ADUI WA MAISHA SEHEMU YA 3



SIMULIZI: ADUI WA MAISHA

MTUNZI: LISSA WA MARIAM

SEHEMU YA TATU

Lameck alisema na kuamua kumpeleka Isabella chumbani kwake, alimuwashia laptop na kuweka movie, yeye akatoka nje hazikupita dakika nyingi alirudi na kukaa karibu yake, waliongea wakataniana, wakachekeshana, wakacheza kama watoto mwisho Lameck alipeleka midomo yake kwenye midomo ya Isabella, wakabadirishana mate, Lameck hakuishia hapo alipeleka mikono yake kwenye chuchu za Isabella

"Mmh Lameck please don't do anything" Isabella aliongea kwa sauti ya chini na kumtoa Lameck mikono

"Baby sifanyi kitu kibaya tunacheza tu" Lameck alijitahidi kubembeleza,

Alitumia kila mbinu mwisho wa siku akajikuta anamshinda Isabella na kilichotokea ni kelele kutoka kwa binti huyo, alilia kupita maelezo tayari alikuwa ameshapoteza usichana wake, hasira zilimpanda lakini hakuwa na chakufanya, zoezi halikuwa la muda mrefu Lameck alimaliza kazi yake,

"Pole baby sikujua kabisa Kama nitakuumiza"

"Sitaki kuongea na wewe Lameck naomba nirudishe hostel" aliongea akiwa amechukia

"Subiri tuoge kwanza mpenzi"

"Sitaki nitaoga nikifika"

"Jaman mbona umechange kiasi hicho Isabella"

"Kwani wewe ulichonifanyia unaona kizuri, mi nilikwambia usinifanyie hivyo wewe ukatumia nguvu na ukaendelea, umeona sasa ushaniharibia maisha yangu"

"Sasa kwani Mimi nimekuacha? Au nimekupa mimba alafu nimeikataa mpaka unasema nimekuaharibia maisha? Bella sipo Kama unavyofikiria tutaendelea kuwa pamoja usijali"

Isabela hakujibu kitu alisimama ili avae lakini alihisi kutembea kwa shida aliamua kuingia bafuni na kuoga, alipotoka akavaa pasipo kuongea kitu

"Subiri nikajimwagie maji"

"Nipeleke hostel sasa hivi!! kama ukienda kuoga mimi nitaondoka mwenyewe"

"Mmh Bella punguza hasira"

Lameck alighairi kuoga, alivaa tshirt na kuamua kumpeleka Isabella hostel, walipofika Isabella alishuka na kuanza kuondoka

"Mke wangu hata huniagi?" Lameck nae akashuka na kumuwahi akamkumbatia

"Me sitaki bana, niache sikutaki tena" Isabella alimsukuma akafungua geti na kuingia ndani,

Lameck alimuangalia na kuamua kuondoka

*******

Siku iliyofata Lameck aliwahi chuo mapema, alishangaa kumuona Isabella anampita bila kumsalimia kama hamjui, akaamua kumfuata

"Isabela hivi una nini wewe? kwanini unanipita? bado una hasira na mimi?"

"Lameck wewe endelea na mambo yako mi sitaki tena mambo yale, tena niache tu" Isabella alimaanisha kweli akaondoka,

Lameck alibaki akimsindikiza kwa macho mara Denis akafika

"Vipi tena mzee baba?"

"Dah Isabella anazingua kweli"

"Amefanya nini? embu funguka upewe ushauri"

Ilibidi Lameck amuhadithie Denis sababu ya yeye kugombana na Isabella

"Kumbe hilo tu! wewe sikia nikwambie, kwakuwa mzigo umekula tulia, kwanza ndo umepata urahisi wa kumuacha, yeye mwenyewe atakutafuta hizo hasira tu, yule kukuacha moja kwa moja hawezi coz we ndo boy wake wakwanza, wewe mkaushie tu, tena ikiwezekana tafuta demu mwingine hapa chuo, atakiona cha moto"

"Poa mwana"

Lameck aliamua kumpotezea Isabella, akablock na namba ili asiweze kuwasiliana nae, hata Isabella mwenyewe alishangaa kwanini Lameck hamtafuti tena, zikapita siku nne ikawa wanapitana tu wakiwa hawasalimiani

************

"Hallo naongea na Isabella? Ilisikika sauti ya msichana aliyempigia simu Isabella

"Yeah ndo mimi, je naongea na nani?

"Naitwa neema nilikuwa nahitaji kuonana na Wewe"

"Mmhh una shida gani kwani?"

"Mbona una wasiwasi? mimi nasoma hapa hapa CBE, niambie upo wapi nije tuongee"

Isabella aliposikia Neema anasoma pale anaposoma yeye, aliamua kumuelekeza alipo, imani yake ilimtuma lazima huyo msichana katumwa na Lameck huenda,

Baada ya dakika tano alifika

"Mi ndo Neema niliyekupigia simu, ni mpenzi wa Lameck, tena wa muda mrefu sana" Neema aliongea huku akimuangalia Isabella kwa dharau

"Kwahiyo ulikuwa unasemaje" Isabella alijikuta akiuliza hivyo

"Nimegundua kuwa Lameck anadate na wewe, hivyo nikaona nikutafute ili nikuonye mapema, achana na huyo mwanaume, kabla hatujawa na vita kubwa hapa chuoni"

"Sikiliza Lameck sina mahusiano nae so nipotezee"

"Unajitia unakataa, sasa ole wako siku nikukute nae utaona nitakacho kufanya, kwaheri" Neema alimaliza na kuondoka,

Isabella alijikuta akitetemeka huku akihema, roho ilimuuma vibaya mno

"Ina maana Lameck alinichezea tu mimi? kumbe ana mwanamke wake hapa hapa chuoni" aliwaza huku akijikaza asiweze kulia,

Mara rafiki yake Eliza alifika

"Oya muda wa kula twende zetu"

"Tangulia tu mi nitakula hata baadae"

"Vipi mbona upo hivyo?"

