NILIZAA NA KUOLEWA NA SHEMEJI KUMKOMOA MME WANGU PART: 02



NILIZAA NA KUOLEWA NA SHEMEJI KUMKOMOA MME WANGU



PART: 02.

Ilipoishia, Baada ya kumpigia, nilimueleza mwanzo mpaka mwisho ndipo aliponijibu,

"Pole sana kwa hilo! mda huu nipo kazini lakini nimeamua kuacha kazi ili nikakusaidie"

"Asante sana shemeji" nilimshukuru sana huku nikiomba afike mapema maana nilikuwa nimebanwa na haja kubwa.

Baada ya mda kidogo, niliamua kuchungulia kama wameshaondoka lakini walikuwa bado wamenisubiria. Niliendelea kufunga  mlango huku nikisubiri msaada kutoka kwa shemeji yangu Julius.

SONGA NAYO...

Niliendelea kumsubiri shemeji mpaka mda ukawa unaenda sasa ndipo nilipomoigia simu kwa mara nyingine tena.
Wakati nampigia simu, kumbe alikuwa karibu na mlango ndipo aliponiambia nifungue mlango.
Nilijifunga kidedea kisha nikafungua mlango ndipo vurugu kali ilipoanza ambayo ilifanya kivumbi kikali kutimuka.

"Mnafanya nini hapa! hamna kazi za kufanya! ngoja niwaoneshe kazi sasa" Shemu Julius akiwa na fimbo ya kunesanesa aliwambia wadogo zake.

"Sikia kaka..yaani anamtukana mama halafu unataka kumtetea! alaa! " walimjibu .

"Ondoka...! ondoka" Shemu alianza kuwachapa fimbo za migongoni huku wakiwa wanatimua mbio kuelekea nyumbani.

"Mamaaa!  mama!.. " walipiga kelele huku wakiendelea kupata fimbo za mgongoni.

Ama kweli sikuamini kama shemeji yangu angeweza kunisaidia kiasi hicho kwani bila kufanya hivo sijui ingekuwaje.

Mda si mrefu Shemu alirudi nyumbani kwangu huku akiwa anahema kisha nikaanza kumsimulia  mwanzo mwisho jambo ambalo lilimfanya aweze kunionea huruma huku akinihakikishia ulinzi na amani kwa namna yoyote ile.

Tukiwa ndani , gaflq mama mkwe akiwa na mawifi wangu alikuja akiwa amejifunga kanga kisha akasimama kwenye kiwanja changu ndipo alipoanza kuongea,

"Julius...! Julius." Naam mama.

"Wewe mtoto umerogwa au!"

"Kwani mama nimefanya nini?"

"Unafikia hatua ya kugombana na wadogo zako ambao wananitetea ...huyu ni mke wako! subiri sasa"

"Mama kwanini mnamnyanyasa?, kama  kuna shida  ni bora mkae chini myamalize ila sio kumfanyia hivo"

"Hee! nikae na huyu mbwa ili iweje! sasa kama utabaki na maneno yako hayo tafuta pakulala! sitaki mtu mjinga nyumbani mwangu" 

"Sasa nina kosa gani? nimewachapa maana nimewakuta mlangoni mwake huku wakiwa wamemsubiri kumuumiza jambo ambalo ni hatari sana"

Baada ya majibizano hayo, mama mkwe alimpigia simu mme wangu ambaye baada ya mda kidogo aliweza kunipigia simu huku akionekana kuwa na hasira kwelikweli.

"We mwanamke! bado hutaki kusikia, sasa nasema sitaki nikukute ndani laa sivyo utakuwa unanitafutia kifungo cha maisha. Nimekuvumilia kwa mda wa miaka 6 sasa bila mtoto lakini unaanza kuleta kiburi mpaka unagombana na mama! yaani....yaani...tena nakuja mda si mrefu"
Aliniambia maneno makali mpaka nikawa naogopa ndipo kwa sauti ya uoga nilipomwambia

"Samahani sana mme wangu, nakupenda sana lakini suala la kumpiga mama mkwe ni uongo mtupu ambao wanauzusha. Sijagombana naye wala kupigana naye usipokuwa tu ni maneno ambayo wananibambikiza na kisa ni kukosa mtoto" nilimjibu

"Sasa kama huwezi kubeba  mimba si bora uondoke! nikija naoa mke mwingine wala sikutaki nyumbani kwangu."

