza nani kamuonyesha naishi hapa aah.! Huuu ni upuuzi sasa atanizoea vibaya san" niliongea kwa hasira huku nikiwe nimeuma meno yangu.
Sikutaka kumfagilia sana, niliingia bafuni na kuweza kujimwagia maji, baada ya hapo nilitoka na kwenda zangu kupata glass ya juisi.
"Hivi huyu Jacob ananichukuliaje kwa mfano, hivi ananiona mimi kama takataka au toka nimeondoka kwake hadi mda huu hajapiga hata simuu kuuliza khalii yangu kwelii ana roho ya uhasama" niliongea mwenyewe huku namalizia glass ya juisi.
Nilivyomaliza kunywa juisi, nilirudi chumbani kumshukuru Mwenyezi Mungu kisha nilijipumzisha zangu.
Siku iliyokuwa inafata ilikuwa weekend , hata mimi huwa siendagi kazuni napumzika kuifanya akili yangu ijiandae kwa wiki inayofata.
Niliamka alfajiri na kufua nguo zote kisha, nilipanga ndanina kuweza kupata chakula cha mchana baada ya hapo nilikumbuka sina kifurushi, nilichukua hela ili niweze kwenda dukani kununua vocha.
Ili niweze kufika dukani lazima nipite karibu na chumba cha Jacob, nilitembea taratibu kwa madaha wala sikuwa na haraka. Kabla sijafika kwenye chumba cha Jacob nilishangaa kumuona nje anafua lakini sio yeye tu hata Issa nae alikuwa nje anafua.
Jacob alivyoniona alibinua mdomo utazani shoga wa kiume, jambo lili likinikera sana wakati nazidi kushangaa Issa aliita kwa sauti ya upendo " kichaa wangu njoo tusaidiane kufua mama"
Nilichoka mwili na roho sikutegemea kama Issa angeniita , wakati nazubaa alipita dada mmoja mzuri kaumbika haswa, alipita kwa madaha hadi alipo Jacob na kuanza kuchukua nguo za Jacob kuanika. Jambo lile lilinifanya nizidi kukasirika zaidi
.
Kwa hasira nilimfata Issa na kuanza kumfulia, nilifua kwa hasira hadi Issa mwenywe alishanga.
"Mammmy mbona kama kuna kitu kinakusumbua.!" Issa aliuliza swali ambalo lilinifanya nitamani kulia.
"Amna kitu Issa nipo sawa kabsa ondoa shaka" nilimjibu kwa upole
"kapumzike kule kwangu maana nakuona haupo sawa kabsa" Issa aliongea huku akinishila mkono hadi kwake, kwanza nilistaajabu saana baaba ya kuingia kwake, licha ya ulevi wake ila alipangilia ndani kwake vizuri sana. Nilikaa kwenye kochi la mtu mmoja, Issa aliingia kwenye friji na kuweza kunimiminia maziwa.
"Asanteee Issa" ukwelii sikutaka hata kumwangalia usoni, nilikuwa namchukia mno kutokana na ulevi wake
Sikufurahishwa kabsa na yeye kunywa pombe.
"Yu.. Mama najua huwezi kuwa na mtu kama mimi ila naomba unipe hata robo ya kuwa karibu yako, najisikia amani sana nikiwa karibu yako."
"Ooh...! Sawa usijali ondoa shaka juu ya hilo, mimi nataka kwenda dukani"
", dukani.! Unaenda kufata nini mda huu?"
"Naenda kuchukua vocha"
"Aaah... Usiende bhana ngoja nikununulie," Issah alibojeza siku yake, baada ya mda tayari alishaweza kuninunulia kifurushi. Sikutaka kuendelea kubaki pale, nilitoka nje niweze kwenda kwangu, nilivyofika karibu na Jacob aliongea kwa sauti ya chini.
"Sema una umbo zuri la kuvuti, kesho uje tena , maana leo umetoka kugawa kwa huyo cha pombe" aisee niliuma meno kwa hasira kitendo kile kilinifanya nikosea amani.
Nilijiona mpuuzi saaana kila nikimwangalia Jacob hafananii kabsa na mambo ambayo anayafanya. Niliangaza huku na kule sikuweza kumuona yule mwanamke wake.
Nilitembea haraka haraka hadi kwangu, nilivyofika kwangu nilimkuta Fety na Jenny.
"Eee shoga angu nasikia wapangaji wote wanajua tumiwa na Jacob, eeee! " aliongea Fetty kwa sauti ya kimbea kabsa.
"Yaani Yustar na ujanja wako wote umeachiwa manyoya khaa! Pole shoga angu" Jenny nae alidakia kwa sauti ya kimbea.
"Hivi nyie mnauhakika gani na hicho mnachokisema? Au mnaongea tu kufurahisha midomo?! Na hata kama kanitumia inawauma nini? Punguzeni umbea , mlishindwa nini kuja kuniuliza mwenyewe fyuu... Nitokeeni hapa." Tayari nilishakwazika alafu bado na wao wanazidi kunikwaza aaah....
"Maisha ni kujifunza shoga etu, sisi hatujakutuma kwenda kujibebisha huko ila tulichogundua Jacob ni mkaka mwenye tabia za kishetani kaa nae mbali, nasikia kapitia wapangaji wengi sana hapa na akishakupitia anatangaza "
"Mmmh! Aaah aya sawa , tokeni njee nahitaji kupumzika"
Sikutaka usumbufu wa aina yoyote ile hivyo niliomba waondoke nibaki mwenyewe, nashukuru walikuwa waelewa kila mmoja aliondoka na kuniacha pekee angu.
Nilitafakari saana maneno ya marafiki zangu ila niliona niyapuuzie sikutaka kuyaeka kichwani saaana.
Wakati natafakari meseji iliingia kwenye simu yangu, nilivyoisoma niligundua imetoka kwa Jacob, nilishtuka saana baada ya kuona ila meseji.
Haraka nilivaa na kwenda hadi kwa Jacob.....
Unazani Yustar kaona nini? Usikose kufatilia mkasa huuu.
ITAENDELEA.....
BAKI HAPA HAPA KWENYE APP YETU, MUITE NA MWINGINE.
Maoni
Chapisha Maoni