BALAA LA PENZI LA JINI, PART:05



BALAA LA PENZI LA JINI

MTUNZI: McLAURIAN


PART: 05

Ilipoishia, Haya sasa, wakati kaylin anaendelea kumsubiria mme wake kwa hasira kali, Dicky yeye hatimaye alibakiza mwendo mfinyu mno kufika nyumbani kwake.
Alipunguza speed kisha akaikata kona na kuelekea nyumbani kwake huku zikiwa zimebaki mu
Mita chache hivi mpaka nyumba yake ilikuwa inaonekana kwamacho.
Barabara ya kwenda kwake, ilikuwa mbovu hivo alipita kwa uangalifu mkubwa sana hali iliyopekekea mke wake kuhisi kama kuna mlio wa gari .
Kaylin alisimamisha masikio yake kama panya aliyehisi uwepo wa panya huku macho yakiangaza huku na huko.

Haya sasa, Dicky hatimaye alifika getini kwake huku akiwa .mtupu kabisa na bila kujijua kama yupo mtupu ndipo alipowasha taa iliyofatiwa na mlio wa honi.
Kama haamini hivi, Kaylin alijifunga kanga yake vizuri kisha akaenda kufungua mlango wa geti...

KILICHOENDELEA MI SIJUI...

SONGA NAYO...

Taratibu mlango ule ulifunguliwa na Kaylin ndipo alipoona gari ya mme wake. Moyo ulimpweta mbiombio, machozi yakaanza upya kuchuruzika huku uso wake ukiwa ukejaa ndita kama mikunjo ya kontua kwa sababu ya hasira kali.

Dicky baada ya kuzama getini mwake, alifungua mlango wa gari yake kisha taratibu akaanza kushuka ndipo alipohisi kama mwili wake kuwa na baridi hivi . Wakati anahisi ubaridi huo, Kaylin alistaajabu na kutoa macho kama maskini aliyeshinda BIKO ya milioni 50.
Alimtazama kwa mara nyingine huku akidhani labda macho yake yamewekewe ukungu lakini ilikuwa hivohivo.
Bila kuongea chochote, Kaylin aliingia ndani kisha akaketi kwenye sofa.
Ama kweli kilikuwa kituko kwa Dicky ambaye alikuwa mtupu kabisa huku akiwa hajui kama yupo hivo.

Dicky naye aliingia ndani akiwa mtupu mpaka sebuleni hapo huku uso wake ukionesha wasiwasi mkubwa sana .

"Ehee.! Unatokea wapi mda huu!," kwa sauti ya ukali ambayo ilichoma mpaka moyoni mwake , Kaylin alimwambia mmewe huku akiendelea kumshangaa.

"Samahani mke wangu nilipata hitilafu baada ya gurudumu la mbele kupasuka ndiyo maana nimechelewa wala usinichukulie vibaya..i love you" Dicky bila aibu yoyote alimwambia mkewe kisha akataka kumkumbatia na kuachia busu la upendo lakini lilikataliwa katakata na Kaylin.

"Niache wala usiniguse..!" Kaylin alimsukuma mme wake.

"Mke wangu mbona huniamini? Mimi nakupenda sana wala siwezi kukucheat hata siku moja" Dicky alimbembeleza mke wake kwa maneno laini.

"Hivi umechanganyikiwa au ! Unajiona upo sawa hapo!" Kaylin alimwambia mmewe.

Baada ya kuambiwa hivo, Dicky alishangaa kuona anaambiwa hivo ndipo alipojishika mfukoni mwake ili atoe simu yake iweze kumpa kampani lakini aliishia kujishangaa mwenyewe mara baada ya kujikuta mtupu kabisa.

Maneno yalikata, aibu kali ikatanda moyoni mwake kisha akainamisha kichwa chake chini.
Bila kuongea chochote kile alitaka kunyanyuka kwenda chumbani kwake ili walau akapate nguo za kujistiri lakini mke wake alikuwa mkali kama mbogo aliyejeruhiwa.

"Hakuna kuondoka hapa mpaka useme kwanini unatembea na wake za watu ..." Kaylin alivuta mkonga wa mme wake ili asiondoke.

