DIMBWI LA HUBA SEHEMU YA 3



SIMULIZI: DIMBWI LA HUBA

MTUNZI: ALLY MBETU

SEHEMU YA TATU

“Vipi?”

“Safi, pole na kazi.”

“Asante, nikusaidie nini?”

“Zulfa yupo?”

“Zulfa! Wewe nani unayemuuliza Zulfa?”

“Ni rafiki yake, naomba uniitie.”

“Mmh! Wewe ndiyo uwe rafiki na Zulfa?” yule mtunza nyumba alishtuka.

“Ndiyo, naomba uniitie.”

“Siwezi, unataka nifukuzwe kazi kwa ajili yako, unamjua Zulfa au unamsikia?”

“Huwezi kufuzwa.”

“Ndugu yangu, wavulana wengi wamekuwa wasumbufu sana kiasi cha

kumfanya mzee ampeleke shule za kukaa hukohuko.”

“Najua hunijui lakini Zulfa akisikia nilikuja na wewe umekataa kuonana naye

naamini utaikosa kazi na kama utanikutanisha naye nina imani utaongezewa

mshahara.”

“Wewe umetoka wapi?”

“Mjini, najua ana siku chache za kuwepo kabla ya kwenda kusoma nje ya

nchi.”

“Pamoja na hayo lakini siwezi kukuitia wacha anifukuze kazi kwa kutokuitia

muhuni kama wewe.”

“Naomba nikutume kitu kimoja wala usimwite atoke nje, nenda tu

kamwambie Sued toka mjini yupo nje.”

“Halafu?”

“Wewe utaona.”

“Bwana wewe king’ang’anizi, ngoja nikamwambie.”

Yule jamaa hakwenda ndani, alizunguka kwenye chumba cha Zulfa na

kumgongea dirishani, Zulfa aliyekuwa amejipumzisha baada ya kuwachachafya

wazazi wake, alijinyanyua na kusogea dirishani, akafungua na kukutana na

Mabula, mtunza nyumba.

“Mabula vipi?”

“Eti kuna jamaa mmoja anasema sijui nikutajie jina lake.”

“Ili iweje? Mabula nimeshakukataza mara ngapi kuniita kutokana na upuuzi

wa wanaume, au nimweleze baba akufukuze kazi?” Zulfa alikuwa mkali.

“Nimemueleza na kusema eti kama akiondoka bila kuonana na wewe, ukijua

basi mimi lazima unifukuze kazi.”

“Mabula usinichekeshe, nikufukuze kazi kwa ajili ya kutoonana na mtu?”

“Amesema na kama ukikutana naye basi lazima uniongeze mshahara.”

“Mabula nawe kwa utani, huyo mtu ni nani?”

“Anaitwa Su..su..sudiii.”

“Acha utani anaitwa nani?”

“Sudi.”

“Anatoka wapi?”

“Mjini.”

“Wewe! Sued au Sudi?”

“Inawezekana ni Sued.”

“Mungu wangu! Mabula unasema kweli au unatania?”

“Kweli yupo nje ya uzio.”

“Mwambie nakuja mpeleke maeneo ya ziwani nakuja huko sasa hivi,” Zulfa

alijikuta katika furaha ambayo hakuitegemea muda ule.

“Dada mbona umefurahi ndiye shemeji nini?”

“Mabula bwana mpeleke kwanza nakuja kama ni yeye nitakupa zawadi

kubwa sana.”

Mabula alirudi mpaka kwa Sued na kumpeleka maeneo ya ziwani kumsubiri

Zulfa huku akimshangaa.

“Aisee rafiki wewe kiboko yaani Zulfa hajawahi kuwa na rafiki wa kiume, sote

huwa tunamwita Bikira Maria.”

“Hata mimi ni rafiki wa kawaida tu.”

Zulfa ndani alipagawa na kuwa kama kuku anayetaka kutaga kwa furaha,

hakutaka kutokea mlangoni kuepuka kuulizwa, akatokea dirishani ili kwenda

kumuona laazizi wake, Sued.

