MCHUNGAJI MCHAWI, EPISODE:11



Story: MCHUNGAJI MCHAWI.

Mtunzi: Nellove

Episode: 11


Ilipoishia...

Alipofungua mlango tu macho yake yalitua juu ya wazee watatu waliokuwa hapo nje wanamtazama.

Endelea...

Mshituko mkubwa ulitua ndani ya moyo wake, nao mshangao haukuwa mbali kwani sura zilizokuwa mbele yake zilikuwa ngeni kabisa machoni pake.
Sasa taa ziliwaka ndipo alipofanikiwa kuwaona vizuri zaidi wazee hawa. Kumbukumbu zake zilithibitisha kwamba ni kweli hakuwahi kuwatia machoni hawa watu,, Mchungaji alibaki ameduwaa tu.
"Vipi bwana mbona hutukaribishi?" Alitamka mzee mmoja aliyekuwa mbele zaidi na bila shaka ndiye aliyegonga mlango.

"Ah! karibuni wazee wangu" alisema kwa kubabaika Mchungaji alionekana kushindwa kabisa kuidhibiti ile hali ya wasiwasi iliyomtawala. Muda wote alikuwa anajiuliza ni nani hawa? Wametoka wapi na wamefuata nini kwangu usiku huu?? Alijiuliza maswali mengi sana bila kupata majibu ndipo alipoona ni busara kukaa nao awasikilize. Basi aliingia nao ndani na kuwaonesha mahali pa kukaa. Wazee walikaa na moja kwa moja waliyaelekeza macho yao kwa Mama David aliyekuwa chini. Walimtazama kwa sekunde kadhaa kisha walimgeukia Mchungaji Joshua.

"Habari za hapa bwana" alitoa salamu mzee yuleyule aliyeonekana kuwa muongeaji.
"Salama kidogo, sijui mtokako" alijibu Mchungaji,,, wazee hawakuonekana kushitushwa na jibu hilo.
"Tutokako ni heri"
"Oooh! Shukurani, karibuni sana." Alisema mchungaji huku akimtikisa mwanae kwa staili ya kumbembeleza. Macho yake yaliyojawa na mshangao yalikuwa kwa wazee hawa ambao nao walikuwa kimya wanamtazama Mama David kwa mara nyingine,, ukimya ulitawala.
"Naaam karibuni wazee wangu"
"Ahsante sana" alijibu tena yule mzee,, hali nile ilimpa wasiwasi Mchungaji.
"Mmmh!" Aliguna.

Walitumia sekunde kadhaa kumtazama Mama yule kama watu wenye kudadisi jambo kisha muda mfupi baadae walianza kujitambulisha kila mmoja. Alikuwepo mzee aitwaye Mbira, Kingozi pamoja na mzee Makusi yule muongeaji.
"Nashukuru sana kuwafahamu, basi wacha niwapatie chochote kulainisha koo" alitamka na kutaka kuinuka lakini walimzuia.
"Hapana! wala usisumbuke tafadhali,,,, sisi sio wakaaji hapa japo itategemea lakini bila shaka hatukai sana" aliongea mzee Mbira.
"Anhaa sawa" alijibu Mchungaji,, hlizuoa ukimya mfupi tena,,, hakika hakupata kuwaelewa wazee wale.



"Kwanza nikupe pole kwa yote yaliyokukuta" alizungumza mzee Makusi.
Kabla mchungaji hajajibu alishangaa na kujiuliza kama wanajua juu ya yaliyomkuta,, kumbuka tangu jana hakuthubutu kumwambia mtu yeyote kuhusu hili, sasa hawa wamejuaje?? Au wamekosea nyumba?
Hakutaka kuwaza sana kwani aliamini pengine ni kwa sababu wamemuona mke wake alivyolala pale chini.
"Ahsante sana"
"Sawa sasa sisi tumekuja hapa kwa jambo moja tu." Alisema mzee Makusi na kujikoholesha kidogo.
"Naaam! nawasikiliza wazee wangu"
"Tunahitaji kukusaidia juu ya changamoto iliyokukuta,, ukifanya uzembe hakika utampoteza huyu Mama" Hii ilikuwa kauli iliyomchanganya sana mchungaji. Na kama hilo ndilo lengo lililowaleta sasa wamejuaje kama kuna shida hiyo? Nani amewapa taarifa?

