MY FIRST DAY, EPISODE:10
MY FIRST DAY
MTUNZI: McLAURIAN
EPSODE: 10
Ilipoishia, nilitoka kuoga bafuni na kisha nikaketi kwenye sofa huku nikianza kuangalia Tv. Mwalimu naye alienda bafuni kuoga huku akiwa anatokwa damu na kuchechemea kwa mbali.
......SONGA NAYO.....
Nikiwa nimekaa kwenye sofa, gafla mkuu naye alitoka bafuni huku akiwa anatembea kwa kama mtu aliyetolewa ngozi yake ya soksi huku akionekana mwenye maumivu makali.
Nilimuonea huruma lakini nami pia nilihisi maumivu japo kwa mbali.
Alifungua taulo lake kisha akajipakaa mafuta na kisha akavaa suruali yake huku akiwa anaivuta polepole ili isiweze kumuumiza.
Baada ya kumaliza kuvaa, aliniambia kuwa kikao kimehairishwa hivo tunatakiwa kuondoka asubuhi kwani shuleni palikuwa mbali sana.
Niliongozana naye, na kisha akakabidhi funguo na kuaga huku akionekana kutokuwa na furaha.
Nilianza kujiuliza kujiuliza maswali juu ya kikao hicho huku nikibaki bila majibu.
Mkuu alifungua gari kisha tukaingia na kuanza safari huku nikiwa tiyari kwenye Uniform.
Mkuu aliendelea kuendesha gari huku akianza kusema kuwa anahisi maumivu makali na kila anapokanyaga moto anajitonesha na kusababisha damu kutoka.
Nilianza kuogopa sana lakini safari iliendelea kama kawaida na hatimaye tukakaribia kufika shule.
Mnamo mda wa saa 12 jioni tuliwasiri shuleni huku mkuu akiwa na maumivu makali sana.
Aliendelea kuendesha gari kuelekea maeneo ya nyumba yake ili aweze kuegesha huku suruali yake ikiwa imelowana damu kwa upande wa mbele.
Nilishuka kisha akanambia nirudi bwenini huku naye akianza kuelekea nyumbani kwake.
Wakati naanza kuelekea bwenini nilisikia sauti kama ya kike fulani, baada ya kugeuka nikaona mwanamke amesimama mlangoni huku mkuu wa shule akiwa anaishilia ndani ya nyumba yake.
Nilipokaribia staff, gafla Mwalimu wa nidhamu aliniita nami nikaamua kwenda kumsikiliza huku nikiwa naogopa mno kwani Mwalimu huyo alikuwa mkali sana.
Baada ya kukutana naye huku nikiwa nimeshikilia mkoba wangu, aliniambia niende ofisini kwake kuna kitu anataka kuongea na mimi.
Nilianza kutetemeka lakini nikapata nguvu kwani mkuu alishaniambia kuwa yeye ndo kila kitu shuleni.
Tulifka ofisini tukakaa kwenye viti na kisha Mwalimu huyo akaanza kuniuliza maswali na kunihoji wapi natokea na kwa nini nilienda bila ruhusa kwani yeye ndiye mtu pekee anayetoa kibari cha mtu kutoka nje shule kwa mda maalumu.
Alikuwa mkali sana na kisha akanilazimisha nipige magoti na akaanza kuniambia kuwa niandike barua ya maelezo yenye kurasa zisizopungua nne na kisha nieleze kwa urefu wapi nilikuwa na kwanini nimeondoka bila ruhusa.
Aliendelea kunitisha na kunambia kuwa kama itabainika kuna kitu chochote nimekifanya lazima anifukuze shule kwa kushirikiana na kamati ya shule.
Nilianza kutokwa machozi na kulia huku nikiwaza kuwa nikifukuzwa shuleni nitaongea nini na pia kwenye barua nitaandika nini.
Nilinyanyuka huku nikiwa kama mtu aliyechanganyikiwa huku mwalimu wa nidhamu akiendelea kutoa sauti ya ukali kama simba mwenye njaa.
Wakati naanza kutoka ofisini huku nikiwa na kibegi changu, aliniita tena na kisha akaniambia nifungue kibegi hicho ili kuona kilichomo.
Nilitaka kukataa lakini nilijikuta nafungua kisha akanambia nimwage chini kila kitu kilichokuwemo.
Baada ya kumwaga chini, Mwalimu huyo wa nidhamu aliona nguo zangu mpya ambazo nilinunuliwa na mkuu wa shule.
Baada ya kuziona, aliinamisha kichwa nakuwa mtu aliyechanganyikiwa huku akiniangalia kama mtu aliyemuibia mke wake. Nikiwa nimesimama nililamba kofi kali sana mpaka kichwa kikaanza kuzunguka.
