MIMBA YA JINI SEHEMU YA 3

MIMBA YA JINI 03 ILIPOISHIA: "Basi bosi kapumzishe akili utajua pete umeiweka wapi." Mustafa alirudi ofisini kwake na kukaa kitini, alijitazama vidole vyake asiamini kama kweli hakuja na pete. Akiwa bado anavishangaa vidole vyake simu yake iliita, alipoangalia alikuta ni Shehna. Aliipokea: SASA ENDELEA..." Haloo." "Haloo Mustafa samahani, niliwahi kutoka kwa vile kuna sehemu nilitakiwa kuwahi." "Umepitia wapi?" "Jamani Mustafa kuna njia ngapi ya kuingia na kutokea ofisini kwako?" "Moja." "Basi ndiyo niliyopitia." "Mbona sekretari wangu hajakuona?" "Nimemkuta yupo bize ila sikutaka kumsumbua kwa vile mlango wako ulikuwa wazi." "Huyo hajakuona, na mlinzi?" "Sikumkuta inawezekana alikuwa msalani." "Mmh!" "Mustafa unaguna nini?" "Aah! Basi yaani bado ujio wako umekuwa kitendawili, pete yangu umechukua?" "Mustafaa! Niichukue ili iweje tuna uhusiano...