"Mmmh!! Nashindwa kuwaelewa wazee wangu. Mnasema mmekuja kutoa msaada,,, mmefahamuje kwamba kuna tatizo ilhali siwafahamu na bila shaka hayupo aliyewapa taarifa???"
"Huu sio muda wa kuhoji hayo,,, wewe turuhusu tufanye kazi"
"Ni msaada gani mnataka kutoa???"
"Utaona,,, wewe turuhusu tufanye kazi" Mchungaji Joshua aliendelea kuchanganyikiwa,, Swali moja lilipata kugonga kichwa chake.
"Hawa wana uwezo gani wa kumsaidia mke wangu wakati huo nimekesha usiku mzima kumuombea bila mafanikio?"
Aliwaza huku anawatazama,, akili yake ilimwambia wale ni washirikina. Naye hakuwa tayari kuruhusu ushirikina ndani ya nyumba yake.

"Ni vyema kama utaturuhusu mapema,,, Tuna muda mchache sana sana,,, tafadhali turuhusu tufanye kazi"
Mchungaji alitabasamu na kusema
"Hiyo ruhusa haipo wazee wangu hivyo kama hamna lingine basi kistaarabu naomba muondoke tu"
"Aaaah! Unaamua kutufukuza sasa!!" Alizungumza kwa namna ya kustaajabu mzee aitwaye Kingozi.
"Mna lingine??? Kama halipo Naomba muondoke" Mchungaji alisimamia msimamo wake.
"Sawa sisi tunaondoka lakini unamtesa mtoto,,, atanyonya wapi na utamleaje?? Utatukumbuka"
Baada ya kusema hayo wale wazee walitoka nje kuondoka,, Mchungaji Joshua alipiga hatua za haraka kwenda kufunga mlango na kabla hajafunga aliangaza macho huku na huku labda atawaona lakini hakuwaona.

"Kwamba ndani ya sekunde chache wameshakata kona ile?? Mmmh!!!" Mchungaji alishangaa maana haikuwa rahisi hivyo alipata wasiwasi mkubwa juu ya wazee hawa.
Aliamua kufunga mlango,, aliufunga vizuri na kurudi sebuleni,, alikaa kwenye kochi pembeni yake alimlaza mtoto. Macho ya mchungaji yaliganda kwa Mama David,,,
'mmmmmphuuuuu!!!!' alivuta pumzi ndefu na kuiachilia kwa nguvu,, ama hakika alichoka loooh!

Wimbi la mawazo lilianza kubugudhi kichwa chake,,, maswali kemkem yaliyokosa majibu yalimgonga kichwa bila kumuonea huruma,, alizama kwenye dimbwi la mawazo na maswali. Pengine asingetoka kwenye dimbwi lile ila sauti kali ya kilio cha mtoto wake ilirudisha akili zake sawasawa. Mtoto alikuwa analia kwa nguvu pengine kuliko muda mwingine wowote ule. Alimbeba na kumbeleza lakini wapi,, Alijaribu kumnywesha tena uji,, mtoto alikataa katakata,, alikuwa analia tu.

"Mmmh!! Huu ni mtihani sasa na sijui utaisha lini" alisema na kukumbuka maneno ya wale wazee.
"((Sawa sisi tunaondoka lakini unamtesa mtoto,,, atanyonya wapi na utamleaje?? Utatukumbuka))"
Ama hakika aliwakumbuka japo hakujua ni namna gani wangemsaidia.
Muda ulienda kwa kujikongoja sana na sasa ilikuwa saa nne usiku,, ama hakika asubuhi ilikuwa mbali.
"Kutakapopambazuka nitampeleka hospitalini" alisema baada ya kuona hakuna namna. Na sasa alitamani angekuwepo na mzee wa kanisa hapo ili wasaidiane lakini mzee huyo alikuwa safarini kuelekea Rukwa.

Alitamani pia hata angefanya mawasiliano na wazazi wa mke wake lakini Mama yake alifariki muda sana na Baba yake ndio yule adui yake mkubwa ambaye anaitwa mzee Jangala,, ni adui mkubwa akiwa miongoni mwa wachawi wa Tungi, sasa wangeongea nini???
"Kesho nampeleka hospitali akatibiwe"
Hiyo Kesho ilikuwa mbali sana.

