JOANA ANAONA KITU USIKU SEHEMU YA 2



JOANA ANAONA KITU USIKU

02

MTUNZI: STEVE MOLLEL

Mwanafunzi aliyefariki alijulikana kwa jina la Judith Onenke, mwanafunzi kutoka Nigeria. Miongoni mwa wanafunzi wacheshi na wenye uwezo mkubwa darasani.

Masomo yakaihirishwa na taarifa ikatolewa polisi waliokuja mara moja kupeleleza tukio.

Walipekua na kuchambua mazingira ya chumba yalipotokea mauaji. Wakamuuliza pia na maswali kadhaa meti wake marehemu Judith, aitwaye Lilian Smith. Ambaye kwa muda wote huo alikuwa anatetemeka kwa hofu na bumbuwazi.

Aliona kama tamthilia ya kuigiza inatukia mbele ya macho yake, ila tamthilia asiyoipenda, inayotisha, na rimoti imejamu asiweze kubadili.

"Wakati mwenzako anapiga kelele usiku, wewe ulikuwa wapi?" Aliuliza askari. Alikuwa mwanaume mnene mrefu. Mweupe sana.

Pua yake ilikuwa nyekundu. Mustachi dhaifu na lips nyembamba. Macho yake yalikuwa madogo ila makali. Alijitambulisha kwa jina la inspekta Bronel Westgate.

"Mimi sikusikia lolote," akajibu Lilian akitikisa kichwa. Macho yake yalikuwa mekundu, uso wake ukipwaya.

"Ni ajabu. Mimi sikusikia kitu mpaka pale asubuhi nilipoamka na kumkuta Judith akiwa amelowana damu."

Jambo hilo likawashangaza polisi. Walifanya upekuzi chumbani lakini hawakuona kiashiria chochote cha uvamizi. Mlango ulikuwa umefungwa kama kawaida.

Kila kitu kilikuwa kimekaa kwenye mazingira yake. Ni shuka tu la kitanda ndilo lilikuwa limetimka.

Polisi wakaondoka na Lilian kwenda naye kituoni kwa maelezo zaidi. Alichukuliwa pia na kiongozi wa usalama bwenini akatoa pia maelezo.

Kutokana na hofu iliyokuwa imetanda kwa wanafunzi kwasababu ya mauaji kadhaa sasa, chuo kikaazimia kufungwa watu warudi makwao.

Ilitolewa notisi wanafunzi wakipewa juma moja tu la kujiandaa na kuondoka. Baada ya hapo asionekane yeyote ndani ya eneo la chuo.

Wanafunzi wakaanza kujiandaa. Na hata wale wa karibu wakajiondokea mapema zaidi.

Joana alibakia na meti wake wa chumba, Lisa Moan, ambaye yeye alipanga kurudi nyumbani baada ya siku nne.

Walikuwepo pia wanafunzi wengine waliokuwa wanajivuta kurejea makwao. Huwa hawakosekani watu hawa wa tarehe za mwisho. Ila walikuwa na sababu mbalimbali.

Wanafunzi wakapewa msisitizo wa kutotembea na kuzura huko nje nyakati za usiku. Lakini pia wawe wanafunga milango ya vyumba vyao kwa usalama.
Zikapita siku tatu tangu Judith Onenke afariki.

Siku ya nne, ikiwa ni usiku, wanafunzi fulani wawili wa chuo walikuwa wapo nje majira ya usiku wa saa nne.

Wanafunzi hawa walikuwa wapenzi. Walikuwa wameketi mahala palipokuwa tulivu na miti mingi. Walikuwa hapa kutafuta faragha na kubadili mazingira.
Mwanamke alikuwa amevalia sketi fupi mno ya jeans na topu ndogo ya pinki. Mwanaume alikuwa amevalia suruali chakavu ya jeans pia, na tisheti yenye maandishi mekundu:

"WE GONNA DINE IN HELL!"

Walikuwa wamekaa mikao ya kimahaba wakipeana mabusu na kunyonyana ndimi. Mazingira yaliwashawishi.

Walijihisi wapo peke yao hivyo basi wanaweza wakafanya lolote lile kujifurahisha.

Walienda mbele zaidi wakaanza kuvuana nguo, mwanamke akiwa mhanga wa kwanza. Alivuliwa topu akabaki kifua wazi.

Mwanaume akalala chini wakaendelea na zoezi la kuvuana nguo. Mwanamke akavua sasa hata sketi yake na kubaki na nguo ya ndani.

Mwanamke naye akaanza zoezi la kumvua mwanaume suruali. Hakuimaliza, mara wakasikia vishindo vya miguu.
Walishtuka wakaangaza.
"Watakuwa wanyama," akasema mwanaume.

Uchu ulikuwa umemvaa na basi hakujali. Wakaendelea kufanya mambo yao, msichana akimvua suruali mwanaume kwa madaha, kwa mahaba.

Si bahati, suruali hiyo haikumalizika tena. Wakasikia sauti ya vishindo vya miguu! Walishtuka!

Huyu hakuwa sasa mnyana kama mwanzoni walivyofarijiana. Huyu alikuwa binadamu! Tena aliyesimama kandokando yao akibebelea kisu mkono wake wa kuume.

Mwanamke aliyevalia gauni jeupe la kulalia. Nywele zake ndefu na giza zikimkinga uso.

Wapenzi hawa wakashtuka haswa! Ni wazi walikumbuka hadithi za mauaji yanayotukia hapo chuoni. Ni wazi walikumbuka mauaji hayo yanafanywa na nani - mtu mwenye kisu.

Hivyo ndiyo huyu?

