MSITU WA AJABU EPISODE:10



Story: MSITU WA AJABU

episode:10

Mtunzi: Nellove


Ilipoishia...

Jay alitoa wazo lake ambalo lilimuacha mdomo wazi kila mmoja
"Aaah hapana kwakweli,,hilo haliwezekani"alisema David na kila mmoja alipingana na wazo hilo

Songa nayo...

Jay aligeuka na kumtazama David kwa sekunde nyingi tu huku akionesha dhahiri chuki yake usoni. Japo wote hawakuwa tayari kwa wazo lake hilo ila yeye alikuwa anaona kama David ndiye mpingaji mkubwa wa wazo lake.

"Asee wewe unapinga kama nani eeh??? Kwa lipi hasa ulilonalo hata unaamua kupinga???"alifoka Jay macho kayatoa kudhihirisha namna asivyopendezwa na kitendo kile. Hakuna aliyeshughulika kumjibu,,hata David mwenyewe hakujibu,, alifunga kinywa chake.
"Sasa mkubali mkatae ni kwamba kazi hii lazima ifanyike na wazo la kujigawa ni lazima liheshimiwe"alisema kwa msisitizo mkubwa sana

Kiufupi ni kwamba Jay alitoa wazo kwamba inabidi wagawanyike kimakundi kwa madai kwamba ikiwa hivyo basi kazi itafanyika haraka sana kuliko wote wakiwa pamoja. Wenda ni wazo zuri lakini kwa mazingira yale ambayo hatari yake ilishajulikana hili wazo halikuwa na usalama kabisa.

"Sawa Jay lakini unachofanya sio kizuri,, kumbuka sisi ni kundi hivyo linapotokea jambo fulani ni lazima tushirikishane na kujadili kwa pamoja na sio kufosi kama ufanyavyo,, hili ni kundi bwana"alisema kwa kulalamika Donald.
"Ahahaha!! Asee kama hili ni kundi basi mimi ndio kiongozi wa kundi,, kwahiyo hakuna namna"aliongea kimzaha Jay ila ndio alishasema hivyo.

"Hatuna muda wa kupoteza,, Rose, Stewart Queen,David, na Suzy mtakuwa kundi moja alafu Nuru ,Donald, Daniel, Martha na Zachariah mtakuwa pamoja kisha Steven, Mariam, Evar tutakuwa wote na mimi,,, sisi tu ndo tupo wanne,,nahisi Emmanuel angekuwepo ,nasi tungekuwa watano" alisema kiutani pasipo kujua kama alimkumbusha Queen kutoweka kwa mpenzi wake.

Hakukuwa na mtu yeyote aliyejaribu kubisha zaidi walibaki kunyong'onyea kila walipowaza kugawanyika,,, wengine walikuwa makundi tofauti na wapenzi wao. Ukiacha mengine yote Steven alifurahi kuwekwa kundi moja na mpenzi wake ila kisanga ni pale alipoona kuwa hata Evar naye yupo ndani ya kundi hilo hilo. Mmmh

"Kila kundi uelekeo wake tafadhali,," alisema Jay na kuongoza njia ili kundi lake limfuate. Wenye wapenzi ambao walikuwa katika makundi tofauti walitumia wasaa huo kuagana huku wakipeana faraja ya kwamba watamaliza salama japo kiukweli hakuna aliyekuwa na uhakika wa kutoka ndani ya msitu huo. Wenye mioyo mepesi walishangaa machozi yakiwatoka bila ridhaa yao,, huzuni ziliwashika,,lawama kubwa zikirushwa kwa Jay.

Hawakuwa na budi kukubali hali halisi iliyopo. Walitembea kila kundi upande wake huku wakiandaa vijidaftari vyao vidogo ili kuweza kuandika vitu vya msingi wakati vitakapohitajika.

Uchunguzi ulianza kufanyika mdogo mdogo wakianza kuchunguza mimea mbalimbali inayopatikana ndani ya msitu huo,, uchunguzi uliendelea na kuhamia juu ya aina za miti(species) zilizopo katika msitu huo.

Hapo ndipo walipopigwa na butwaa,, jinsi ilivyo ni kwamba kuna vitu walikuwa wanachunguza katika kujua aina fulani ya mti huo mfano mizizi ya mti huo na jinsi ilivyosambaa,, Magome ya miti na saizi ya upana wa magome hayo,, kimsingi ni vitu vingi sana ambavyo walitumia katika uchunguzi wao.

Sasa maajabu ni kwamba mti wa aina fulani uliweza kuonekana una sifa za mti wa aina tofauti kabisa na mti huo. Kitaalam ni jambo la kushangaza japo si sana kwa mtu ambaye si mtaalamu wa masuala hayo. Jambo ambalo lilishangaza waziwazi ni namna ile miti ilivyokuwa inatokwa na maji baada ya magome yake kubanduliwa alafu sasa baadhi ya miti yenyewe iliyotoa maji ilikuwa imekauka,, la ajabu zaidi ni namna maumivu yalivyokuwa yanatawala miili yao yani kama wanachanwa ngozi kadri walivyokuwa wanabandua magome yale.

Ule upande wa kundi la akina Donald na wenzake nao waliendelea ila hali ilikuwa vilevile kama huku kwa akina Steven.
Yalikuwa ni mambo ya kutisha sana.iliwalazimu kuweka kambi kutuliza miili yao ambayo ilikuwa na maumivu mengi ambayo hata chanzo chake hawakukifahamu.
Walijituliza hapo wakitafakari namna kazi hiyo inavyowatoa jasho kali lisiloelezeka.
"Jamani hadi kufikia hapa nimechoka na sidhani kama tutaambulia chochote kuhusu uchunguzi huu,,,sio kwa maajabu haya jamani"alisema David huku anavua shati lake baada ya kuhisi joto lisilo la kawaida mwilini. Aliinuka na kwenda kuliweka ndani ya hema kisha aliamua kutoka akiwa tumbo wazi ili angalau upepo umpige.

Lilikuwa ni jambo la ajabu sana kujisikia joto ndani ya msitu uliokuwa na upepo wenye baridi lililowafanya wengine kuvaa masweta. David alitoka akielekea mahali walipo wenzake ila alishangaa mno kuona namna wenzake walivyokuwa wanamuogopa kila walipomuangalia.
"Heee jamani,,imekuwaje tena wananiogopa wakati sahivi tu tulikuwa wote?? Au sababu nimevua shati"alisema na kujichunguza mwilini wala hakuwa na tatizo lolote lile. Aliendelea kuwafuata.

"Mamaaaaaaaaaaa nakufaaaa,,, usinifuateeee"Alikuwa Suzy aliyekuwa ameanguka wakati anajitahidi kukimbia.

👉Nini kinaendelea hapa???
👉Vipi kugawanyika kutajenga ama kutabomoa hata kilichojengwa???

👉Mariam, Steven na Evar kundi moja,, itakuwaje hapa??

Maswali ni mengi ya kujiuliza

ITAENDELEA....

BAKI HAPA HAPA KWENYE APP YETU, MUITE NA MWINGINE.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: BINAMU 🔞 SEHEMU YA 11

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 1-5

CHOMBEZO: MASSAGE ROOM🔞 SEHEMU YA 21