SHAIDA SEHEMU YA 3



SIMULIZI: SHAIDA

MTUNZI: AISHA KHAN

SEHEMU YA TATU

"Kaelekea wapi? "

"Mjini"

"Atarudi lini?"

"Sijui. aliniambia nimsubiri atakuja kunichukuwa"

Mzee Athuman hakuongea zaidi. Alimtazama binti yake na kumsikilitia Kwa kutikisa kichwa kisha akaingia ndani.

"Heee!! Sasa itakuwaje mdogo wangu"

Shaida aliangua kilio bila kujua nini kitaendelea kwenye Maisha yake.

"Usilie, jikaze atakuja kukuchukuwa"

"Najikuta naanza kujuta"

"Hapana naimani Eddy anakupenda"

"Aibu hii sijui ntaipeleka wapi"

"Usiongee hivo, kikubwa rudi nyumbani tumsubiri huwenda atakuja hivi karibuni" Aisha alizidi kumtia moyo mdogo wake licha hata yeye pia alikuwa ameanza kupata mashaka.

Siku zilisonga Shaida akiwa amerudi kwao. Baada ya mwezi mmoja kupita, dalili za mimba zilianza kujitokeza kwa binti mrembo Shaida. Haikuchukuwa siku mimba iligundulika ikambidi kuvumilia na kuanza kuilea mimba yake akishilikiana na dada yake. Mpaka miezi sita sasa ujauzito unakaribia kujifungua ila hata siku moja hakuwahi kupata simu kutoka kwa mumewe kipenzi. Shaida alijifungua mtoto wa kike akachukuwa jukumu la kumlea kwa shida na Raha. Mwaka mmoja ukakatika bila simu wala barua kutoka kwa Eddy.

"Em mkataze huyo " ilikuwa ni sauti ya Aisha iliskika kwa ndani ambae alimwambia Shaida amkanye mtoto kukaribia jiko la kuni atakuja kuungua.

"Mtoto mwenyewe mtundu Kama baba yake" Shai aliongea.

"Haaa!! Leo umemzungumzia baby"

"Baby au bebelo" majibu ya Shaida yalimfanya dada yake aangue kicheko.

"Leo hii Eddy kageuka bebelo!"

"Kwanza mada ya Eddy imekuja kujaje hapa "

"Ila nilikuwa na wazo"

"Wazo gani? "

"Unajua mdogo wangu, mtoto kumlea mwenyewe si jambo la kawaida em fikiria Mara mbili mbili utanipa majibu"

"Hapo sijakuelewa"

"Namaanisha hivii... ntajitolea nikusindikize jijini dar es salam, tukamtafute baba Umy ili mtoto apate malezi yote ya baba na mama. unaonaje hapo"

"Hapo sahau... sema wewe nakujuwa, unatamani siku moja wende dar "

"Siyo hivyo mdogo wangu, nataka kukusaidia"

"Basi tutaenda, ila tutamtaftia wapi na mji ulivyomkubwa licha sijawahi kufika"

"Tutajuwa mbele ya safari"

Walikubaliana na harakati za kuhamia jijini dar Es salaam zikaanza. Juhudi zao za kutafuta pesa zilifanikiwa maana mzee Athuman aliwakabidhi laki mbili wakajikuta wana pesa ya kutosha kiasi kwamba hawawezi kufika dar wakahangaika.

Safari yao ilianza mpaka jijini dar es salaam. Kama siku chache walipanga chumba maeneo ya Manzese na harakati za kumtafuta Eddy zikaanza. Siku tatu wakimtafuta Eddy bila mafanikio.

"Mi nilikwambia " Shai aliongea Huku akiwa amekaa kitandani baada ya mzunguko wa siku nzima.

"Kwahiyo? " Aisha alimhoji.

"Yaani hata sijui tunafanyaje"

"Hapa kumpata ni inshu nyingine, ila Nina wazo "

"Wazo gani?"

"Pesa inazidi kupotea kila siku ... Na hatuingizi Bali tunatoa, hii tuichukulie Kama changamoto, ndo hivo tumemkosa na hatujui Kama alitudanganya au laa, Kama vipi tuanze kutafuta kazi"

"Hilo nalo neno, maana baba akiona tunarudi mikono mitupu sijui itakuwaje"

"Bila kumpeleka Eddy nini " Aisha aliangua kicheko na kumfanya Umy nae acheke bila kujuwa wanacheka nini.