Alikuta Mabula tayari amemfikisha ufukweni Sued na kukaa mchangani

wakiangalia ziwani, mitumbwi ya wavuvi ikipita kwa mbali kidogo huku

mandhari yake ikivutia machoni. Zulfa alitokea nyuma yao bila wao kumuona

na kwenda kumziba macho Sued kwa viganja vyake.

“Mmh!” Sued aliguna.

Zulfa aliondoa mikono machoni na kumkumbatia Seud kwa nyuma na kufanya

wote walale chini.

“Siamini...siamini,” Zulfa alisema akiwa amemshikilia Sued mabegani huku

amemtazama usoni.

“Kwa nini?”

“Yaani wee acha tu, ungekuja kusikia Zulfa ameshafariki.”

“Kwa sababu gani tena mpenzi wangu?”

“Ni historia ndefu, samahani Mabula naomba usogee pembeni utupishe

tuzungumze,” Zulfa alimueleza mtunza shamba wao.

“Dada mi si nikaendelee na kazi?”

“Hapana Mabula, kakae pale unisubiri, ukirudi nyumbani baba akikuuliza

utasemaje?”

“Baba amekwenda mjini.”

“Whaooo! Basi kaa hapohapo mpaka tumalize mazungumzo yetu.”

“Hakuna tatizo dada.”

Mabula alisogea pembeni huku akishangaa kumuona Zulfa akionesha

mapenzi mazito kwa mwanaume, kitu ambacho hakuwahi kukiona katika siku

zote alizokaa pale akiwa mfanyakazi wa kazi za nje. Siku zote aliamini kabisa

Zulfa hayajui mapenzi kutokana na kuwazodoa wavulana wote waliomfuata

kupitia kwake na mwisho kutishiwa kufukuzwa kazi. Lakini siku ile aligundua

kumbe Zulfa naye anapenda kama watu wengine na mapenzi yalivuka mipaka

na kuwa kichaa cha mapenzi.

Wakati Mabula akiwaza hayo, Zulfa bado hakuamini kama angeweza kuonana

na Sued siku kama ile, mtu ambaye alikuwa ameanza kumkatia tamaa na kutaka

kutoroka kumfuata mjini.

“Unajua siamini!” Zulfa bado alionesha kumshangaa Sued.

“Kwa nini Baby?”

“Nimeamini Sued unanipenda, sikuamini kama ungefunga safari kuja mpaka

huku kunifuata.”

“Wee acha tu huwezi kuamini uzalendo ulinishinda nikaja shule kuuliza.”

“Wewee! Pale shule hawaruhusu mtu yeyote kuingia tofauti na mzazi au

mlezi, tena anayefahamika kwa maandishi.”

“Basi mimi nilifika kukuulizia.”

“Naona uliishia getini, walikujibu nini?”

“Nilitengeneza uongo wa ajabu.”

“Wewee! Ikawaje?”

“Nilikutana na mkuu wa shule.”

“Muongo! Yupoje?”

“Mzee mmoja amefuga sharubu.”

“Mmh! Labda ulimuona nje.”

“Alinikuta getini nikiulizia kwa mlinzi, alinishangaa kuwepo pale, ndipo

niliposogea kwenye gari lake na kukuulizia.”

“Jamani Sued, ulimuulizia vipi ikiwa familia yangu yote anaijua?”

Sued alimueleza alivyomuulizia na majibu aliyojibiwa shule.

“Baada ya kuelezwa unasafiri bado wiki mbili, nilichanganyikiwa siku ile kwa

kweli nilishindwa kula.”

“Mmh! Pole sana mpenzi wangu, hata mimi nilichanganyikiwa kufikia hatua

ya kukorofishana na wazazi wangu.”

“Kwa sababu gani?”

Zulfa alimuelezea yote yaliyotokea wiki mbili kabla ya kurudi shule na yote

yaliyoendelea mpaka asubuhi ya siku ile.

“Kwa hiyo ulikuwa unasemaje?” Sued baada ya kumsikiliza Zulfa alimuuliza.

“Wazo langu lilikuwa kutoroka na kukufuata mjini tuishi pamoja.”

