ASANTE KWA KUNIFUTA MACHOZI (HISIA ZANGU) SEHEMU YA 13-14
Simulizi: ASANTE KWA KUNIFUTA MACHOZI (HISIA ZANGU)
Mwandishi: JOSEPH SHALUWA
SEHEMU YA 13
Nimejiuliza maswali mengi lakini bado sijapata majibu.
Kweli Lilian umesahau mapema kiasi hicho? Kweli umesahau wema wangu wote? Sasa naanza kuamini kuwa, kumbe hukuwa na mapenzi ya dhati kwangu.
Nimeelewa ni kwanini ulikuwa unaninyima penzi lako. Bila shaka utakuwa umeshatolewa bikra ndio maana hukutaka nijue. Umeniumiza sana. Nahisi harufu ya damu mbichi ndani ya moyo wangu.
Hata hivyo, bado una nafasi ya kutafakari upya. Una muda wa kufikiri na kuamua vinginevyo kama utaona inafaa. Nakupenda sana kutoka ndani ya moyo wangu. Ahsante kwa yote lakini kumbuka sikupaswa kuachwa kwenye maumivu makali kiasi hiki, tena wakati huu wa mwanzoni kabisa wa masomo yangu huku Malaysia.
Moyo wangu unateseka!
Edo.
Kwa hakika Edo hakuweza kuvumilia, muda wote aliokuwa akiandika ujumbe ule, machozi yalikuwa yakimtiririka mashavuni mwake. Haikuwa rahisi kukubaliana na hali ile.
Hakuweza kufanya chochote tena, baada ya kutuma ujumbe ule kwa Lilian, alijitupa kitandani na kuanza kuvuta kumbukumbu za mpenzi wake upya kabisa.
Zilikuwa kumbukumbu za mateso sana. Lilian alikuwa amemtenda katika kiwango kikubwa sana!
***
Lilian aliingia kati. Lucy alikuwa na kazi ya ziada akimshawishi acheze. Kwa aibu akajikuta akicheza. Kwa mbali Pam na rafiki yake Big walikuwa wamekaa wakiendelea kukata kinywaji.
Walikuwa watu wenye fedha zao. Pam alikuwa akisubiri kwa hamu kukutanishwa na Lilian. Hilo ndio lilikuwa lengo lake. Usiku ule alikuwa Klabu Maisha kwa lengo moja tu, kukutana na Lilian.
Hiyo ilikuwa kazi maalumu aliyopewa Lucy aikamilishe. Latifa alikuwa beneti na Leila. Tayari alishamshawishi na kuonja mvinyo kidogo iliyomchangamsha!
Ni Lilian pekee ambaye alikuwa hajaonja kilevi mpaka muda ule. Lilian alivyozoea kucheza pale kwenye sehemu maalumu ya kucheza, Lucy alichepuka kidogo.
Hapo akamwonyesha Pam ishara na kwenda kuketi naye sehemu nyingine ambayo Lilian hakuwaona.
?Vipi mama lao?? akasema Pam akicheka.
?Poa baba lao!?
?Nataka kujua ulipofikia. Mambo yanakwenda vizuri?? akauliza Pam akionyesha wasiwasi kidogo.
?Usiwe na shaka baba, mambo yanaendelea. Hatua ya kwanza imeshafanyika. Si unamuona mrembo ndani ya nyumba? Kilichobaki hapa ni kuwakutanisha tu!?
?Utafanyaje sasa??
?Hapa ndio nawaza, lakini nadhani nimpe pombe akilewa, wewe unamaliza!? akashauri Lucy.
?Hapana Lucy. Kumbuka mimi simhitaji huyo msichana kwa siku moja. Nahitaji aendelee kuwa wangu. Kumnywesha pombe halafu ndipo niondoke naye najua hatafurahia.
?Unaweza kuwa mwisho wa uhusiano wetu. Kwanini nisitumie njia za kistaarabu? Kitu pekee unachotakiwa kufanya ni kunikutanisha naye tu. Mambo mengine niachie mwenyewe.?
?Kweli Pam??
?Kabisa.?
Lucy akarudi kuungana na akina Lilian kuendelea kucheza. Muziki ulikolea kwelikweli. Baadaye wakaamua kupumzika kidogo kwenye viti vyao.
Hapo Lucy akatoa wazo la kwenda kukaa na marafiki zake. Hakuna aliyejua hao marafiki ni akina nani isipokuwa Latifa tu. Wote wakakubali. Wakasimama na kuwafuata Pam na Big.
?Pam kutana na marafiki zangu, Leila, Latifa na Lilian,? akasema Lucy haraka kisha akawageukia rafiki zake na kuwaambia:
?Huyu ni rafiki yangu, anaitwa Pam!?
πππππππππππππππ
SEHEMU YA 14
?Nashukuru kuwafahamu, warembo sana.?