"Jamani mme wangu mbona umenivumilia kwa miaka sita bila kunifukuza?, nitaenda wapi sasa maana nimeshapoteza ushichana wangu na kwenye jamii sijui watanichukuliaje"

"Nimeshakwambia fanya ufanyalo kuondoka ni lazima" 
Alinijibu kisha akakata simu.

Baada ya hapo, nilitupa simu chini kwa maumivu makali sana ndipo Shemu alipoikota kisha akaninyanyua taratibu mpaka  ndani ya nyumba.
Ama kweli nilianza kuwaza nini nifanye kwani  mme wangu ameshanisaliti tayari huku mama mkwe na mawifi wakiwa hawataki hata kuniona usoni mwao.

Baada ya mda kidogo, nilipata ahueni kidigo huku nikianza kupanga mipango ya wapi nielekee.
Mnamo mida ya saa 2 usiku, nilisikia mlango wa unagongwa ndipo nilipostuka kisha nikasema,

"We nani?" nilimuuliza

"Ni mimi shemeji yako Julius" alijibu.

"Ohh kumbe ni wewe,  karibu shemu"

Nilinyanyuka kisha nikafungua mlango  naye akaigia ndani.
Kwakuwa ulikuwa mda wa chakula, nilimtengea chakula kisha tukaanza kula kwani nilikuwa nimeandaa chakutosha.

Baada ya kumaliza kula tulianza kuogea mawili matatu kisha nikaenda kuoga ili badaye niweze kujipumzisha. Nikiwa nimejifunga kanga ambayo ilikuwa imelowana kwa mbali, shemu aliniita kisha akaniambia,

"Shemu asante kwa  chakula ila kuna kitu nataka nikwambie hapa" 

"Sawa shemu ngoja nivae nakuja" niliingia chumbani kisha niavaa gauni langu huku nikiwa nawaza nini anataka kuniambia.

Baada ya kumaliza nilimfata shemu kisha nikamwambia 

"Niambie shemu"

"Sasa naomba kitu kimoja kwa leo sijui kama itawezekana lakini.."

"Kitu gani hicho?" nilimuuliza huku nikiwa na shauku kubwa.

"Ni kwamba katika mchakato mzima wa kukutetea, mambo yamezidi kuwa makubwa hasa baada ya mama na wadogo zangu kunichongea kwa mzee ambaye amenifukuza kwenye nyumba. Sasa naomva kwa leo nilale kwako huku nikiwa najipanga kutafuta chumba cha kupanga" aliniambia.

"Pole sana shemu ..sehemu ya kulala ipo lakini sasa kaka yako sijui kama umempa taarifa.."..

"Taarifa sijampa wala nyumbani hakuna anayejua na sitaki wajue kama nipo huku"

"Ohh sawa sasa si watakuona"?

"Hapana nitaamka asubuhi na mapema sana"

"Ohh sawa haina shida ila mama mkwe mhhh..."

Baada ya kumjibu hivo,nilianza kuwaza wapi nitamlaza? maana sikuwa na godoro la ziada kwa ajili ya wageni . Nilitamani kumtandikia mkeka kwenye sakafu lakini niliona aibu ndipo nilipoanda chumbani nikatandika kitanda vizuri ili shemeji alale kitandani nami nilale kwenye mkeka.

Baada ya kumaliza kutandika, nilimuita shemu,

"Shemu.."

"Naamu.."

"Njoo ulale .."

"Sawa nakuja"

Baada ya kufika chumbani, nilimkaribisha kisha nikamwambia naenda kulala sebuleni jambo ambalo shemu hakulipenda kabisa,

"Shemu sitaki niwe shida kwako, (please) naomba uje ulale kitandani  nami  nitalala sebuleni" 

"Mhh shemu wewe lala tu  wala usihofu kitu  chochote kwangu"

"Hapana siwezi kulala kitandani afu wewe ukalala sebuleni"

"Mhh.."

Nilibaki nimesimama huku nikiwa sijui wapi nichague kati ya kitandani au sebuleni..

ITAENDELEA.....



TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: BINAMU 🔞 SEHEMU YA 11

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 1-5

CHOMBEZO: MASSAGE ROOM🔞 SEHEMU YA 21