PENZI LA KIKOMANDO EPISODE 2
PENZI LA KIKOMANDO
ABELUKA FILM
EPISODE:02
TULIISHIA
Kiongozi anatoa amri kwa sauti kali "uweniiiiiii" ghafla sauti nyingine ya kike inasikika nyuma yao.
"Subirini kwanza ..." Ilikuwa ni sauti nyororo tamu sana iliyowafanya waasi wote wageuke kutazama ni nani huyo aliyefika hapo majira hayo ya usiku ndani ya msitu wa vita?
ENDELEA...
Waasi wote wanageka na kumuona mwanamke mmoja mrembo aliye shika siraha kubwa mkononi .
"We binti ni nani?..na unafanya nini saa hizi za usiku? au upo pamoja na huyu mwanajeshi?...." Aliongea Aboku ambaye ni Kiongozi wa wale waasi taratibu akiwa anamsogelea karibu yule mwanamke.
"Naitwa wonder nimekuja kufanya biashara na nyie, ila kama hamtoitaji mi naondoka..?
Aliongea binti kwa mapepe sana akiwa anamuangalia James.
"Biashara!!, Biashara gani binti?...." Aliuliza Aboku akionekana kushangazwa .
Wonder taratibu anaingiza mkono wake kwenye suruali aliyovaa na kutoa kitu ambacho kinamfanya Aboku ashituke na kushangazwa nacho.
"Gold key !! , Binti umepata wapi huo ufunguo ..." Aliongea Aboku kwa furaha sana akiwa anamsogelea wonder karibu zaidi ili apatiwe ufunguo ule aliokuwa nao Wonder mkononi.
"Mm, mmh ,mmh ... Hapana nipatie huyo kijana mliye mshikilia na mimi nitakupa Gold key ..." Aliongea wonder akiwa anaufichaufunguo nyuma yake.
Aboku anashikwa na hasira za ghafla baada ya kuambiwa amuachie James.
"We binti unanitega ety? siwezi kumuacha uyu askari..."
Msaidizi mmoja wa Aboku anamsogelea Aboku mpaka sikioni na kumnong'oneza.
"Mkuu hasira za nini sasa, tumuachie tu huyu jamaa tuchukue Gold key,Tukipeleka hii makao makuu bosi atafurahi sana....." Aliongea yule msaidizi kwa kunong'ona sikioni kwa Aboku.
"Wote shusheni silaha chini ..."Aboku alitoa amri james aachiwe baada ya kupatiwa ushauri kidogo na yule msaidizi wake aliyefahamika kwa jina la kipeta, waasi wote wakashusha siraha walizoelekeza kwa James.
"Binti siwezi kukupa huyu mtu kirahisi rahisi hivi kwa sababu ameuwa watu wengi lazima alipie.. " Aliongea Aboku akiwa ananyanyua siraha yake.
"Sasa unataka kumfanya Nini?.." aliuliza wonder Aboku anajibu kwa vitendo anampiga James risasi moja kwenye paja la mguu wa kulia .
"Ahaaaaaaaaa.........." James alipiga kelele za maumivu.
"Haya binti mtu wako huyo hapa unaweza kumchukua naomba sasa hiyo Gold key... "
Aliongea Aboku akiwa anamsukumia James kwa Wonder.
Wonder bila kujiuliza mala mbilimbili anampatia Aboku Gold key kisha anashika mkono wa kushoto wa James na kuuweka kwenye bega la mkono wake wa kulia ili amsaidie James kutembea sababu tayari James alikuwa ana risasi mguuni.
"Kwa herini jamani........"aliongea
Wonder kwa sauti ya juu akiwa anaondoka na James .
"Bosi hatimaye Leo tumeipata.."
Wonder alipofika mbali kidogo na waasi akaanza kumkokota James kwa haraka.
"Ayaaaaaaaaaa!.....unaniumiza we binti twende taratibu basi! ..."
Aliongea James kwa sauti iliyobeba maumivu makali .
"We mpumbavu inatakiwa tutoke haraka ndani ya huu msitu maana Hao jamaa nimewachezea mchezo wa kitoto..." Aliongea Wonder akiwa anaendelea kumkimbiza James mchaka mchaka.
KWA WAASI
" Hahahaha, hahahaha leo nimekupata Gold key, mwa..mwa..mwa " Aboku alikuwa akicheka sana na kuibusubusu Gold key kwa furaha wenzake wakiwa wamekaa pembeni wanamtazama tu kiongozi wao alivyo pagawa.
Kadri Aboku alivyozidi kuishika shika Gold key ndivyo ilivyozidi kutoka rangi ya juu. Aboku anashituka baada ya kuona rangi ya gold inatoka katika funguo , anachukua tochi na kuangalia kwa umakini ndipo anagundua amepewa kitu fake.