Dicky alikuwa mlaini kweli huku akijilaumu kwanini amajisahau mpaka anasahau kuvaa nguo.
Alikaa chini kisha akajitutumua kama mwanaume na kutoa kauli..

"Aisee mke wangu kuna vibaka walinivamia wakati gari yangu imepata hitilafu kisha wakataka niwape chochote na bahati mbaya sikuwa na pesa yoyote .Nilipowambia hivo hawakunielewa kabisa mpaka walipochukua maamuzi ya kunivua nguo zote pamoja na simu zangu zote.." Dicky huku akiwa anapepesa macho, alimwambia mke wake.

"Hivi unanionaje? wewe wakunidanganya kiaso hiki! Kwa taarifa yako naelewa kila kitu mwanzo mwisho.." Kaylin alimwambia mmewe.

Baada ya kuambiwa hivo, Dicky alishituka kama mtu aliyepigwa na shoti ya umeme lakini siku zote mfa maji hakosi kutapatapa ndipo alipozidi kukomalia msimamo wake.
Alijishika kichwani mwake kisha akaanza kujikuna kama mtu mwenye chawa ndipo makosa makubwa ya kudondosha jani dogo lililokuwa kichwani mwake lilipofanyika.

Baada ya jani hilo kudondoka, Zayna alizinduka kaburini kwa mara moja ndipo alipomuona Dicky akiwa nyumbani kwake.

",Hee! Si alijifanya mjanja sasa atatapika nyonga au akubali tuishi wote huku!" Zayna alijisemea mwenyewe.

Alinyoosha mikono yake juu kisha akaishuka ndipo sura yake ilipobadilika. Kucha zake zilirefuka sana kwa mita kama 2 hivi, shingo lake lilikuwa kama la twiga huku uso wa sura yake ukiwa unatisha kwelikweli.
Alivaa nguo yake nyeupe kisha akaifunga kipande cha kitambaa cheupe ili safari ianze.

Zayna alikuwa kwenye muonekano wa kutisha sana mpaka yeye akawa anajiogopa japo ni mwili wake.

Haya sasa, Dicky kichwa kikiwa kinamuuma na mkewe pia kwa mawazo makali sana, aliamua kwenda chumbani kisha akavaa pensi na kaushi.
Hali ya ububu ilitawala ndani humo ndipo Dicky alipoamua kwenda kwenye gari lake walau apunguze upweke na kuandaa majibu ya kumridhisha mkewe.

Kaylin aliingia chumbani mwake kisha akajilaza kwa mda ndipo alipoanza kujiuliza maswali ambayo yalikosa majibu mda huo.

"Sasa hapa niondeke nirudi kwetu lakini itakuwaje? Au nibaki nyumbani hapa lakini nitakaaje na mme ambaye sio muaminifu ? Ee mola wangu naomba unipe nuru ili niweze kumaliza mtihani huu mgumu sana kwangu..." Kaylin alijisemea mwenyewe huku akibaki njia panda juu ya nini afanye...

Naye Dicky..., aliingia ndani ya gari yake huku kichwa kikiwa kinamuuma kwelikweli.
Haya sasa, akiwa anaanda majibu ya na maelezo ya kutosha, Zayna alianza safari yake akiwa anapaa angani mpaka nyumbani kwa Dicky.

Sekunde chache sana, Dicky akiwa kwenye gari alishangaa kuona mwanga mkali ukiwaka huku kikionekana kitu cha ajabu, vinyweleo vyake vilisimama ndipo alipotoa sauti ya mshangao.

"Hee!.." Nini hiki...Dicky alisema huku akiwa ametoa macho

"Leo ni leo.." Sauti ilisikika kwenye gari ndipo Dicky alipotaka kufungua mlango wa gari lakini haukuweza kufunguka...

JE ILI ILIKUWAJE?....

TUKUTANE SEHEMU IJAYO....

BAKI HAPA HAPA KWENYE APP YETU, MUITE NA MWENZAKO

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: BINAMU 🔞 SEHEMU YA 11

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 1-5

CHOMBEZO: MASSAGE ROOM🔞 SEHEMU YA 21