MCHUNGAJI MCHAWI EPISODE:25




Story: MCHUNGAJI MCHAWI

Mtunzi: Nellove 😎

Episode: 25

Ilipoishia...

Waganga walishindwa kumpindua, wachawi wenzake hawakumfikia na hata baadhi ya wachungaji waliishia kwenye udongo mara tu walipoamua kupambana naye, hata hivyo habari za ujio wa mchungaji Joshua kutoka Morogoro alizipata na siku hiyo alishuhudia watu wakichomolewa mapepo na uchawi aliopanda ndani ya watu hao,,, alishuhudia hayo kwani naye alikuwa katikati ya umati ule kwa lengo maalumu.

Mzee Shirima alianza kumjaribu jaribu Mchungaji Joshua.

Songa nayo...

Mchungaji alipata kuhisi uwepo wa jaribu kutoka kwa mtu mbaya lakini hakutaka kushughulika naye sana,,, aliendelea na shughuli ya kiroho.

Hata hivyo utofauti mkubwa ulipata kudhihirika,, Mzee Shirima aliona moto uliosababisha ugumu katika jaribio lake. Hii ilikuwa tofauti na wachungaji wengine kwani pindi alipowajaribu tu alifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana.

Ile nguvu aliyotuma kumjaribu mchungaji Joshua aliishuhudia ikiteketea na kuyeyuka ndipo aliona ni heri aweke majeshi yake sawa sawa ili kumfunza adabu huyu anayechokoza himaya yake,,, aliondoka pale.

Mkutano uliendelea huku lengo likitimia, watu wengi waliguswa na kuponywa matatizo na shida zao mbalimbali. Wengi walikuwa na mapepo na uchawi uliopandwa kutokana na kulishwa vitu vichafu usiku.

Hii siku watu walifunguliwa huku hivyo vitu vichafu vikitoka kwa njia ya kutapika.
"Wewe uliyefika katikati ya mkutano huu, kutana na mkono wa Bwana. Huo uchawiiiii utokeeeee kwa jina la Yesuu!!!." Ilikuwa sauti kuu kutoka kwa mchungaji Joshua.

Uponyaji uliendelea kwa nguvu isiyo ya kawaida. Ukiacha wale waliopandikizwa uchawi pia walikuwepo viwete wengi ambao walikutana na nguvu ile iliyoenda kuwaponya moja kwa moja na kubadilisha historia ya maisha yao.

"Leo ni ufunguzi na yote mliyoyaona ni mwanzo tu. Yapo mengi ya ajabu mtaenda kuyashuhudia kwani Mungu wetu ni mwenye mamlaka kuliko chochote. Wape salamu wachawi" Alisema maneno hayo baada ya kumaliza huduma ya uponyaji kwa siku hiyo ya Jumatano.

Nyimbo za taratibu zilisikika huku watu wakianza kutawanyika.

"Nyie Mungu ni muweza, ujue nimepona kabisa"
"Mimi hata sijui niseme nini, huu mgongo umekuwa mpya kabisa" walikuwa wanazungumza wamama fulani waliokuwa katikati ya mkusanyiko huo. Kila mmoja alizungumza lake kuhusianisha na alichokutana nacho.

Muda wa nusu saa ulitosha kabisa kwa umati ule mkubwa kutoweka mahali pale. Waliosalia walikuwa ni wahudumu wa mchungaji Joshua pamoja na walinzi. Mchungaji Joshua na mke wake tayari waliondoka kuelekea kwa Mchungaji Christopher ambaye aliwapokea kwake huko Arusha.

                    †

Mzee Shirima baada ya kutoka kwenye mkutano ule alirudi moja kwa moja hadi nyumbani ambako alikuwa akiishi peke yake.
Hakuwa na mke wala watoto japo katika historia yake ameitwa mume wa jumla ya wake watano. 

Mke wa kwanza alipokuwa na ujauzito alimfanya kafara kwa kuanza kumuua mtoto aliye tumboni na kupelekea kifo cha Mama. Alioa Mke wa pili ambaye naye alitolewa kafara huku kifo chake kikifuata baada ya ugonjwa wa ajabu ambao haukutibika.

Mke wa tatu yeye alikufa kwa kafara ya kuchinjwa kama kuku wakati huo mke wa nne na wa tano walikimbia ndoa ila walikokimbilia walikutana na vifo vya ajabu.

Huyu mzee Shirima aliishi pekee kwa kutazama kwa macho ya nyama ila kiuhalisia hakuwa pekee kwani ndani mwake palijaa misukule iliyohifadhiwa katika chumba maalum kwa maswala yake mbalimbali.

Ujio wa Mchungaji ulimtia hasira sana na katika hili hakutaka mchezo ndipo sasa baada ya kufanya mchakato wa kula basi majira ya jioni aliingia kunako chumba chake hicho. Alivaa kaniki na kujifunika sanda kisha alikaa kitako huku macho yake akiyaelekeza kwenye kibuyu kilichokuwa kinafuka moshi. Hiki kibuyu kilikuwa mbele yake.

