KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 6



RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.

MTUNZI : ALEX KILEO.

SEHEMU YA SITA.

_______________
ILIPOISHIA..
________________
Omari alipotoka msalani akawa
anaelekea nje kuwafuata wenzake,
ndipo mbele yake akawaona Askari
wapatao watano wakiwa wanaelekea
upande aliopo huku wameongozana
na msichana ambae hakuweza
kumtambua kutokana na umbali
ulikuwa kati yao, ila kadri walivyozidi
kusogeleana ndipo sura ya yule
msichana ilivyozidi kumjia, zilipofika
hatua mbili kabla hawajapishana
ndipo Omary alipopata mshtuko
baada ya kugundua kuwa yule
msichana ni Mhudumu wa ile bar
ambayo Kayoza alifanya mauaji.

Omary aliuficha mshtuko wake ila
sasa yule Mhudumu akawa
anamuangalia sana Omary, Omary
akatamani hata apotee gha fla kama
upepo ila i l ishindikana na akaamua
aendelee tú kwenda mbele kiume.

Wale Askari na mhudumu
walipomfikia Omary wakampita na
kufanya Omary ashukuru Mungu
baada ya kupishana nao.
Yule Mhudumu alipompita Omary,
alihisi hiyo sura siyo ngeni kwake,
alitembea hatua mbili kisha
akasimama, ikabidi Askari wote nao
wasimame, kisha Mhudumu akageuka
na kumtupia jicho Omary ambaye
nae aliwageukia na sura yake
ikaonekana vizuri na Mhudumu na
kumfanya Mhudumu atoe mguno wa
mshtuko..

____________
ENDELEA..
____________

Omari akaona akijifanya kukimbia atakuwa amejikamatisha, akajifanya hana habari nao na kuendelea kutembea kuelekea nje, tena ukizingatia wale polisi walivaa kiraia basi hata wasiwasi kwa Omary haukuwa mkubwa.

Mhudumu akiwa na
hakika asilimia 95 kwa kile anachokiamini, aliendelea kumuangalia Omary aliyekuwa anatembea na kuzidi kuwaacha,

"Wewe dada vipi?" Sajenti Minja aliuliza huku akimuangalia Mhudumu,

"yule ni mmoja kati ya
watu waliongia guest kwetu na wale wasichana waliokufa" Mhudumu alijibu huku akimuelekezea kidole Omary, Polisi bila
kupoteza muda wakamuita Omary aliyekuwa tayari yuko mbali nao, ila sijui ni kutokana na uoga au kujiamini, Omary alijikuta akirudi mpaka Pale alipo yule Dada Mhudumu na Askari,

"mambo vipi kaka", sajenti minja
akamsalimia omari,

"poa", omari
akajibu huku wasiwasi ukianza kuchukua nafasi,

"sisi ni askari, je unamjua huyu
binti?" Sajenti Minja alijitambulisha na kisha akauliza swali huku akinyooshea kidole
mhudumu.

kiukweli Omary alishtuka
ila hakutaka kuunyesha mshtuko wake, ila tayari askari walishaligundua hilo kitambo.

"simjui, kwani vipi?" Omary akajibu kwa pupa,

"Dada unamjua huyu?" Sajenti Minja alimuuliza Dada Mhudumu huku akimuangalia Omary,

"Ndiyo namjua" Dada Mhudumu alijibu na kumfanya Omary ahisi tumbo likimvuruga,

"Unamjua kama nani?" Sajenti Minja alimuuliza tena,

"Huyu ni mmoja kati ya wale vijana waliokodi chumba na wale wasichana wa chuo waliouwawa" Dada Mhudumu alijibu,

"Wewe dada utakuwa sio mzima wewe" Omary alijikuta anaongea huku amemtolea macho yule dada Mhudumu,

"mkamateni mumfunge pingu, atajieleza zaidi
kituoni" Sajenti Minja akatoa amri.

Omari ujanja mfukoni, akachukuliwa
mpaka kwenye land cruiser ya polisi iliyokuwa imeegeshwa nje.

Ile gari ya polisi ikatoka
eneo la hospital kwa spidi ya ajabu utasema imempakia jambazi sugu.