"Mwanao ameanza kudata"

"Naogopa kumuachaacha mwenyewe, saahizi kila ntakapokuwa naenda, Ntakuwa naenda nae "

"Ni sawa "

Madada Hawa walianza kutafuta kazi ila nayo ikagonga mwamba. Ila kwa bahati nzuri walipewa taarifa kuwa kuna kazi imepatikana inahitaji watu wa wili, ila kazi hiyo ni kazi ya ndani. Hawakuwa na budi iliwabidi kukubali ili kuweza kayaokoa maisha yao ya mbeleni.

"Sasa nafanyaje na huyu Umy?" Shai aliongea.

"Atabaki"

"Hapana dada ningumu Sana na umeshaskia nikazi ya kulala huko "

"Basi tufanye hivii. Twende ila tujifanye Mimi na wewe hatujuani kisha utaomba ufanye kazi na mtoto utasema siyo Mtundu...wakikataa itabidi nifanye kazi Mimi na wewe ulee mtoto tu "

"Sawa haina shida dada yangu "

Walikubaliana, na siku iliyofuata dalali aliwapeleka Mikocheni maana ndiko walitaliwa wakafanye kazi. Walipofika kwenye mjengo wa kifahari, walikaribishwa ndani mpaka sebuleni aliko baba mwenye nyumba na binti yake.

"Shkamoo" Shaida na dada yake Aisha walitoa salamu Kwa heshima kisha ikapokelewa na mzee huyo na kuwakaribisha wakae.

"Boss ndiyo hawa, naomba Kama hutojali niwaache kwanza" aliongea dalali.

"Sawa nashukuru sana" baba tajiri mwenye mwili wake mzuri aliwageukia kina Shaida baada ya dalali kutoka.

"Enhe!!! Karibuni, sijui mnaitwa kina Nani na mumetokea wapi? "

"Naitwa Aisha natokea mwanza kwasasa naishi magomeni" ilibidi Aisha kudanganya.

"OK na wewe"

"Naitwa Shaida, kwetu Zanzibar ila naishi Manzese kwasasa"

"OK huyo mtoto ni wa Nani? "

"Ni wangu"

Muda huo Kabla boss hajajibu chochote, aliingia kijana mmoja na begi ya nguo, pamoja na mwanamke huku wakicheka kwa furaha. Baada ya kufika sebuleni, binti wa tajiri huyo alinyanyuka na kuwakimbilia Huku akiita "wifi jamani umerudi"

Shaida na dada yake waligeuka kutazama watu hao, wakajikuta macho yao yakipigwa shoti baada ya kumuona Eddy akitabasamu na kufurahiya kumuona binti huyo ambae alionekana kuwa dada yake.

Uso wa Shaida ulipokea huzuni na mshtuko mkubwa baada ya kugonganisha macho na mumewe aliyemtelekeza. Eddy kwake ilikuwa Kama ndoto, hakuamini kuwaona na hapo furaha aliyokuwa nayo ilitoweke na kumuachia mashaka.

"Karibu Sana wanangu. Honeymoon imeendaje huko" tajiri huyo aliwauliza kina Eddy na kumfanya Eddy ashindwe kujibu kutokana na hofu. Shaida pamoja na dada yake Aisha, walishangaa baada ya kusikia Eddy anatoka honeymoon, ikimaanisha huyu mdada aliekuja nae ni mkewe.

"Yes dad. Nimewamiss Sana ndomaana tumeona tuondoke South Africa haraka" mdada Yule mrembo, aliongea kwa kujinadi huku akiendelea kucheka na wifi yake.

"OK! naomba niwatambulishe, Hawa watakuwa wafanyakazi wetu wapya" mzee aliongea na kumfanya Eddy atulie moyoni maana muda wote alihisi Shaida amemfuata yeye. Upande wa Shaida alikaza moyo ikambidi kujifanya Kama vile hajawahi kumuona Eddy kabla.

"But hujanijibu binti... " baba yake Eddy alimgeukia Shaida ambae alishtuka Sana Kama vile alikuwa mbali.

"Huyu mtoto ni wako? "

"Ndio boss" Shai alijibu na kumfanya Eddy amtazame kwa mshangao.

"Sasa utafanyaje kazi na mtoto. Huoni Kama atakusumbua? " aliongea mzee.

"Hapana boss, mwanangu namjuwa vyema, nakuhakikishia hatosumbua" Shaida alijibu huku moyo wa ujasiri ukimuishia na kumfanya machozi yatawale machoni pake.

Eddy hakusubiri Sana, aliondoka Haraka na kumuacha dada yake akimlalamikia.



ITAENDELEA......


TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: BINAMU 🔞 SEHEMU YA 11

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 1-5

CHOMBEZO: MASSAGE ROOM🔞 SEHEMU YA 21