KOFI LA KISOGO SEHEMU YA 8

“KOFI LA KISOGO” Na:Arnold Machavo Mbeya—Tanzania Sehemu ipatayo ya 08 ★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★ ««Ilipokomea... “Kwanini unanikimbia sasa?” Waridi alihoji baada ya kuambiwa ukweli. “Hakuna kitu eti nimefikiria tuu nisogee pembeni,” Zena alimjibu huku akitabasamu. Tabasamu lenye ishara ya kuwa amani ipo kati yao hivyo dada mtu asihofu... TEREMKA NAYO...»» “Sawa hakuna tatizo nashukuru sana kwa msaada wako chei wangu.” “Hahaha eti chei. Hicho kijina chenu na mama nilishakisahau usinikumbushe kabisa hata sikitaki,” Zena aliongea na kusababisha kicheko kwa wote wawili mara baada ya kukumbuka jinsi jina hilo la utani lilivyokuwa likitumika hususani kipindi walipokuwa wadogo. Jioni Hussein aliporejea nyumbani alipokelewa na kitu cha kwanza kwake kilikuwa ni kumuona Hassan wake furaha yake kubwa. Walipotulia Waridi ndiye alikuwa wa kwanza kugusia juu ya kutaka kuondoka kwa Zena. “Haa kwanini sasa? maan...” Hussein aliongea. “Aah aah jamani kaumri kanasogea na yeye,” Waridi alimjibu kwa kumkatis...