ZOMBI WA DAR EPISODE 2
ZOMBI WA DAR
ABELUKA FILM
EPISODE YA 02
TULIISHIA...
"Mamaaaaaa...." Some alikuwa ni kijana wa mjini sana alipiga kelele baada ya kuona sura ya yule mtu imeanza kuoza na meno yake yakiwa na damu mingi. Ghafla jamaa akafumbua macho yake mekunduuuu yaliyo onyesha njaa kali, some akainuka haraka na kutaka kukimbia anavutwa na kurudishwa pale chini.
"Aaaaaaaaaa.... "
ENDELEA...
"aaaaaa...Hapana usiniuwe..." Same alipiga kelele alipoona yule zombi anapeleka mdomo kwenye bega lake Tena akiwa amepanua mdomo wote.
""Ahaaaaaaaaa..." Same aliendelea kupiga kelele lakini yule zombi akaacha haraka na kusimama juu .
Same alisimama kwa kasi na kukimbia kuelekea kwenye gari yake simu yake aliacha palepale chini hakuwa na mda nayo.
"Hivi kweli nilitaka nimle mtu haiwezekani kwa hiyo mimi zombi?.." aliongea moyoni yule Zombi akiwa anamtazama same kwa mbali akitimua gari yake kwa Kasi Sana.
"Alinigonga na gari lakini sijafa Wala sijasikia maumivu yoyote inamaana viungo vyangu tayari vimekufa Mimi Ni maiti haiwezekani!, nilikufaje kufaje mpaka niwe zombi haya maisha siyawezi mimi..."
Yule zombi aliongea kimoyomoyo kwa hasira baada ya kujigundua yeye ni zombi. kwa masikio ya kawaida alikuwa anatoa muungurumo tu.
Same alikimbiza sana gari akiwa katikati ya msitu mala gari ikazima.
" Waka basiiiiiiii..." Aliongea kwa hasira akiwa anajaribu kuwasha lakini haikuwaka.
"Niende Nikafungue mbele niangalie tatizo kwenye engeen?.." alijiuliza Same akiwa ndani ya gari kabana madirisha yote.
"Aaaa wewe sitoki tena nje ya gari Mimi.." alijijibu na kuegamia kwenye usukani wa gari.
mda huo redio ya gari lake ilikuwa inapiga nyimbo ya harmonize akapeleka mkono mpaka kwenye kitufe Cha kubadilishia nyimbo nakuplay nyimbo ya dini kwa mbali akiwa anafuatiza maneno ya ile nyimbo aliyoplay.
Akiwa haelewi nini afanye maana simu alidondosha kule nyuma alipoona zombi, mala Anaanza kusikia muungurumo was mtu nje ya gari.
"We Mungu weka mkono wako kwenye maisha yangu leo..." aliongea taratibu akiwa anageuza kichwa kutazama dirishani kitu kinachounguruma.
Alupotazama dirisha la kushoto ilipotoka sauti hakuona chochote na ule muungurumo haukusikika Tena.
"Asante Mungu hili ni wenge tu sio kweli.." aliegama kwenye usukani na kuanza kufanya maombi.
Akiwa anaendelea na maombi mala mlango wa gari unaanza kugongwa (ngo,,,,,, ngo ,,,,,ngo,,,)
Aliacha kusali akatulia kimya Kama hakuna mtu ndani ya gari.mlango ukagongwa kwa mala nyingine (ngo....ngo.....ngo.) na sauti ya muungurumo ikiwa inasikika mlangoni.
"Mwenyezi Mungu nimeweka maisha yangu mikononi mwako mi nafungua.." aliongea taratibu Sana akiwa akiwa anaogopa ( ngo...ngo ..ngo...)mlango uligonga tena
"Sawa nafungua...." Some alisogea kidogo na kufungua mlango wa gari kijasho chembamba kikimtoka.
Baada ya kufungua alimuona zombi akiwa ameshika simu yake. Zombi aliunguruma na kumnyoshea Some simu.
Some akatulia Kama sekunde tano bila kuichukua alafu akaivuta kwa nguvu na kubana mlango wa gari. Moja kwa moja Alienda kwenye namba na kupiga lakini mtandao haukushika mda huo.
"Mtandao huu vipi aaah..."alitupa simu kwa hasira
Mwisho alitazama Tena dirishani alimuona zombi akiwa ameegesha kichwa upande mmoja anamtazama kwa huruma sana.
"Huyu mchawi vipi mbona ananingaria kwa huruma mpaka saizi hajanizuru!.."alifikilia akiwa anaangaliana na zombi.
"Jamaa inamaana haelewi Kama nahitaji msaada wake.." zombi alikuwa anafikilia kimoyo moyo aliendelea kutazama ndani ya gari kwa huruma taratibu ananyoosha mikono juu na kubananisha viganja vya mikono yake kuonyesha kuomba msaada. .