* * * * * * * *

Baada ya shughuli ya kuaga miili kuisha, uongozi wa chuo
ukatoa risala fupi kuhusu marehemu
na shukrani kwa wanafunzi waliofika
kuaga wenzao, pia uongozi wa chuo
ukachukua mda huo kuwatangazia
wanafunzi likizo ya mwisho wa
semister.

Kayoza na Denis baada ya
kutawanyika eneo lile, wakaenda moja kwa moja nje
ya hospitali.

"mchizi kaenda kukojoa
kamba nini? Mkojo gani nusu saa?" Denis aliuliza huku akiangalia saa yake ya mkononi,

"simu yangu haina
kitu, kama una salio muendee
hewani" kayoza alimueleza mwenzake.

Denis akachukua simu yake akapiga namba ya Omary, lakini
simu iliita muda mrefu bila kupokelewa, akarudia tena na tena lakini hali ilikua ile ile.

"mpotezee, si unajua leo siku ya kufunga shule,
labda yuko na demu" Kayoza akasema.

"poa, nini kinafuata sasa?" Denis akauliza,

"twende chuo tukachukue mabegi, leo tulale mjini" Kayoza akatoa
maoni yake,

"haina mbaya, ni wazo zuri" Denis
alijibu kwa kumuunga mkono mwenzake na kisha wakaenda kutafuta usafiri uliowafikisha chuo.

Walipofika chuo baada ya
kuoga na kujitayarisha kuondoka, Denis akarudia tena kupiga simu ya
Omari, safari hii alipiga mara moja tu na simu ikapokolewa

"wewe dogo vipi
napiga simu muda mrefu haupokei, uko
wapi?" Denis akaongea kwa pupa,

"samahani mwenye simu yuko Polisi, hapa ni kituo kikuu cha Polisi dodoma
mjini" upande wa pili ukajibu,

"Polisi?, amefanya nini tena?" Denis
akauliza,

"wewe ni nani yake kwani?" ule upande wa pili badala ya kujibu, wakaongeza swali.

Denis kichwa kikafanya kazi haraka, akahisi akijibu hovyo hovyo bila kufikiria, anaweza akajiingiza matatizoni,

"mimi ni kaka yake" Denis alijibu,

"Sawa, mdogo wako anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuua wasichana wawili akishirikiana na wenzake ambao nao bado
wanatafutwa" upande wa pili ukatoa
maelezo,

"Sawa, nipe dakika kumi nitakuja hapo" Denis
akamalizia kisha akakata simu na kuanza kupumua kwa nguvu,

"kaka kumeshaharibika, beba mabegi tuondoke" Denis alimwambia kayoza,
"Sikuelewi, ebu nyoosha maelezo" Kayoza aliongea huku akimuangalia kwa makini Denis,

"Omary amekamatwa na Polisi kwa tuhuma za mauaji ya pale guest" Denis alimjibu Kayoza,

"Mimi si niliwaambia hapa sio pa kukaa tena?" Kayoza aliuliza huku hiyo habari ikionekana kumgusa,

"Hakuna muda wa kubishana hapa" Denis aliongea kwa ukali kisha wakabeba mabegi yao haraka, safari ya
kwenda mjini ikaanza.

* * * * *

Omari baada ya kuchukuliwa na
polisi, alifkishwa kituoni kwa ajili ya mahojiano hawali. 

"unaitwa Omary Said
Mkwiju, si ndio hivyo?" Sajenti Minja alikuwa anamuuliza Omary huku
kashuka kitambulisho cha Omary,

"ndio" Omary akajibu.

"sisi hatuna ubaya na wewe, ila ukweli wako ndiyo
utaokusaidia" Sajenti Minja alianza kwa mtindo huo, kisha akaendelea, 

"mlikua watatu,
wenzako wako wapi mlioshirikiana
nao katika mauaji?"

"jaman mimi sijaua,
huyu dada kanifananisha" Omary alijitetea huku macho yakiwa makavu, 

"mchukueni mmuweke
ndani, naona hayuko tayari kutoa ushirikiano" Sajenti Minja alitoa amri.