" Nyie washenzi chukueni silaha zenu haraka watafutwe na wauliwe wajinga hawa....." Alitoa amri Aboku kwa hasira sana akianza kukimbia yeye kuelekea kule walikoelekea Wonder na James.
UPANDE WA PILI WA MSITU
" Wewe ni nani ?, Kwanini umenisaidia mimi.?.na ile gold key uliyowapatia wale waasi umeipata wapi? ..." James alikuwa akimuuliza wander maswali mengi lakini wonder hakujibu hata moja aliendelea kumvuta James haraka haraka.
Ghafla sauti za waasi zinasikika nyuma yao zikiambatana na milio ya risasi.
"We binti hawa wana tutafuta tena sisi wakati umesha wapa gold key! , Kwa nini sasa ?
"Ndio wanatutafuta sisi, niliwapatia gold key fake sasa itabidi tuongeze mwendo hata kama kimguu chako kibuvu lasivyo tutafia huku...." Aliongea wonder akiwa anamuweka vizuri James begani na kuendelea kumvuta.
Binti kimbia okoa maisha yako mimi niache hapa hapa nitajua la kufanya sitaki uwe kwenye hatari sababu yangu...". Aliongea James aliposikia sauti za waasi nyuma yao zikiendelea kusikika kwa kishindo zinakaribia walipo wao.
"Unafikili kwa hayo maneno yako ndo nitakuacha. Kwa taarifa yako haachwi mtu hapa Kama kufa tutakufa wote sawa we Afande kijana..." Aliongea wonder akiendelea kumkimbiza James.
Waasi walitawanyika msituni ili wampate James na wonder lakini ilikuwa ni kama kazi bure sababu James na wonder walipita njia tofauti iliyowafanya watoke nje ya ule msitu wa vita. Sehemu wanayoingia ni tulivu na yenye kiza kinene kana kwamba hakuna mtu yeyote anayeweza kumuona mwenzake ndani ya eneo hilo mida hiyo ya usiku.
"We Afande nilikwambia lazima tutawapoteza wale waasi umeona Sasa..." Aliongea wonder kwenye hicho kiza kinene lakini James alikuwa kimya tu alionekana kupata maumivu makali mguuni.
" Uliniambiya unaitwa James okay James inatakiwa tuitoe risasi kwenye paja lako Sasa hivi...." Aliongea wonder akiwa anamsaidia James kukaa chini .
"Hotoweza kunitoa risasi na hiki kiza we mwanamke, acha tu nitajaribu mwenyewe....." Aliongea James akionekana kupatwa na maumivu sana mda huo wakiwa hata hawaonani sura zao sababu ya kiza kinene.
" Subiri na uone..." Aliongea wonder akiwa anapapasa papasa pembeni kutafuta kimti
Anachukua kimti na kumuwekea James mdomoni.
"Jikaze...." wonder taratibu anapeleka mkono wake sehemu ilikopita risasi kwa hisia bila kutumia macho. Vidole vinazama ndani ya jeraha kutafuta risasi huku meno ya James yaking'ang'ania kwa nguvu kijiti kilichokuwa mdomoni.
"Haaaaaaaaaaaaa..." James alipiga kelele kubwa baada risasi kuvutwa kwa nguvu .
"Hahahaha tayari imetoka umeona sasa ....." Aliongea wonder akiwa anacheka risasi akiwa ameishika mkononi.
James akaichana nguo yake ya jeshi na kujifunga sehemu ilipotolewa risasi ili kuzuia damu.
" We kweli ni malkia wa nguvu mrembo hongera..." Aliongea James furaha yake ikionekana kurejea akiwa anakaza kitambaa alichojifunga pajani.
"Hahahaha..nilikwambia afande kijana mi huwa sishindwi kitu... "
Kweli mrembo.."
"Acha uongo Afande umejuaje Kama mi mrembo wakati tumekutana mazingira ya kiza.."
"Hahahaha sawa nitakuona vizuri kesho asubuhi.."aliongea James usingizi ukianza kumkamata maeneo hayo.
"Afande mbona Kama unalala unayaamini haya maeneo..?
"Usiniulize zaidi maana huishiwi maneno mi nalala.."
"Sawa lala mi nitakulinda na huu mjegeja wangu.."
Usiku huo wa saa tisa James na Wonder wanapitiwa na usingizi wakiwa katika eneo hilo lenye kiza kinene.
ITAENDELEA.....
Je , wataweza kuwa salama usiku mzima wakiwa wakiwa ndani ya Hilo pori
Je, nini kitatokea asubuhi yake ?
Vita vikaliiii
Siri iliyojificha kuhusu wonder ni Nani huyo binti na Kwanini ametoa msaada kwa james??
TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.
Maoni
Chapisha Maoni