Aliwaka kwelikweli na kusema kuwa sheria za shule haziruhusu nguo yoyote ya nyumbani kuvaliwa na ni kosa la kufukuzwa shule.
Alizipeleka nje kisha akazimwagia mafuta ya taa kama masihara hivi, zikaunguzwa.
Nilitoa kilio kikali sana mpaka wanafunzi waliokuwa kwa karibu wakawa wanachungulia huku moshi ukiwa unatanda mazingira ya shule.
Alinifukuza na kuniambia kuwa kabla ya saa moja usiku niwe nimeleta barua ya maelezo na ikibainika kuna uvunjifu wa sheria nitafukuzwa shule.
Niliindoka na kisha nikaelekea bwenini ambapo niliwakuta rafiki zangu Upendo na Mariam Wakiwa wamekaa kitandani.
Baada ya kuniona walinishangaa kwa nini ninalia na kisha wakaniuliza wapi nilipokuwa?
Sikuweza kujibu chochote bali kilio tu na kisha nikajilaza kama dakika 5 hivi lakini usingizi ukawa hata hauji.
Nikiwa nimepumzika, nilikumbuka maneno aliyoniambia mkuu kuwa likitokea lolote basi nije nimwambie na yeye atalimaliza kwani ndiye mkuu wa shule.
Niliamka na kisha nikajifuta machozi na kisha nikaenda kumuona mkuu wa shule.
Nilikaribia maeneo ya mkuu wa shule na kutaka kuingia ndani. Niligonga hodi mara mbili lakini nilikuwa nasikia makele ya majibizano kati ya mkuu na sauti ya kike.
Mara mlango ukafunguliwa na mama fulani aliyekuwa na umri wa miaka 40 hivi huku akionekana mwenye hasira.
Alinikaribisha kisha akaegesha mlango tena.
Bwa baada ya kuona hivo nilimuomba kuonana na mkuu aliyekuwa amejilaza kwa maumivu makali.
Mkuu aliuliza kuna anayemuhitaji nami nikataja jina langu, baada ya kusikia hivo mkuu alijifanya kama hanijui na kuuliza kuwa nina shida gani?.
Aisee nilijikuta machozi yanazidi kunitoka huku mda alioniambia mwalimu wa nidhamu ukiwa unakaribia.
Nikiwa bado ninajishauri gafla mama yule akatoka huku akiwa na fimbo kubwa na kutaka kuniburuza nayo mgongoni.
Nilifungua mlango kwa kasi lakini fimbo ilifanikiwa kunipata kisogoni na kunikwaruza kidogo japo sikupata maumivu sana.
Nikitimka mbio kali sana huku nikijiuliza kuwa hapa mambo yatakuwa yametibuka na huenda mkuu alinidanganya kuhusu kutokuwa na mke kwa sasa.
Nilipogeuka nilimuona huyo mama akitaka kurusha jiwe na kunifanya niongeze speed kali sana.
Nikiwa nakimbia kwa mbele yangu nilimuona Baraka akiwa na wasichana kama watatu hivi wakiwa wameshikilia vitabu nami nikajikuta ninajikwaa nakudondoka chini.
Niliumia sehemu za magoti na kiwiko kisha nikaanza kutokwa na damu.
Baada ya dakika kama 5 hivi akina Baraka walifika na kuniangalia huku wakiwa na mshangao ya kipi kinanikimbiza kiasi hicho cha kunifanya mpaka ninajikwaa hivo.
Sikuweza kujibu chichote badala yake niliongeza kilio cha maumivu huku nikiwaza mda wa kupeleka barua kwa mwalimu wa nidhamu.
Wasichana wale waliokuwa na Baraka walianza kumwambia Baraka waondoke kwani wameshachelewa kwenda kudiscuss lakini Baraka aliwambia watangulie kama dakika 5 hivi anakuja.
Nilipandwa na hasira mara 2 mara baada ya kusikia wasichana hao wanatoa kauli kama ile.
Nilijipangusa vumbi na kisha nikamwambia Baraka aniache kwani sikuwa vuzuri na nisingeliweza kujibu chochote.
Nilirudi bwenini na kisha kutaka kuanza kuandika barua kwani mda ulikuwa umebaki dakika 40 .
Nilipoanza kuandika, nilijikuta naandika mistari minne tu na kisha nikakoswa cha kuandika.
Nilikosa namna na kuamua kumuona Mwalimu wa nidhamu na kisha nimwambie kila kitu na kama ataweza kunisaidia basi anisaidie.
Nilijipanga na kisha nikaanza kuelekea nyumbani kwa mwalimu wa nidhamu ili nikamuombe msamaha....
NINI KITAJIRI?.....
ITAENDELEA....
BAKI HAPA HAPA KWENYE APP YETU, MUITE NA MWENZAKO
Maoni
Chapisha Maoni