BALAA LA PENZI LA JINI PART:04



BALAA LA PENZI LA JINI


PART: 04

Ilipoishia, "Ebu nipe niongee naye kama anakudai basi hiyo elfu 30 nitailipa mda huu ili asiendelee kukusumbua my baby" Zayna alimwambia Dicky.

"Hapana wala haina shida nitamlipa mwenyewe ila sio leo wala kesho" Dicky alimwambia Zayna.

"Hapana, naomba simu hiyo mara moja ili nimlipe hela yake maana ni haki yake na aliitolea jasho lake hivo anastahili kulipwa mara moja" zayna aliingiza mkono kwenye suruali ya Dicky iliyokuwa pembeni kidogo kisha akaanza kuitoa taratibu kwani suruali ilikuwa imejikunja sana.

Wakati anamalizia kuitoa, simu iliita tena kwa mara ya 3 ndipo Dicky alivyoamua kutimua mbio huku akiwa mtupu na kumuacha Zayna akiwa anacheka na kushangaa ...

SONGA NAYO...

Zayna alipokea simu hiyo kwa makini kabisa huku akikaa kimya bila kuongea chochote kile, alikunja uso wake , hasira zikampanda kama mwanafunzi aliyefeli mtihani wakati hakuwahi kuwa mtoro hata siku moja.

Aliweka simu hiyo sikioni mwake huku.akiwa ametoa macho kwelikweli kisha akasema ,

"Wewe ni nani unayeongea na mme wangu usiku huu?" Alimuuliza.

",Hee! Mme wako yupi! Huyu ni mme wangu tena nimefunga naye ndoa sasa nashangaa kuona unaniambia hivi"

"Kama ni mme wako sasa hii simu nimeitoa wapi? na mda huu unaye hapo?" Zayna alimuuliza..

"Hapana ameniaga kuwa anatoka kidogo lakini mpaka mda huu hajarudi.."

"Sasa kuanzia mda huu naomba uelewe kuwa ndo mme wangu na nikiha kukuta naye..utajuta.." Zayna alikatisha mazungumzo kisha akamtizama Dicky lakini hakuweza kumuona.

Bila kuchelewa, Zayna alitoka nduki kumfata Dicky huku kijasho cha hasira kali kikimtoka mwilini mwake.
Baada ya kufika sehenu lilipokuwa gari, alishangaa kutolikuta ndipo wasiwasi ulipomjaa lakini kwa kuwa alikuwa na nguvu ya ajabu basi hakujali kuhusu hilo.

Naye Dicky.., baada ya kufanikiwa kupenya kwenye tundu la sindano, alitimua mbio kali sana kiasi kwamba visigino vya miguu yake viliweza kugusa mgongoni mwake huku akiwa anateleza na kuamka.

Kama bahati hivi, wakati anataka kudondoka chini kwa mara ysa pili, alishika tawi la mti ambalo lilikuwa limedondokea barabarani ndipo jani moja la mti huo lilipodondoka kwenye nywele zake jambo lililomfanya aweze kuona gari yake.

Akiwa amevalia boksa tu, alifungua gari yake kisha akaliwasha na kuanza kuelekea nyumbani kwake maeneo ya mbezi beach.
Wakati anaendesha gari lake hilo, alimanusura alimkosa kumgonga kijana mmoja ambaye alikuwa anavuka barabara maeneo ya mwenge huku walinzi waliokuwa kwa nje wakabaki na mshangao mkubwa.

Dicky aliongeza speed mpaka gari ikawa inarukaruka mpaka hapo alipofika maeneo ya Tegeta ndipo alipojishangaa kuona yupo katika mwendo huo.
Alushusha pumzi kidogo lakini bado akili ilikuwa haijakaa sawa kabisa.

Wakati Dicky anakaribia kufika nyumbani kwake, Zayna alianza kujikuna kichwa na kwa mshangao mkubwa kwani kila alipoangaza macho yake hakuweza kumuona wala kuliona gari lilipo.
Hakuamini kabisa ndipo alipopaa juu kama ndege ili kuweza kuona wapi alipo lakini hakuweza kumuoa .

Taratibu na kwa uchungu mkubwa sana, Zayna alianza kurejea kwenye makazi yake ili aweze kujitafakari wapi Dicky amemzidi mbinu na nini akifanye kwa mda huo.

Alipofika kwenye makazi yake, alizikunja nguo za Dicky kisha akazifunga na kipande cha kitambaa cheupe na kushuka nacho mpaka kaburini.
Anapifika kaburini, Zayna hubadilika na kuwa kiumbe kingine tofauti ambacho hakipumui wala nini.

Kwa kawaida,Zayna hujitojeza mara nne au 5 kwa siku nzima hivo alikuwa bado na mda wa kuamka tena.

Mda uliendelea kutaradadi huku mishale ya radi ikimulika anga zima kwa kuashiria hali ya mvua kali.
Kwenye mida ya saa nane na nusu usiku, mke wa Dicky aitwaye Kaylin ambaye alikuwa anamwaga machozi kwa kile alichoambiwa kwenye simu na bi mdada aitwaye Zayna, alikosa uvumilivu kabisa ndipo alipoamka kitandani kisha akakaa sebukeni na kujaribu kumpigia simu mmewe lakini haikuweza kupatikana.

Kaylin aliangua kilio peke yake kilichoambatana na maombolezo ,

'Mme wangu Dicky..kwanini unanifanyia hivo! Nimekupenda kwa moyo wangu wote teba sijawahi hata kukucheat lakini unafikia hatua mpaka unanizimia simu! Mungu yupo. Kitu gani kwangu umekikosa mme wangu! Kila siku najitoa kwa moyo wangu wote kukuonesha mahaba ya dhati lakini...ila ngoja uje kitaeleweka na mke wako huyo" Zayna aliongea peke yake huku akichuruzisha machozi kama mvua za kiangazi.

Aliwaza na kuwazua mpaka akatamani kufanya maamuzi magumu lakini aliogopa.
Vitambaa vilivyokuwa kwenye sebule, alivishika kwa hasira na kuvitupatupa kama mtu aliyechanganyikiwa.

Haya sasa, wakati kaylin anaendelea kumsubiria mme wake kwa hasira kali, Dicky yeye hatimaye alibakiza mwendo mfinyu mno kufika nyumbani kwake.
Alipunguza speed kisha akaikata kona na kuelekea nyumbani kwake huku zikiwa zimebaki mu
Mita chache hivi mpaka nyumba yake ilikuwa inaonekana kwamacho.
Barabara ya kwenda kwake, ilikuwa mbovu hivo alipita kwa uangalifu mkubwa sana hali iliyopekekea mke wake kuhisi kama kuna mlio wa gari .
Kaylin alisimamisha masikio yake kama panya aliyehisi uwepo wa panya huku macho yakiangaza huku na huko.

Haya sasa, Dicky hatimaye alifika getini kwake huku akiwa .mtupu kabisa na bila kujijua kama yupo mtupu ndipo alipowasha taa iliyofatiwa na mlio wa honi.
Kama haamini hivi, Kaylin alijifunga kanga yake vizuri kisha akaenda kufungua mlango wa geti...

KILICHOENDELEA MI SIJUI...

      BAKI HAPA HAPA KWENYE APP YETU, MUITE NA MWENZAKO

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: BINAMU 🔞 SEHEMU YA 11

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 1-5

CHOMBEZO: MASSAGE ROOM🔞 SEHEMU YA 21