Wakacheka!
?Huyu hapa ni rafiki yangu mkubwa hapa mjini, mfanyabiashara mwenzangu, anaitwa Big!?
?Tumefurahi sana kukutana nanyi,? Latifa akajibu akijifanya haw afahamu.
Ukweli ni kwamba Latifa aliwafahamu wote. Vinywaji viliendelea, Leila akiwa ameshazidi kuchangamka. Lilian alikuwa kimya akitumia juisi ya matunda muda wote.
?Kwanini unakunywa juisi muda wote? Nafikiri ungekunywa wine kidogo ili uchangamshe mwili. Siyo kali, ni laini kabisa,? Pam akamwambia Lilian.
?Mh! Naogopa mwaya,? akasema Lilian akionekana kujawa na haya.
?Huna sababu ya kuogopa, ni nzuri. Tafadhali jitahidi unywe hata glasi moja tu!? akazidi kushauri.
?Kweli kaka Pam? Unaniahidi siyo mbaya??
?Acha ushamba bwana, kama ingekuwa inalewesha mimi ningekuwaje? Mbona nimekunywa muda wote na bado nipo poa,? sasa Leila alidakia.
?Haya bwana, ngoja nijaribu!? akajibu Lilian baada ya kupata ujasiri kutoka kwa rafiki yake Leila.
Bila kupoteza muda, Pam akachukua glasi mezani na kummiminia Lilian kisha akamkabidhi.
?Karibu ufurahie matunda ya mzabibu!? akasema Pam akijilamba midomo, tabasamu aliliachia.
Lilian akapokea akizidi kuonyesha aibu waziwazi. Akapiga funda moja kubwa. Akakunja uso kidogo kutokana na uchungu kiasi aliohisi kutoka katika mvinyo ule.
Maskini, hakujua hatari iliyokuwa mbele yake!
Pam alitabasamu! Lilikuwa tabasamu pana ambalo halikujificha kabisa. Alikuwa na haki ya kutabasamu maana alikuwa na uhakika kuwa kazi yake sasa ilikuwa ikielekea kuwa nyepesi kuliko kawaida.
Uso wa Lilian ulikunjika sawasawa. Kwa tabu akameza funda moja kubwa la mvinyo. Ikaingia kooni taratibu kabisa! Akatikisa kichwa kwa nguvu!
?Mh! Nitaweza kweli?? akasema Lilian.
?No! No! No! Utaweza. Sikia... hutakiwi kunywa nusunusu, kwakuwa ni mara yako ya kwanza unatakiwa kumaliza hiyo glasi yote kwanza, halafu kutokea hapo ndiyo utaanza kuzoea.?
?Paaaam!? Lilian akasema akimwangalia Pam machoni.
?Yes! Ndiyo ukweli kama unahitaji kuzoea. Siyo chungu sana bwana!?
?Ngoja nijaribu.?
Lilian akanyoosha mkono wake kisha akachukua glasi na kuipeleka kinywani mwake. Aliigika ile mvinyo yote. Aliposhusha glasi ilikuwa tupu kabisa.
?Mnawezaje lakini?? Lilian akauliza.
?Acha hizo bwana, endelea kufurahi,? Leila akasema akionekana tayari ameshalemewa na mzigo mzito kichwani.
Haraka Pam akachukua chupa yenye mvinyo kisha akaijaza tena ile glasi ya Lilian. Akamwangalia kwa jicho la kumkaribisha kisha akarudisha macho yake kwa Lucy.
Wakatabasamu!
Kuna nini tena?
Kazi nyepesi kiasi gani?
?Karibu mama, endelea kufurahi,? akasema Pam.
Sasa Lilian akaichukua tena ile glasi, huku akionekana kuwa na uzoefu kidogo. Alikunywa kidogo, kisha akarudisha glasi mezani.
?Kweli sasa umekua mtoto wa mjini, na wewe inaonekana utazoea mapema sana!? akasema Lucy.
?Kweli wewe una akili sana. Umegundua hilo kama mimi??
?Yeah, ndicho ninachokiona kwa Lilian,? akasema Latifa.
Kweli Lilian alionekana kuchangamka sana, glasi moja na nusu aliyokunywa tayari ilionekana kumbadilisha kabisa. Uchangamfu wake ukaongezeka ghafla. Hakuna ambaye hakujua kilichotokea.
Ilikuwa tabasamu la pombe!
Palepale Lucy akamwonyesha ishara Pam wasogee pembeni kwa ajili ya mazungumzo. Alianza Lucy kuondoka kisha akafuata Pam, wote wakisema kuwa wanakwenda msalani.
?Nipe chang u,? akasema Lucy akitabasamu.
?Usijali, haina shida. Pesa yako utapata.?
ITAENDELEA........
TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.
Maoni
Chapisha Maoni