RAFIKI SEHEMU YA 7
SIMULIZI : RAFIKI
MTUNZI : MADAM YUSTAR
SEHEMU YA SABA
Tuendeleee...
Nilishanga sana kitendo cha mimi na Viviani kuitwa , wakati nilitambua kabsa mwenye makosa ni mimi peke angu.
Viviani aliweza kuniambia niwe na ujasiri kwani hii kesi ni ngumu pia inaweza kuwa rahisi kama nikimwamini Muumba wangu.
Mda tulipewa wa kwenda kwenye ofsi ya nidhamu uliwadia, nilienda kwenye ofsi ya nidhamu nikiwa pamoja na Vivani.
Tulivyofika kila mmoja alitoa heshima kea viongozi wetu , walianza kutuangalia kwa zamu kama vile walikuwa wakitujadili kwa macho.
Baada ya kimya cha dakika tano mmoja wao aliweza kuongea.
"Binti mcheza video za kikorea pamoja na msambazaji wake" wote walikuwepo pale walicheka.
"Fetty.. Tumekuita hapa uweze kutuelezea sababu za wewe kuamua kutuchafulia chuo chetu? Ulishindwa kuficha makucha yako hadi yameekwa hadharani? Mbona watoto wa sikuizo hamuuogopi laana? Ulivyo hata hifananii na ulichokifanya, hufananii kabsa mdogo wangu"
"Ukw..ee..eeli" niliongea kwa sauti ya kukata kata iliweza kusindikizwa na machozi yangu.
"Acha kulia lia hapa sio msibani useme umefiwa, makosa umeyafanya wewe mwenyewe ukiwa na akili zako timamu hatutaki unafiki hapa. Kwanza hili swala tulishalijadili na mwisho kabsa kamati iliamua kuwa wewe na huyo Vivani mrudishe kila kitu ambacho kinahisiana na hiki chuo. Kuanzia leo nyie hamtambuliki kama wanafunzi wa chuo hiki.."
"Mimi nina kosa gani hadi nifikuzwe chuo? Kosa langu ni lipi?!" Viviani aliuliza kwa jaziba.
"Kwamba unataka kusema huelewi chochote kinachoendelea? Ok.! Kosa lako ni kusambaza video chafu za mwanafunzi mwenzio, ni kosa kisheria kufanya upuuzi kama ulioufanya wewe maana unaweza hata kufungwa kama mwenzio akienda mahakamani"
"Viviani.! Ni wewe, wewe ndo uliweza kusambaza hizi video alafu siku zote upo na mimi kunichora. Nilizani nimepata rafiki kumbe na wewe ni wale wale"
"Fetty sio kweli mimi sijaweza kufanya uchafu kama huo, sio kweli Fetty.. Mna ushahidi gani kama kweli mimi ndo nimesambaza hizi picha? Nipeni ushahidi"
Walichukua laptop na kuweza kuieka mbele yangu, zilionyeshwa meseji za Viviani akiwa annipondea kwa marafiki zake kuwa lazima atanizalilisha sana. Tunaonyeshwa na tarehe ambayo Vivani aliisambaza hiyo video kwenye magroup matatu.
Sikuamini kile nilichokiona nilihisi huwenda nipo kwenye ndoto, Viviani mtu pekee niliyeamini amekuja kunipa faraja huyo huyo ndo nyoka wangu wa kwanza. Nilitoka pale ofsini hatabsikuhitaji kusikia chochote kutoka kwa viongozi hao wa shule.
Nilienda moja kwa moja hadi kwangu, kutokana na hasira nilizokuwa nazo niliweza kulia hadi pale nilipoweza kupitiwa na usingizi.
Siku iliyofata niliamka na kuanza kutafakari maisha yangu yatakuaje baada ya hapa? Nitawaeleza nini wazazi wangu ambao wananitegemea? Nitawaeleza nini ndugu zangu? Ulikuwa ni mtihani mkubwa sana katika maisha yangu.
Niliangalia akiba yangu , nilikuwa na kiasi cha Tsh laki moja tu. Niliwaza kodi bado miezi miwili iishe, bado sijala, maji , umeme na mahitaji yangu mengine ya muhimu.
Nilianza kuamini kwamba rafiki sio mtu wa kumwamini kabsa, akili yangu ilichok saana. Wakati naendelea kuwaza Viviani aliingia ndani akiwa amevimba usoni, hii ilionyesha kwamba usku kucha alikuwa anakesha akilia tu...
Ni kweli Viviani ndo msambazaji wa video? Mimi na wewe hatujui, hebu tuendelee kufatilia mkasa huu mwanzo hadi mwisho tujue hatima ya maisha ya hawa wanafunzi walioweza kufukuzwa shule!...
ITAENDELEA.....
BAKI HAPA HAPA KWENYE APP YETU, MUITE NA MWINGINE.
Maoni
Chapisha Maoni