SAA ZA MWISHO EPISODE 2
SAA ZA MWISHO
****Ep2***
S.P.Owino
Mda ulizidi kusogea tititi! Mshale wa saa ya ukutani ulisogea, mama Kaka na dada Helena walipewa sehem wapumzike usikuule! Bila kufaham kilicho tokea kwa mgonjwa wao!
Ilitimia saa 7:00 usiku
Vipimo vikiwa vina onyesha kwamba tayari nilisha fariki, nilistuka moyo ukiwa kasi kweli nilihisi kizunguzungu na kichefuchefu mpaka nikatapika taa zilikua zime Zima hospitali nzima kimya. Nilijaribu kukohoa sauti ilikua kubwa Sana kwani nilikua mwenyewe nilie toa sauti.
Niliogopa kidogo kwani kulikua na giza niliamka nikapapase ukuta ili nitafute switch niwashe taa, niligusa bila mafanikio ghafla taa iliwaka ndipo nilipo iona ile sura ya nesi Alie kua na mavazi ya kutisha nilitaka kupiga yowe ohooo! Kumbe siwezi kuongea tena ulimi wangu ulikua mzito. Alinisogelea aka niambia wewe niwakwetu na tumekupa siku tano ili ukubali kujitoa kwetu kwa ihari yako na hauta kiona kifo" una siku tano za kua hai ndani ya hospital hii Yani masaa 124, aliupanua mdomo wake alitoa Moshi mweusi ulio nikaba nilikohoa mpaaka Nika poteza faham! Ila kwakwel sura ya yule nesi nakumbuka Kama nilisha wai kuiona sehemu Tena katika familia yetu Ila sikumbuki tu ni wapi!
Ilitimia saa 1:30 asubuhi
Mule aliingia nesi kuja kufanya usafi nesi ambae usiku alikuwepo naalishuhudia nikifariki wakati anafanya usafi Ali hisi Kama mwili unahema aliposogea alitambua nipo hai!
Alikimbia kupeleka taarifa kwa daktari ambae ndo alikua ameripoti mda mchache tu!
Mama Kaka na dada Helena walikua wamesha amka wakisubiri kuambiwa chochote ghafla waliona kundi la nesi likiongozwa na daktari waliingia katika chumba nilichokua nimelazwa mama alihisi labda nimekutwa na Jambo baya aliomba kuingia walimzuia daktari aliomba pazia zishushwe ili ajionee kilicho tokea!
Kweli nilikua hai na ile ripoti iliyo andikwa kuhusu taarifa za kifo changu ilibidi waichane daktari aliomba isije ikaonekana kwani ni hatari kwa hospital yao! Itaonekana Kama wanaua wagonjwa!
ITAENDELEA..........
TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.
Maoni
Chapisha Maoni