Majira ya saa 5 za usiku akiwa palepale sebuleni usingizi unamnyemelea nyemelea ghafla ilisikika sauti ya glasi ikidondoka chini na kupasuka. Alishituka sana, nao usingizi ulipotea moja kwa moja. Alitazama huku na huku kisha alikaa kimya baada ya kusikia upepo ukivuma kwa mbaaali. Moyo ulidunda na hofu iliongezeka zaidi punde tu aliposikia sauti ikimuita kutoka chumbani.
"Babaa!!!"
Hii sauti ilimtisha hata hivyo ilimfanya amkumbuke mwanae. Alitazama mahali alipomlaza mwanae,, hakuwepo.
"Yuko wapi???" Alijiuliza na kuangalia chini ya meza,,, hakutaka kuamini kama ndiye aliyepo chumbani. Ni mdogo ameendaje chumbani?? Hata kama angeenda na huo uwezo wa kutamka ameupata wapi?? Na kama sio yeye je mtoto yuko wapi?? Mama yake angekuwa mzima labda Mchungaji angesema ni yeye ndiye kamchukua mtoto,, Mama yupo chini hajielewi.

Akili ya Mchungaji Joshua ilivurugika zaidi.

Wewe unahisi angefanyaje??? Aliamua kupiga hatua kuelekea chumbani kuhakikisha ni nani huyo aliyemuita lakini hata kabla hajafungua mlango wa chumbani kwake ilikuwa ghafla mlango wa nje uligongwa. Akiwa ameduwaa basi kwa mbali alisikia mlango ukifunguliwa kisha hatua za watu waliokuwa wanatembea kuingia ndani zilisikika.
"Mmmh!! kwani mlango sikuufunga???" Alijiuliza,,, kumbukumbu zake zote zilimwambia aliufunga vyema na ni kweli kabisa aliufunga mlango ule wa nje,, sasa imekuwaje?? Kwanza alisitisha lile zoezi la kumtafuta mtoto.
"Ee Mungu nisaidie!??" Alisema hayo huku Macho yake akiwa ameyaelekeza upande ule ulipo mlango.

Ndani ya sekunde ambazo hazikuzidi 20 alipata kuwaona wazee wapatao watano kwa idadi wakiingiia huku wameshika mishumaa mikononi mwao. Miongoni mwa wazee hawa walikuwepo wale wazee watatu waliokuja mara ya kwanza na sasa walikuwa wamevaa kanzu nyeusi zenye kofia ambazo zilifunika vichwa vyao. Wazee wengine wawili walivaa kanzu nyeupe na kujifunga vitambaa vyeupe usoni,,, hawa sasa hakuwatambua.

"Mbona naandamwa hivi?? Ni wapi nimekosea??" Alijiuliza mchungaji Joshua huku moyo ukimdunda kwa kasi kutokana na maajabu anayoendelea kuyashuhudia,, hakujua nini kitatokea hapo.
Wale wazee waliingia huku wanaimba kwa sauti ya chini na hawakuonesha kumjali sana Mchungaji Joshua. Walitembea taratibu hadi Mahali alipolala Mama David na kuanza kumzunguka huku wakiendelea kuimba.

Mzee mmoja alivua kofia ya kanzu na kufungua kitambaa chake alichofunga usoni,,, mchungaji alipata kuiona sura yake lakini hakumjua kwani hakuwahi kumuona mahali popote. 
Yule mzee mwingine naye alifungua kitambaa chake usoni na sura yake ilipata kuonekana vyema,, Mchungaji Joshua alishituka sana kumuona. Naye hakuwa mwingine bali niiiiiiiiiiiiii....Baba mzazi wa Mama David(Fabiana),, mzee Jangalaaaaaa!!!!!!



👉NINI KITAENDELEA HAPA???

MTOTO YUKO WAPI???

      BAKI HAPA HAPA KWENYE APP YETU, MUITE NA MWENZAKO.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: BINAMU 🔞 SEHEMU YA 11

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 1-5

CHOMBEZO: MASSAGE ROOM🔞 SEHEMU YA 21