MSITU WA AJABU EPISODE:09



Story: MSITU WA AJABU

episode:09

Mtunzi: Nellove


Tulipoishia...

".....vipi na mimi nikisema yale niliyoyaona usiku??,, inahitaji moyo,,hii kazi ni nzito,, tumevamia pasipovamiwa"

Songa nayo...

Kila mmoja alikuwa kimya kusikiliza kitakachosemwa na Emmanuel,, yani hata wale waliokuwa wanampinga Steven midomo yao ilifungwa,,macho kodo,,masikio ndii yamesimama vyema kusikiliza hayo maajabu ambayo huenda yangeogopesha moyo. Emmanuel alitulia kimya kama mtu ambaye hakujua ni wapi aanzie kusimulia matukio hayo.

"Nilisikia sauti ya kilio kikubwa cha mwanamke huku nje,, nilitamani kutoka ila niliogopa sana kwani niliamini hiyo ni mizuka ya humu msituni,, niliendelea kusikia ile sauti na jinsi muda ulivyokwenda ndivyo sauti iliposikika kwa ukaribu zaidi yani kama aliyekuwa analia yupo karibu na sikio langu,, hata hivyo niliitambua sauti ile,, nilishangaa sana kwani ile sauti ilikuwa ya Mariam"alieleza hayo kwa umakini mkubwa huku akipangilia vyema maneno yake. Hakika kipaji cha kuelezea Alikuwa nacho.

Hizi taarifa zilimshitua kila mmoja hasa Mariam na Steven,, waliona ni uzushi sasa kwa sababu wao walikuwa ndani na hata kutoka kwenyewe hakutoka Mariam. Kwanza wewe unafikiri angeanzia wapi kuinua mguu atoke,,, alafu woga atakuwa ameuacha wapi??? Hizi taarifa zilikuwa kama hadithi zozote za kutunga hasa zile za babu kusimulia wajukuu kuhusu zimwi.

Emmanuel aliendelea kusema
"Baada ya kutambua ni nani hakika nilikosa nguvu ya kuendelea kubaki mule ndani,,nilijikaza nitoke kwenda kuchunguza ilo kama ni Mariam kweli basi nimuokoe,, nilitoka taratibu hadi mlangoni na kiukweli niliishia hapo kwani nilipomulika tochi nilishtuka kwa nilichokiona,,, niliona kiumbe cha ajabu sana yani kama alikufa basi kitambo mno kwani baadhi ya sehemu za mwili wake zilikuwa mifupa tupu ,,nyama zilikuwa zimetoweka,, hiyo haikunifanya niogope sana,, kilichoniogipesha mno ni namna Maria... Ma.. mar.. maaaa..." Alianguka chini huku anarusha mikono huku na huku na povu lilishasambaa kinywani mwake.

"Ooh my God,,ni nini tena"zilisikika kelele za kila mmoja akiwa haamini macho yake. Hofu ya kumpoteza mwenzao ilikuwa kubwa sana na walipojaribu kujiuliza juu ya sababu iliyopelekea awe hivyo hawakujua kabisa,,, hawakujua wanafanya nini ili kumuokoa mwenzao ambaye haki yake ni mbaya hadi mbaya tena,,

"Jamani naomba begi langu,, kuna zile dawa za kutuliza hali hii,, fanya haraka tunaweza kufanikiwa kuokoa maisha yake"alisema kwa Papara kubwa David ila kabla aliyeagizwa hajageuka kufuata hilo begi,,macho yao yalishuhudia Emmanuel akiwa kimya huku macho kayatumbua,,ulimi ameung'ata. Hakuna aliyetaka kuamini kama mwenzao hayupo tena. Wingu kubwa la huzuni lilitanda kwenye anga la mioyo yao,, mvua ya machozi ilianza kunyesha kutoka kwenye macho yao. Sauti za radi za vilio zilisikika kutoka ndani ya vinywa vyao kiufupi hakuwepo ambaye alisalia na nguvu kuzuia yote hayo. Wanaume ,wanawake wote macho yalikuwa mekundu dah.

Steven hakuamini macho yake kama ni kweli rafiki yake hayupo ,,leso yake ilikuwa ikipita kwenye uso wake kujaribu kufuta machozi ila kufuta machozi pasipo kukifuta kilio ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu. Machozi yaliendelea kutengeneza mito usoni pake. Alitoa leso yake na kuyaelekeza mahali ulipo mwili wa Emmanuel.

