Kocha wa Yanga Atajwa Simba

Kocha wa Yanga, raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi. IMEELEZWA kuwa, licha ya Mwekezaji wa Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’, kuachia nafasi ya Uenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo, lakini bado anahusika kwenye baadhi ya mambo ikiwemo kipindi hiki cha mchakato wa kusaka kocha mpya wa kuinoa timu hiyo. Wakati Simba ikiwa kwenye mchakato wa kumsaka mrithi wa Kocha Didier Gomes aliyeachia ngazi Jumanne ya wiki hii, baadhi ya viongozi wa Simba wameonekana kulijadili jina la Kocha wa Yanga, raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi. Kwa mujibu wa chanzo kutoka Simba, viongozi wa timu hiyo wamekuwa bize kwenye vikao juu ya kuangalia nani atakuwa kocha sahihi wa kurithi mikoba ya Gomes. Mtoa taarifa huyo alieleza kwamba, katika mjadala wa kumpata mrithi wa Gomes, wapo waliolitaja jina la Nabi kutokana na kuhitaji kocha ambaye anayajua mazingira ya soka la Tanzania, lakini pia mwenye uzoefu wa michuano ya kimataifa. “Ndugu yangu suala la kupata kocha mpya limechukuliwa sura tofauti sana na Mo, kwani...