Walikurupuka wakakimbia haswa. Mtu yule mwenye kisu hakuwakimbiza, alisimama akiwatazama, akikunja shingo kushoto, na kisha kulia.

Kulipokucha, kwenye majira ya saa tano asubuhi, polisi kadhaa wakafika msituni hapo. Tayari taarifa ilitolewa ya kuonekana maiti mbili: mwanamke na mwanaume.

Ni wale wapenzi waliokuwa hapo usiku. Wote waliuawa kwa kisu vifuani, kila mmoja na mahala pake. Wote wakiwa na nguo za ndani pekee.

Inspekta Bronel Westgate akafanya upekuzi na upelelezi wake. Mauaji yalikuwa ya aina ile ile. Na muuaji akisadikika kuwa mmoja.

Nani huyu?

Wanafunzi waliamriwa kuondoka siku hiyo hiyo warudi zao makwao. Hakuna tena kubaki chuoni. Wakatii amri.

Kesho yake inspekta Bronel akiwa kituoni, anapembua na kupitia data alizozikusanya kuhusu kesi yake kwa umakini zaidi. Kuna jambo akagundua.
Kulikuwa kuna nyayo za aina mbili udongoni. Maana yake za watu wawili tofauti waliokuwa wamekanyaga chini pasipo viatu.

Nyayo ya kwanza itakuwa ya marehemu yule mwanamke, yeye maiti yake ilikutwa akiwa peku. Je, ya pili hii itakuwa ya nani ingali mwanaume marehemu alikutwa na viatu miguuni?
Inspekta akagundua itakuwa ndiyo ya muuaji, ama tuseme mtuhumiwa wa kwanza wa mauaji. Na muuaji huyu alikuwa ni mwanamke.

Nyayo zilikuwa za mguu wa kike.
Akakata shauri kwenda tena eneo la tukio. Eneo hilo lote lilikuwa limezungushiwa utepe wa njano wa kukataza mtu kupita hapo ili kutoharibu mazingira ya upelelezi.

Akazama ndani na kuanza kufuatilia akitumia kifaa cha kioo mkuzo. Alitazama vema nyayo za miguu. 
Mwishowe akagundua nyayo ile aliyoitilia shaka zilionekana mara tatu tu. Mara ya kwanza mtu huyo alisimama, mara ya pili alionekana akiwa karibu na mwanaume, tena eneo ilipokutwa maiti.

Mara ya tatu na mwisho, nyayo hizo zikaonekana zikiwa karibu na nyayo zingine, yani za yule mwanamke marehemu ambaye alionekana alikimbia kabla ya kumalizwa.

Inspekta akashangazwa. Mtuhumiwa huyo alikuwa anatembeaje nyayo zake zionekane kwa mafungu!?
Anapaa? Anaruka? 

Alipima urefu wa nyayo hizo, pamoja pia na kina chake. Hakuona kama mwanamke huyo anapaa, kwani kina cha nyayo zake kilikuwa cha kawaida.
Akarudi kazini akiendelea kutafakari. Lakini akiazimia punde wanafunzi watakaporudi chuo, atafanya jitihada kujua mguu ule ni wa nani.

Zaidi, ataendelea kufuatilia kwa walinzi wa chuo. Alikuwa na matumaini atapata kitu muda si mrefu sana.

Siku moja Joana akiwa huko kwao, Ubelgiji, ndani ya jiji la Brussels, majira ya usiku wa saa nane, alikurupuka toka usingizini.

Alijihisi joto akataka kuoga apate ahueni. 

Yalikuwa ni majira ya joto muda huko Ulaya. Joana hupata shida sana majira haya ukizingatia hawezi tumia viyoyozi sababu ya pumu.

Akaenda bafuni kwenye shawa, bomba la mvua, apate kuoga. 

Wakati anaoga akagundua maji yaliyomiminikia chini yana na damu. Akashtuka sana. 

Damu imetokea wapi?

Akajikagua mwili mzima lakini hakupata kitu. Akazidi kupata hofu. Hakujua kama alitoka kufanya mauaji kabla hajaamka.

Alienda kumuua jirani yake akaaye peke yake nyumba ya pembezoni, kama nusu kilometa toka kwao.

Jirani huyu alikuwa ni mwanamama mjane. Tena asiye hata na watoto.
Na pasipo kujua, damu ya mtu huyo aliyemuua ndiyo hiyo iliyokuwa inamiminika. Ilikuwa imemganda kwenye viwiko vya mikono.

Akiwa anajiuliza, akafunga bomba na kutoka bafuni. Akaelekea chumbani na kuketi akijiuliza.

Aliunganisha tukio hilo na lile lililotokea chuoni. Akapata mashaka sana. Akaona kuna haja ya kwenda hospitali kesho akaonane na daktari.

Kabla hajalala, akatazama dressing table apate bangili yake aliyoivua alipoenda kuoga.

Hakuiona.

Akajiuliza imeenda wapi na ilhali aliacha pale? Akatafuta chumba kizima lakini hakuiona kabisa. Alistaajabu. 
Alichoka kutafuta akaamua kujilalia. Asubuhi alipoamka, akaikuta bangili hiyo mkononi!

Alishangaa. Ila hakuwa na muda wa kujiuliza maswali mlango wake ukagongwa. Alikuwa ni mama yake.
Mwanamke mnene wa umri wa miaka hamsini mwenye nywele za goldi. Macho yake yalikuwa ya bluu kama ya paka. Alivalia suti ya pinki.

Akamtaarifu mwanaye juu ya msiba wa jirani. 

"Ameuawa jana usiku kwa kisu!"



ITAENDELEA........



TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: BINAMU 🔞 SEHEMU YA 11

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 1-5

CHOMBEZO: MASSAGE ROOM🔞 SEHEMU YA 21