Omary akabebwa juu juu akapelekwa
Selo ingawa aliendelea kulalamika anaonewa kwani yeye hajui chochote kuhusu vifo vya hao wasichana. 

"Kwanini asipelekwe magereza kabisa" Askari mmoja aliuliza,

"Muacheni huku kwanza, nitamrudia usiku" Sajenti Minja alijibu huku akichukua koti lake la suti alilokuwa amelitundika ukutani, na kisha aliondoka.

Usiku Sajenti Minja alirudi
tena, akaongea na askari wa zamu, kisha Omary akatolewa nje, akavuliwa
nguo zote, kisha akaanza kuhojiwa tena, ila bado alikua mbishi,
wakaitwa watu wanne waliokuwa wameshiba
haswa, ni mijibaba ya miraba minne,
wakaamrishwa wamchape.

walimchapa haswa. Hadi akalainika, akawataja wenzake. Mda huo huo wa usiku Sajenti Minja akamfundisha
Omari jinsi ya kuongea na simu, kisha akawapgia wakina wakina
kayoza. 

"oya mko wapi wana?" Omary alianza kuongea
hivyo, 

"vipi, wewe si uko polisi?" Kayoza
aliuliza huku akishangaa mwenyewe, 

"ni habari ndefu ila
wameniachia, wamedai
wamenifananisha, wamenipa hela
kwa ajili usumbufu" Omary alijibu huku akishusha pumzi ndefu,

"ehe siku hizi polisi wanatoa hela!?, aya
upo wapi?" Kayoza aliuliza,

"Mi niko guest moja hivi karibu na Railway,
nimeona giza limeshaingia nikaona bora nipumzike tu kwa maana polisi wamenisumbua sana. Nyie mko
wapi?" Omari aliuliza,

"tupe ramani tukufuate hapo ulipo kwa maana hata mabegi yako ya nguo tumekubebea" Kayoza alimwambia Omary,

"Chukuenu bajaji, mwambieni awapeleke kilimani lodge, mtanikuta hapo" Omary aliongea huku Sajenti Minja akiwa pembeni akimfundisha maneno ya kuongea na kisha akakata simu.

Baada ya mtego wa Sajenti Minja kukamilika na kufanikiwa kwa
asilimia nyingi, akachukua taxi, kwa maana aliogopa kwenda na gari ya polisi kwa kuwa endapo wakina kayoza wataiona kipindi wamawasili, basi wanaweza kukimbia.

Sajenti Minja alichukua taxi na askari watatu wenye bunduki, wakafunga safari hadi eneo walilopanga kukutana na wakina Kayoza, akachukua chumba,
kisha wakamuingza omari na askari wote watatu wakaingia chumbani kwa ajili ya kuwakamata wakina Kayoza pindi watakapofika, kisha Sajenti Minja yeye alirudi
nje kakaa ndani ya ile taxi na Dereva, huku akifuatilia kila kinachoendelea nje.

Wakina kayoza walipofika Kilimani lodge, wakampigia simu Omary,

"Tumefika, tupo nje hapa" Denis aliongea baada ya Omary kupokea simu,

"njoon chumba namba
7" Omary akawaambia wenzake ambao walimlipa dereva wa bajaji pesa waliyokubaliana nae, kisha wakabeba mabegi yao na kuelekea ndani.

Sajenti Minja hakuwa na wasiwasi na vijana wake,
aliona jinsi wakina Kayoza
wanavyopiga simu na aliwasikia pia wanachoongea na Omary,
ila hakua na pupa, aliamini wakina Kayoza wanaenda kukamatwa na vijana wake aliowaweka chumbani pamoja na Omary, kwa hiyo akaacha vijana wake wafanye kazi. 

Denis na Kayoza
walipofika mlango namba 7, wakagonga mlango, na Omary akafungua,

"Karibuni ndani, ingieni" Omary aliongea huku akiwa amechangamka na wakina Kayoza wakaingia ndani bila kujua katika hicho chumba walichoingia,wapo Askari watatu wenye bunduki wakiwasubiri wao.....

******ITAENDELEA******


TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: BINAMU 🔞 SEHEMU YA 11

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 1-5

CHOMBEZO: MASSAGE ROOM🔞 SEHEMU YA 21