Alishituka na kuhisi labda amesahau
"Mmmh mwili si ulikuwa pale asee"alisema kwa sauti kubwa hata wenzake walisikia na kuelekeza macho yao mahali pale. Nao waliungana naye katika mshangao kwani mwili wa Emmanuel haukuwepo pale,,yalibaki mapovu na nguo alizokuwa amevaa.

"My Gooood,,, jamaani mwenzenu nishaishiwa nguvu mwenzenu,,sina hamu tena mimi. Ndio mambo gani sasa haya??? Ndio maana hii kazi tuliipinga ila Jay tu ndo kalazimisha na bado utasikia tuendelee na kazi"alilalamika mwanadada Queen. Ilisikika sauti kutoka ndani ya hema.
"Kazi iendelee,,kazi iendelee" Alikuwa Jay aliyekuwa ndani ya hema muda wote huo. Kwa sasa alikuwa anatoka ,, mkononi alikuwa na mikate pamoja na juisi.
"Jamani msisahau leo ndio tunaanza kazi kazi hivyo basi tule haraka tuanze kazi mara moja" alisema Jay akiwaacha wenzake na mshangao mkubwa sana kwamba je hajui kama mwenzao amefariki,, alafu hajagusia chochote kuhusu hilo wala hata chembe ya huzuni haikuonekana usoni pake. Jay alimshangaza kila mmoja.

"Jay tunaanzaje kula hata kuanza kufanya kazi hiyo wakati tumempoteza mwenzetu ??"
"Mwenzetu yupi??"aliuliza kwa mshangao mkubwa Jay
"Emmanuel amefariki"
"Oooh mwili wake uko wapi!?"aliuliza
"Mwili ulikuwepo hapo"alijibu Steven na kunyoosha kidole kuelekea mahali ambapo ulikuwepo mwili wa Emmanuel,,kwa sasa hata nguo hazikuwepo.mshituko tena

"Unajua hebu acheni utoto,,kama kafariki mwili uko wapi??? Potezea, njooni tuendelee kula tukafanye kazi"alisema Jay ila nguvu ya kula ingetoka wapi kwa hawa wengine??

**************

Ni majira ya saa tano za asubuhi ,vijana wote kumi na nne wapo katika kutembea taratibu kuanza uchunguzi,, umakini ulikuwa mkubwa japo kiuhalisia akili hazikuwepo pale,,kila mmoja alikuwa anawaza ni jambo gani litatokea tena na litamuhusu nani. Muda wote huo Steven naye alikuwa mbali kimawazo akiwaza ni nini ambacho Emmanuel aliona kinamtokea Mariam usiku ule kutoka kwa hicho kiumbe chenye kutisha,,na kwanini alipotaka kusema kuhusu Mariam yakatokea yale hata kupoteza maisha.
Steven aligundua kuna jambo lenye hatari kubwa sana linawaandama.
"Hivi haya ndio maajabu yaliyoandikwa kwenye kile kitabu kweli??,, mbona kama kuna vitu havipo sawa,,,"alisema huku akihamisha mawazo yake kwa Jay ambaye kwa akili ya kikubwa na kichunguzi hakuelewa kabisa mambo ya Jay.
Kwanini usiku huo asikie mambo ya ajabu nje na sauti za kuita majina yao na alipotoka amkute Jay eti anapunga upepo. Na ni usiku huohuo ambao Emmanuel naye aliona hayo tena yakimuhusu Mariam,, kwanini Mariam??? Na nini hasa kilitokea kwa Mariam?? Haya maswali yalimtoa Steven ndani ya msitu na kumuingiza ndani ya chumba cha mtihani wenye maswali magumu yenye kumshinda hata mtungaji wa maswali hayo.mara kadhaa alijigonga kwenye miti

Akiwa anaendelea kujiuliza maswali mengi ghafla Jay alisimama na kuwaambia kwamba ana wazo.
Japo lilikuwa wazo kama alivyosema ila wenzake waliamini ndio itakuwa kama atakavyo kwani huwa anafosi mambo .
Jay alitoa wazo lake ambalo lilimuacha mdomo wazi kila mmoja
"Aaah hapana kwakweli,,hilo haliwezekani"alisema David na kila mmoja alipingana na wazo hilo

Ni wazo gani hilo??
Maswali ni mengi sana ya kujiuliza,, endelea kufuatilia.

ITAENDELEA...

BAKI HAPA HAPA KWENYE APP YETU, MUITE NA MWINGINE.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: BINAMU 🔞 SEHEMU YA 11

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 1-5

CHOMBEZO: MASSAGE ROOM🔞 SEHEMU YA 21