SAA ZA MWISHO EPISODE 2

SAA ZA MWISHO ****Ep2*** S.P.Owino Mda ulizidi kusogea tititi! Mshale wa saa ya ukutani ulisogea, mama Kaka na dada Helena walipewa sehem wapumzike usikuule! Bila kufaham kilicho tokea kwa mgonjwa wao! Ilitimia saa 7:00 usiku Vipimo vikiwa vina onyesha kwamba tayari nilisha fariki, nilistuka moyo ukiwa kasi kweli nilihisi kizunguzungu na kichefuchefu mpaka nikatapika taa zilikua zime Zima hospitali nzima kimya. Nilijaribu kukohoa sauti ilikua kubwa Sana kwani nilikua mwenyewe nilie toa sauti. Niliogopa kidogo kwani kulikua na giza niliamka nikapapase ukuta ili nitafute switch niwashe taa, niligusa bila mafanikio ghafla taa iliwaka ndipo nilipo iona ile sura ya nesi Alie kua na mavazi ya kutisha nilitaka kupiga yowe ohooo! Kumbe siwezi kuongea tena ulimi wangu ulikua mzito. Alinisogelea aka niambia wewe niwakwetu na tumekupa siku tano ili ukubali kujitoa kwetu kwa ihari yako na hauta kiona kifo" una siku tano za kua hai ndani ya hospital hii Yani masaa 124, aliupanua mdomo wake a...