"aaannnmmm! mkuu wa kuzimu, nijaalie nguvu ya vita" alizungumza hayo baada ya ukimya wa dakika chache.
"Vita ya kumpiga mwanaharamu mwenye kutaka kuharibu himaya yako." Alitulia kidogo huku akitikisa tikisa kichwa chake taratibu.

"Ulinipa kazi hii na nimeifanya kwa moyo wote. Bila nguvu kutoka kwako hii kazi uliyonipa isingefanikiwa na haitafanikiwa. Nipe nguvu ya vita mfalme" alizungumza na kuinama kwa namna ya kusujudu,, alifanya hivyo mara tatu kisha alikaa kitako.

Ukimya uliotawala kwa dakika tano ulitoweka baada ya upepo mkali kuanza kuvuma ndani ya chumba kile bila madhara. Baada ya hapo msukule mmoja uliokuwa na kitu mkononi mwake ulitokea na kuanza kupiga hatua taratibu kuelekea alipokaa mzee Shirima.

Ule mkono ulioshika kitu ulitua kichwani kwa mzee huyo na kuruhusu kitu kile chekundu kuingia ndani ya mzee Shirima kichawi.
"Hhuuuu aaaaaarrrrrrhhhh!!!!" Aliunguruma mzee huyo baada ya kuhisi nguvu kali ikijaa ndani yake. 
Achilia mbali nguvu iliyoingia pia iliingia namna ama hali iliyochokoza hasira na uchungu mkali baada ya kuona kazi zake zinateketea ikiwemo ule uchawi aliopanda ndani ya watu.

Baada ya yote hayo alisimama kwa hasira na kuwa kama simba ama chui aliyejeruhiwa vibaya.
Sasa vita ilikuwa karibu kuanza kwani uwanja ulikuwa tayari,, kitu pekee kilichokuwa kinasubiriwa ni muda tu. Mzee Shirima aliona saa sita iko mbali sana.                    

Hatimaye muda muafaka ulifika,, ilikuwa saa sita usiku na bila kupoteza sekunde mzee Shirima alitoka nje ya nyumba yake na kunyoosha mikono juu.
Kilikuwa kitendo cha sekunde kadhaa tu ndipo alitokea mnyama aina ya farasi mweupe akiwa na mbawa.

Mzee Shirima alimpanda mnyama huyo, safari ilianza akielea angani hadi mahali ramani yake ya kichawi ilipomuonesha kuwa ndipo alipokuwa adui yake. 
Akiwa kule kule juu angani aliona moto mkali ukizunguka nyumba ile,, hakuhofia chochote hivyo taratibu alianza kushuka ila kadri alivyoshuka na kuwa karibu, nguvu ya moto ilizidi.

                      †

Siku zote za nyuma hata mara baada ya kumaliza huduma ya mkutano wa siku hiyo Mchungaji Joshua alikuwa akijiuliza maswali mazito juu ya jeraha lillilopo kwenye paji la uso la mfalme wa kuzimu pamoja na swali kwanini mkutano wa injili uhitajike haraka iwezekanavyo!!!? Hakuweza kupata majibu ila aliamini atafahamu kwani mfalme wa kuzimu yupo.

Muda ulienda sana ila licha ya uchovu mkubwa aliokuwa nao, hakulala na wala hakuruhusu hata chembe ndogo ya usingizi kumteka. Wengine wote walilala ila yeye Muda wote alikuwa macho akiwaza hili na lile huku ubongo wake ukiruhusu ufikiaji wa kumbukumbu juu ya jaribio alilofanyiwa jioni ya siku ile. 

Ilifika saa sita usiku bado alikuwa macho vilevile na ndio muda alipoanza kuhisi mabadiliko ya mahali pale na kuanza kuona hali inakuwa nzito. Moja kwa moja alitambua uwepo wa nguvu yenye kutaka kushindana naye ndipo sasa aliinuka na kupambana kwa maombi akimuomba mkuu wa kuzimu.

"Ewe mkuu na mfalme wa kuzimu naomba zungushia moto mkali mahali hapa. Unilinde katika vita hii maana umenituma wewe na naamini utafanya wewe"
Alipomaliza kusema haya moto mkali ulizunguka eneo lile japo ile nguvu yenye kushindana naye iliendelea kugandamiza eneo lile,, Mchungaji Joshua alishangaa.
                      *
Moto uliendelea kuwaka huku mzee Shirima naye akiendelea kushuka japo ule moto ulikuwa unampa changamoto kubwa. Kadri alivyoshuka ndivyo mgandamizo ulivyozidi kwa mchungaji Joshua 
"Ee mkuu wa kuzimu nisaidie katika hili" alitamka Mchungaji na kufanya moto uongezeke na kuzidisha ugumu kwa mzee Shirima.

"Mkuu wa kuzimu nipe nguvu zaidi,,, nipe nguvu nishinde hii vita" alitamka haya Mzee Shirima aliyekuwa juu angani.



ITAENDELEA........



TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: BINAMU 🔞 SEHEMU YA 11

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 1-5

CHOMBEZO: MASSAGE ROOM🔞 SEHEMU YA 21