“Mmh! Tutaishi vipi ikiwa wazazi wangu hawawezi kukubali nikae na

mwanamke?”

“Sasa tutafanyaje, lazima nitoroke katika siku hizi mbili.”

“Mmh! Huu mtihani.”

“Sued acha kuniangusha nakutegemea wewe, mimi nitachukua ndani kiasi

kikubwa cha fedha na kwenda kuishi popote bila matatizo.”

“Tukitafutwa?”

“Kuna sehemu zingine hata magazeti hayafiki, tukienda huko tutakaa muda

mrefu na dawa uwahi kunipa mimba tutakuwa tumefuta safari ya kwenda nje

kusoma kwa vile nitakuwa najiandaa kujifungua.”

“Zulfa naweza kufia gerezani.”

“Nakuapia kama tutafanikiwa kutoroka na kubeba ujauzito nikijifungua

salama narudi nyumbani.”

“Wazo siyo baya, nami nimepata wazo, tukatafute nguo za kuvaa pia ndevu

za bandia ili watu wasikufahamu kama mwanamke ili tuweze kuishi kwa muda

mrefu.”

“Wazo lako zuri, lakini mbona umbile langu la kike nitawezaje kuishi kama

mwanaume?”

“Sikiliza Zuu, kifuani kwako matiti ni madogo hivyo hata ukivaa kanzu hakuna

wa kukujua kama wewe ni mwanamke.”

“Mmh! Sawa, basi katafute vitu vyote hivyo kisha uje tuondoke au mimi

nikufuate mjini?”

“Hapana, tutaondokea hapahapa, wakati unazungumza hayo nilipata wazo.”

“Wazo gani?”

“Upande wa pili wa ziwa hili kuna nini?”

“Kuna vijijini, nasikia wavuvi wa samaki ndiyo wanaoishi huko.”

“Basi huko ndipo pazuri.”

“Bebiii sijazoea maisha ya kijijini, kwa nini tusiende mkoa wowote na kupanga

kwenye hoteli yoyote na kuishi ndani bila kutoka?”

“Tukienda mjini kama tutatafutwa ni rahisi kupatikana, lakini baba yako

mawazo yake yote yataelekea mjini kwa kukutangaza katika vyombo vya habari.

Hapo lazima tutakamatwa kwa muda mfupi pengine kabla hata huo muda wa

kwenda shule haujaisha.”

“Lakini kweli, lazima nikiondoka baba atahamishia mawazo yake mjini na

kutufanya tuishi bila wasiwasi.”

“Sasa tutafanyaje, mi sina fedha.”

“Usiwe na wasi, nikiingia ndani nitamtuma Mabula akuletee.”

“Tunatakiwa tuondoke lini?”

“Kesho, tusipoteze muda, ondoka sasa hivi ukafanye manunuzi ya vitu hivyo.

Kesho njoo majira ya mchana na kwenda kufanya mipango na watu wenye

mitumbwi ya injini mkubaliane kiasi gani cha kutuvusha ng’ambo ya pili. Usiku

nitatoa vitu vyangu vya muhimu vya kutumia huko tuendako na kuvificha

sehemu ili nikitoka mtu asijue chochote.”

“Hakuna tatizo.”

“Basi ngoja nikachukue fedha ili uwahi mjini,” Zulfa alinyanyuka alipokuwa

amekaa na kumgeukia Mabula aliyekuwa mbali kidogo.

“Mabula njoo,” Mabula alisogea kusikiliza alichoitiwa:

“Naam.”

“Kuna mzigo nitakupa umletee huyu.”

“Hakuna tatizo.”

“Mpenzi kama hivyo basi, bai,” Zulfa alimbusu Sued mbele ya Mabula kisha

alimshika mkono Mabula na kurudi naye ndani. Kabla hajafika mbali aligeuka na

kumueleza:


ITAENDELEA.......



TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: BINAMU 🔞 SEHEMU YA 11

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 1-5

CHOMBEZO: MASSAGE ROOM🔞 SEHEMU YA 21