MCHUNGAJI MCHAWI, EPISODE:09
Story: MCHUNGAJI MCHAWI.
Mtunzi: Nellove
Episode: 09
Ilipoishia...
"Binti tunaomba Jibu lako tafadhali. Ulimuona wapi huyu?"
"Huyu nimemuona juzi njiani na ndiye aliyenibaka" alijibu binti Glory
Endelea...
Moyo wa mchungaji Joshua ulisinyaa kutokana na kile kilichopenya kwenye ngoma za masikio yake. Hakuamini kabisa kile alichokisikia kutoka kwa binti yule mdogo,,, Kitete kiliikamata miguu yake na kila kiungo cha mwili wake huku kigugumizi nacho kikizuia sauti ya utetezi kutoka ndani yake. Ndugu na Jamaa waliokuwa upande wa mchungaji Joshua hawakuamini kile walichosikia na hawakuwaza kama mchungaji anaweza kufanya jambo kama hilo. Hakika ilikuwa ngumu kuamini.
"Binti una uhakika ndiye huyu aliyehusika???" Lilikuwa swali la hakimu. Hapakuwa na jibu lolote kutoka kwa binti yule aliyekuwa analia ndani ya muda wote huo.
"Tuthibitishie hili kabla mahakama haijatoa maamuzi yake" alirudia kuzungumza hakimu.
"Binti ameshasema sasa ni uthibitisho gani tena unahitajika??? Afungwee huyuu" ilikuwa sauti ya mzee Martin aliyeungwa na wazee wengine kadhaa waliokuwepo hapo.
"Hakuna la ziada hapo,, afungweee"
Mchungaji Joshua alitazama kushoto kisha kulia, aliwatazama wale wanaomtetea,, aliuona unyonge ulio ndani yao. Aliwatazama wale wazee na kuona tabasamu lililobeba dharau kubwa,, aliumia.
Alimtazama yule binti Glory
"Eeh MUNGU msamehe kwa sababu halijui atendalo pia naomba usiache kunitetea kwenye hili. Baba wewe ndo unayefahamu ukweli hivyo naomba fanya jambo ili mapenzi yako yakapate kutimizwa" alitamka hayo kisirisiri na kuwa tayari kwa lolote.
Basi baada ya hakimu kuuliza mara kadhaa bila kuwepo mabadiliko yoyote, alijiandaa kutoa tamko la hukumu kwa mchungaji lakini kabla hajafanya hivyo yule binti Glory alipaza sauti kwa nguvu.
"Siyo yeye aliyenibaka"
Watu wote walishituka kusikia hivi,, waligeuka na kumtazama kwa mshangao mkubwa huku miguno ikirindima pale.
"Binti Mbona hueleweki!!!"
"Ndio Siyo yeye aliyenibaka"
"Mwanzo umetamka mwenyewe kwamba huyu ndiye mhusika" "nililazimishwa na Baba kusema hivyo,, aliniambia nikisema tofauti ataniua" binti aliongea huku analia sana.
Wazee walikuwa kimya, sura zimepoa haswaa. Mipango yao ilienda mrama na ghafla kesi iligeuka na kuwa upande wa mzee Martin.
Like ukurasa wetu👇
https://www.facebook.com/Topsoundsimulizi/
Sasa Hatimaye siri imefichuka,, kumbe binti Glory alishinikizwa kumbambikia kesi mchungaji Joshua. Kwanini???
Kumbuka Wachawi wa Tungi mmoja wao akiwa ni mzee Martin (Baba Glory),,, walikuja na wazo litakalommaliza kabisa mchungaji. Ilikuwa mbinu ya kibinadamu zaidi kwa kumtengenezea kesi ya ubakaji. Ni kweli Binti alibakwa lakini alibakwa na mtu mwingine kabisa ambapo hata hivyo ilipangwa abakwe.
Sasa Mchungaji Joshua aliachwa huru na alipata kurudi nyumbani ila afya yake haikuwa nzuri sana kwani kipigo alichopewa hapo awali kilikuwa kikubwa. Hali yake haikuruhusu kukaa pake yake lakini angekaa na nani kumhudumia???
Mzee wa kanisa aliamua kutumia busara kwa kumhitaji Binti Fabiana kuwa karibu na mchungaji hadi pale hali yake itakapotengemaa. Halikuwa tatizo.