"Huyu mchawi anaonekana kuomba msaada kwangu ety lakini sielewi anataka Nini?..." Some kidogo kidogo pressure ikahuka akajikuta Anaanza kumzoea zombi.
"We jamaa unaomba msaada gani?.." aliuliza kwa kujiamini Sana akiwa ndani ya gari.
Zombi hakuweza kutoa jibu kwa mdomo, alitumia vitendo alienda moja kwa moja kusimama mlango wa nyuma wa gari akionesha kutaka kuingia.
"Sawa nitakusaidia lakini niahidi
kitu kimoja. Sitaki uungurume ndani ya gari yangu..." Aliongea same na kufungua mlango wa nyuma, zombi ikavuta mlango taratibu na kuingia ndani ya gari.
"Oya bro ngoja nitengeneze gari kwanza.." aliongea same mala hii akashuka bill woga na kwenda kufungua mbele ya gari. Baada ya sekunde chache aliweka vitu sawa na kurudi ndani ya gari, hatimaye gari iliwaka
"Nikupeleke wapi Kaka? ukionekana mjini hivo watakuuwa." Aliuliza same kabla hajaondoa gari. Zombi hakuongea chochote alikaa kimya tu.
"Ok minajua unamatatizo ila ngoja nikusaidie tu..." aliongea same akaplay nyimbo ya harmonize iliyokuwa mwanzo kabla ya shida na kuendelea na safari.
ASUBUHI.
Majira ya moja asubuhi Some anafika nyumbani kwake.
Ni maeneo ya Ubungo tena alikuwa anaishi pekeyake nyumba moja kubwa.
Alishuka kwenye gari na kwenda kufungua geti la kuingizia gari ndani.
Zombi akawa anataka kushuka na yeye.
"We jamaaa usitoke kwanza..."aliongea same akafungua geti haraka na kurudi kwenye gari.
"Inatakiwa uwe makini bro ukionekana huku wanakuuwa sawa.." alionge same akiwa aningiza gari ndani.
Baada ya kuingiza gari alirudi kufunga geti na kumtoa zombi ndani ya gari
" ayaa twende ndani mimi naishi pekeyangu usiogope bwana zombi..." aliongea akiwa ameshatangulia kufungua mlango.
"Bro changamka Basi uingie ndani mwendo gani huo utafika kweli!.."
Zuma anajitahidi kuongeza mwendo lakini alikuwa bado slow Sana.
Zombi aliingia ndani akiwa amechafuka damu na sura yake imeanza kuozaoza.
"Bro mbona uhongei unaweza kuniambia jina lako?.." aliuliza same akiwa anafungua mapazia pale sebureni ili mwanga uingie. Zombo alikuwa anasikia lakini hakuweza kujibu chochote
"Basi bro inaonekana mtu mwema sana licha ya kuwa unatisha kuanzia leo nitajikita zombi, Ila haitakiwi mtu yoyote ajue kama naishi na wewe hapa...."
"Huyu jamaa ni mtu mzuri lakini nitaweza kujicontor nisimle kweli maisha yangu yanategemea nyama.." alikuwa anafikiria zombi akiwa bado amesimama anamtazama sam akiwa anafungua mapazia.
"Zombi Kaa hapo kwenye kiti ngoja nikaanda chochote kitu maana njaa inauma kishenzi.." Some aliondoka pale sebureni na kumuacha zombi peke yake.
Mda huo enjoy mpenzi wake na same anafika nyumbani kwa same akiwa na gari yake nyeupe.
Hakuingia na gari ndani ya fence alishuka na kupita mlango mdogo kwa kunyata taratibu kabisa akiwa na zawadi ya mauwa mkononi ili amsuprise mpenzi wake.
Alifika mlangoni na kufungua mlango kwa nguvu
"Supriseeeee...." Aliongea akijua same yupo mbele yake lakini baada ya kuona kitu kilichopo mbele yake akatulia haraka.
_______itaendelea________
ngoja niwape baadhi ya uhondo utakao tokea mbele ya hii simulizi.
Maisha ya Zombi humo ndani ni vituko kila siku,,,,
Ni kwamba enjoy atatokea kumpenda Zombi wa dar.. mmmmmmh 🔥 ilikuwaje kuwaje mpaka ampende?????
Vipi same atachukua hatua gani??? Mi sijui tuzidi kusonga nayo
Siri nyingi zimejificha hivi kwanini Zombi amekuwa Zombi... Mwanzo alikuwa ni binadamu wa kawaida... Na vipi kuhusu familia yake???. Na jina lake halisi kabla hajawa Zombi??? Alifikaje kwenye ule msitu???
__________________________________________
ITAENDELEA........
TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.
Maoni
Chapisha Maoni