DENI LA MAISHA SEHEMU YA 3
DENI LA MAISHA
SEHEMU YA 03
GREAT MAN
Hakua na sehemu ya kwenda kwani kipindi kile anasoma kwenye chuo cha elimu ya biashara alikua ni mtu wa kuja tu kutoka mkoani
Miaka ishirini imepita hajui kwao kama ndugu zake ni wazima au wamekufa, john akiwa na sura ya makunyanzi iliyoanza kuzeeka, nywele zilizokaa muda mrefu bila kunyolewa na kufanyiwa usafi lakini nguo zake za muda mrefu zilizochoka zilifanya haonekane kama kichaa ndani ya jiji la dar es salaam.
Kwa muda huo akili ya john ilikua kwa sara tu mwanamke ambae haujui familia yake wala hakujui kwao, aliamua kujitoa muanga na kubeba kesi nzito kwa ajili ya upendo wake na sasa aliona wakati umefika wa yeye kupata malipo yake kutokana na wema aliofanya.
John hakutaka kurudi kwao na kwenda kuangalia maisha mengine, mawazo yake yalikua kwa sara, aliamini baada ya kuteseka miaka ishirini gerezani sasa ni muda wake wa kufurahia maisha akiwa na sara mwanamke anaempenda kuliko kitu chochote.
Siku zilipita, john alikua analanda landa mitaani kama kichaa, aliishi maisha magumu kula na kulala kwa shida, muda mwingine alipita kwenye migahawa ya mama ntilie na kuosha vyombo na kuchota maji kisha mshahara wake ni kupewa kula
Ugumu wa maisha haukufanya akate tamaa aliishi kibishi na kuamini ipo siku atakutana na sara na maisha yake yatabadilika, aliendelea kulala kwenye magofu na kula mabaki ya vyakula vya mama ntilie
Miezi ilikatika hakuwahi kumuona sara japo alipita kumtafuta na kumuulizia kwenye makampuni makubwa ya biashara ambako aliamini yaweza kua sara akawa ameajiriwa huko kutokana na kozi aliemuacha anasomea
Siku moja akiwa ndani ya mgahawa mkubwa jijini dar es salaam anaosha vyombo kwa upande wa mbele kulikua na tv kubwa ambayo muda huo taarifa ya habari ilikua inaruka hewani
Lakini akiwa anaendelea na kazi ya kuosha vyombo alisikia mwandishi wa habari akitaja jina ambalo lilimshtua na kumfanya aache kuosha vyombo na kuja karibu na tv
"Mke wa mheshimiwa raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na mfanyabiashara maarufu Tanzania na duniani kwa ujumla, mheshimiwa sara jackson leo hii amezindua kampuni mpya ya tatu mfululizo ya utengenezaji wa nguo za kina mama na watoto, katika uzinduzi huo mheshimiwa sara jackson.............
John hakutaka tena kuendelea kuosha vyombo, jina la sara jackson ambae alikua anasomea elimu ya biashara katika kozi ya usimamizi wa manunuzi na ugavi alilifahamu vizuri
Aliposikia jina sara jackson, alimkumbuka sara wake ambae walitengana miaka ishirini iliyopita, uzuri wa ile habari ilikua inaonesha na picha za mheshimiwa sara jackson ambae ni mke wa raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania lakini pia ni mfanyabiashara maarufu duniani kwa sasa
Alipoiona ile picha hakuamini ni muda mrefu ulikua umepita, ni yeye ndio alimuona sara mwanamke anaempenda zaidi kuliko wanawake wote, mwanamke alieamua kujitoa mhanga wa kukaa jela kwa ajili yake miaka ishirini
Bila kuelewa john alianza kufurahi huku akiwa anapiga kelele mbele za watu,
"Ndio ni yeye, jamani mmemuona, ni yeye sara mwanamke alieniaidi kua nikitoka jela tunafunga ndoa, hatimae nimempata mke wangu mtarajiwa"
Watu wote ndani ya ule mgahawa walimcheka na jinsi alivyo kuanzia mavazi mpaka muonekano wake walijua yule mtu lazima atakua chizi, walimcheka na kumuacha akiwa anaruka ruka peke yake
Ukweli hiyo ilikua ni siku ya furaha kwa john, lakini furaha yake ilikuja kuzimika baada ya kupata maelezo ya mama aliempa kazi ya kuosha vyombo,
"Nimekuona ukiwa unamfurahia sara jackson kwani unamfahamu" mama mwenye mgahawa alimuuliza john
"Ndio namfahamu vizuri tu sara jackson na muda sio mrefu atakua mke wangu" john aliongea kwa kujiamini
"Mke wako?" Mama mwenye mgahawa alishangaa
"Ndio mke wangu unashangaa nini hiyo ndio ahadi yetu tuliipanga miaka ishirini iliyopita"
"We john inaonekana uchizi unakusogelea, sasa unamuoaje wakati yule ni mke wa raisi, au unaota"
Kauli ya mama mwenye mgahawa ilimshtua john na kubaki ameduwaa
"Yule ni furst lady wetu, mke wa raisi wa jamhuri wa muungano wa Tanzania sasa wewe utamuoaje john, ebu osha vyombo umalize nikupe chakula maana inaonesha umeanza kupagawa kweli"
Maneno ya mama mgahawa yalizidi kumchoma john, aliishiwa nguvu na machozi yalianza kumlenga
"Haiwezekani sara aolewe kirahisi hivyo, aliniaidi nitamkuta na usichana wake lakini mimi ndie nitakae kuja kumuoa na kua mume wake sasa imekuaje kanisaliti" alijiuliza maswali bila kuelewa
"Nimekaa jela miaka ishirini kwa ajili yake nimetimiza ahadi yangu, kwanini ameshindwa kutimiza ahadi zake amenikosea sana, huu ni wakati wangu huu ni wakati wa kumfundisha sara hasara ya kutotimiza ahadi" aliongea maneno ambayo ata mama mgahawa hakuelewa
Tena john aliongea kwa uchungu mpaka mama wa mgahawa akahisi yaweza kua kile kitu kina ukweli ndani yake, maana john alikua anaishi kama chizi haongei sana, sasa siku hiyo aliongea kwa uchungu na kumaanisha
Kwa hasira alizonazo john aliamua kuacha kuosha vyombo na kuondoka kwenye lile eneo huku akimuacha mama mwenye mgahawa akiwa anashangaa...................,...
ITAENDELEA.......
TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.
Maoni
Chapisha Maoni