Fabiana aliridhia kumhudumia mchungaji Joshua akiwa naye karibu.
Ndani ya wiki moja alipona kabisa ndipo alipoamua kurudi kanisani kama ilivyo ada. Alisonga mbele na watu wake wachache huku kila mara akimlilia MUNGU wake kumpa mke mwema wa kuishi naye ndipo Ilipokuwa siku moja usiku alipopata ndoto fulani,, aliota yuko mahali fulani akisikia sauti tu ikimwambia sasa ni muda wa kupata msaidizi wake,, naye si mwingine bali ni binti Fabiana. Hakutaka kupoteza muda katika hili,, alizungumza na mzee wa kanisa na kumueleza maono haya.
MWANZO WA BALAA JIPYA KWA MCHUNGAJI JOSHUA.
Maisha yalisonga na ama kwa hakika Fabiana alichaguliwa kuwa msaidizi wa mchungaji kwani sasa mambo mengi yaliyokuwa yanakwama kipindi cha nyuma yalianza kwenda bila wasiwasi wowote,,, Fabiana alikuwa mtoa mawazo na mshauri mzuri sana wa mchungaji Joshua. Sifa ya mke mwema ilithibitika vyema kwa Fabiana,, mchungaji Joshua alimpenda sana sana mke wake.
Mchungaji Joshua pamoja na mke wake wakishirikiana na mzee wa kanisa, waliendelea kufanya kazi ya Mungu na kuhakikisha wanairudisha tena imani ya watu wao. Na hakika Mungu ni mwaminifu,, watu walianza kujaa tena kanisani kila siku za ibada.
"Mimi naitwa Glory Martin. Nimesimama hapa mbele kuyasema haya na kuomba msamaha kwa mchungaji pamoja na Mungu kwa kukubali ule mpango wa kumsingizia mchungaji,, naomba msamaha sana" aliongea binti Glory siku moja alipoenda kanisani kwa mchungaji Joshua.
Alijutia kosa kutoka ndani ya moyo wake na sasa aliamua kujitoa kumtumikia Mungu na kuhakikisha ndugu, jamaa na marafiki zake wanaambatana naye katika kazi ya Mungu. Watu waliongezeka kanisani.
Hili lilikuwa pigo kwa wachawi wale waliokosa kujua namna ya kufanya ili kumshusha mpinzani wao. Kiukweli wachawi waliishiwa kabisa yaani hawakuwa na jipya lolote.
Moto uliokuwa ndani ya kanisa lake kwa wakati huu ulikuwa mkubwa kuliko kawaida ndio maana basi sifa zilivuma pande nyingi kwamba ni tatizo gani halitapatiwa ufumbuzi kwa mchungaji Joshua??? Kila aliyeombewa alipona. Jina la mchungaji Joshua lilivuma na kusikika kila kona ya mkoa hata nje ya mkoa wa Morogoro. Watu waliendelea kukusanyika kanisani kwake wakiponywa kila shida iliyowasumbua.
Miezi mingi ilisonga na hatimaye walifanikiwa kupata mtoto wa kiume waliyemuita kwa jina la David. Furaha iliongezeka maradufu ndani ya familia yake. Waumini walifurahia sana jambo hili na hakika walimpongeza mno kwa zawadi na vitu mbalimbali.
Basi ilikuwa siku moja usiku mtoto akiwa na miezi mitatu,,, wote walikuwa chumbani wamepumzika. Muda fulani Mama David(Fabiana) aliaga kutaka kwenda nje.
Mchungaji Joshua alibaki ndani na mtoto hata Hivyo hazikupita dakika nyingi sana ilisikika sauti
"Mamaaaaaa!!!" Kelele hizi zilisikika kisha sauti kali ya kukoroma ilianza kusikika kutoka sebuleni.
Mchungaji alishituka sana hivyo aliinuka haraka na kukimbia hadi sebuleni ili kujua ni kipi kimetokea.
👉NINI KILITOKEA NA KIPI KITAENDELEA???
ITAENDELEA.......
BAKI HAPA HAPA KWENYE APP YETU, MUITE NA MWENZAKO
Maoni
Chapisha Maoni