"Kuna msichana kaja hapa anaitwa Neema, anasema yeye ni mpenzi wa Lameck kwa muda mrefu, hivyo amekuja kunionya niachane na mpenzi wake" Isabella aliongea kwa unyonge

"Khee makubwa!! kwahiyo ukamwambiaje?"

"Tutaongea baadae, itabidi sasa hivi nimtafute Lameck kwanza"

Isabella alisimama na kuelekea anapokaaga Lameck alimkuta yupo na Denis, alisalimia wakaitikia

"Lameck nina shida na wewe nahitaji tuongee"

"Ongea hapa hapa nakusikia"

"Siwezi kuongea hapa inuka tusogee pembeni"

"Siinuki hapa, kama ukiweza ongea na kama huwezi basi" Lameck alijibu pasipo kumuangalia usoni Isabella

"Oya niga ngoja niwapishe ongea na mamaa" Denis akaamua kuondoka yeye

"Unaniletea mimi dharau mbele ya rafiki yako? Kwanini Lameck unafanya hivyo? then kwanini umeniblock?" Isabella aliongea huku akihema kwa hasira

"Ndo umekuja kuniuliza hicho tu au? Ok nimekublock kwasababu umesema hunihitaji tena, hivyo sikuona sababu ya kubaki na namba yako, je kuna lingine?"

"Lingine lipo, kwanini ulinidanganya huna mwanamke wakati unaye? Na kwanini umempa namba zangu mwanamke wako anipigie ili iweje, wakati tusha achana, au ulitaka mimi na yeye tugombane?"

"Mbona sikuelewi wewe? Mi mwanamke gani nimpe namba zako na za nini labda?"

"Sasa Neema kapataje namba zangu?" aliposema hivyo Lameck alishtuka

"Neema kakupigia?

"Sasa ulivyompa namba yangu ulitegemea afanye nini? kwanini ulinidanganya huna mwanamke wakati unaye? Lameck Mimi sipendi kugombana na msichana yoyote hapa chuoni naomba mwambie mwanamke wako asinifate tena"

"Isabela mimi na wewe si tushaachana tayari? Sasa maneno ya nini? kwanza sihitaji uniletee kesi kama hizo tena sawa? nilichokwambia wakati nakutongoza kuwa sina mwanamke nilikuwa sahihi wala sijakudanganya, Neema ndio alikuwa mwanamke wangu lakini tuliachana kabla sijakuapproach wewe"

"Mngeachana asingenifuata mpaka nilipo na kunitolea maneno ya karaha, ila sitaki kujua sana mahusiano yenu, cha msingi mwambie mpenzi wako asinisumbue tu na nina uhakika namba yangu ulimpa wewe au mlikuwa wote ndio akachukuwa kwenye simu yako, but thanks for everything Lameck, kwa kunidanganya na kunitumia, nakutakia kila la heri"

Isabella alimaliza na kuondoka kwa unyonge, Denis alirudi alipomuacha Lameck

"Vipi imekuaje Tena anaomba msamaha?" aliuliza

Isabella alimaliza na kuondoka kwa unyonge, Denis alirudi alipokuwa Lameck

"Vipi imekuaje Tena anaomba msamaha" aliuliza

"Mmhh hapana, Neema kamfata Isabella kumbe, istoshe sijui alipata wapi namba ya Isabella na kumpigia mpaka wakakutana"

"Duh kwahiyo inakuaje"

"Unajua nimejikaza kumjibu vibaya Isabella ili kuonyesha Sina time na yeye lakini now najisikia vibaya Sana hapa, Isabella ananipenda Mimi nishamuona hivyo siwezi kumpoteza, lazima nifanye jitihada za kumrudisha ili tuendeleze mahusiano yetu, lakini Neema kashaharibu kila kitu, hapa nina kazi ya ziada" Lameck aliongea kwa unyonge

"Kazi ipo hapo, unataka umuombe Bella msamaha"

"Ikiwezekana nitafanya hivyo bila kujali, ila sasa hivi ngoja nimtafute Neema kwanza, naenda kwenye chakula najua atakuwa huko kwasababu ni muda wa kula" Lameck hakutaka kupoteza muda alienda na kumkuta Neema amekaa na rafiki zake, jumla walikuwa watatu, wanasubiri chakula

"Wow! Lameck karibu" alimkaribisha

"Nina shida ya kuongea na wewe haraka tena inuka hapo" Lameck aliongea akiwa hacheki

"Jamani shem kaa utununulie japo juice basi" aliongea mmoja wa rafiki yake Neema.



ITAENDELEA........




TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: BINAMU 🔞 SEHEMU YA 11

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 1-5

CHOMBEZO: MASSAGE ROOM🔞 SEHEMU YA 21