KOVU LA MOYO SEHEMU YA 7
KOVU LA MOYO 07
MTUNZI: DEE LOVEE
"Mambo vipi Jonas" ... Robby alimsalimia kisha Poshie na Angelo pia wakafanya hivyo ... "Jonas huyu si unamfahamu?" .... Robby alimuuliza huku akimuoneshea Angelo ... "namjua ndiyo si Angelo huyo" ... "Vizuri kama unamjua. Huyu Mshikaji bwana alikuwa na matatizo yeye pamoja na mpenzi wake, kwa ufupi ni kwamba Mpenzi wake amefukuzwa kwao na amesusiwa yeye. Mimi niliwasaidia ila Bi Mkubwa amegoma na amewatimua, sasa mshikaji hana pa kulala na mimi naondoka naelekea Uganda naenda kusoma, sasa nilikuwa naomba wajishikize katiika geto lako mpaka Mshikaji atakapo pata kazi basi atachukua chumba chake" ... Robby alimwambia Jonas kwa umakini sana lakini cha ajabu alipomaliza kuongea Jonas alicheka sana na kumwambia ... "Hapa mtaani watu wanakusifu sana Robby kuwa una akili lakini kwa ili umechemka mchizi wangu. Unapata tabu kwa matatizo ya kujitakia? Yeye kajitakia majukumu mwenyewe basi muache aangaike mwenyewe, yani chumba kimoja niende kulala na hawa mataira je demu wangu akija mimi nitalala nae wapi?" ..... "Usiseme hivyo Jonas matatizo yapo kwa kila mtu leo kwako kesho kwa mwenzako" ... "huyu akili hana Angelo wenzake wote tunajipanga kutafuta maisha yeye kaona kumtia mimba mtoto wa watu ndiyo dili., muache ateseke mbona apo bado sana. Kama matatizo yatakuzidi sana, kuna Mzee mmoja yupo Mombasa anawapenda sana vijana kama nyinyi nitakupeleka lazima atakusaidia ila lazima atakuoa ....
Kauli ya Jonas ilimchefua sana Angelo na hakupenda kudhalilishwa mbele ya mpenzi wake, alimfuata Jonas na kumvamia ...
Angelo alimvuta Jonas mpaka kwake na akumuuliza ilimtoka ngumi moja takatifu mpaka katika Sura ya Jonas, ngumi ambayo ilimpeleka Jonas mpaka chini na kuumuka kama ngano iliyotiwa amila kwa wingi.
Angelo alitaka kuendelea kumfuata Jonas ili akamshikishe adabu, lakini robby alimzuia na kumkamata ipasvyo ili amuepushe Shetani.
Jonas baada ya kuinuka ndio alikuwa kama amemeza cd iliyokuwa imejaa matusi na alikuwa ameifungulia mtaa mzima akimtukana Angelo na mwenzake Poshie, na kuwafanya wapita njia waliokuwa wanapita maeneo hayo wasimameme na kutaka kujua nini kinachoendelea ....
Kauli za Jonas zilizidi kumchefua Angelo na hasira zikazidi kumpanda mwishowe akaponyoka na kumkimbilia Jonas ... Alifika na kumrukia miguu miwili ya kifua na kabla Jonas hajainuka Angelo alimfikia na kumkalia na akawa anampa ngumi za uso mithili ya Mike Tyson yupo ulingoni anapambana .... "Angelo muache utamuumiza, tafadhali nakomba mpenzi wangu achana naye tuondoke" ... Poshie alipiga kelele akimsihii mpenzi wake aache maswala ya ugomvi na waondoke eneo hilo ... Robby akishirikiana na baadhi ya watu waliokuja kuamulia ugomvi, waliweza kumshika Angelo na kumtoa pale alipokuwa amemkalia Jonas na akimpa ngumi za haja ...
Jonas aliinuka pale chini na kutaka aachiwe ili akapambane na Angelo huku mdomo ukiwa umepasuka na ukitoka damu kwa wingi ...
Hakuna aliyetaka kumachia na walimkamata ipasavyo, na baada ya kuona ameshikwa sana Jonas aliamua kuendelaza matusi yake akiwatukana kama hana akili nzuri.
"Sijui unafanya mambo gani Angelo? Badala ya tuangaikie maswala yako kwanza, unaenda kuyachokoza mengine sasa kama akienda polisi unafikiri itakuaje?" ... Robby alichukia na kumsema Angelo huku wakiwa wanaondoka pale kwenye ugomvi ... "Labda umwambie wewe Robby anaweza kukuelewa mana wewe ndio Rafiki yake mkubwa. Tatizo la Angelo yeye kila siku bado anajiona mdogo na hataki kubadilika sijui kwanini" ...."Ukisema hivyo Poshie utakuwa unakosea! Inamana wewe umefurahia kwa matusi aliyokuwa anatumwagia yule mpuuzi?" .... "Sijafurahia lakini pia sijafurahia na wewe kwa upuuzi wako wa kwenda kupigana na mpuuzi kwa sababu waote mmeonekana wapuuzi mbele ya watu ambao walikuwepo pale, kwani we ungenyamaza na tukondoka pale inamana matusi yake yangetutia vidonda? ... Poshie alimwambia Angelo huku akiwa amechukia kwa swala ambalo Angelo ametoka kulifanya pale.
Baada ya kina Angelo kuondoka eneo lile, wale Watu waliokuwa wamemshika Jonas walimuachia na kuondoka zao .... Jonas aliokota kipande cha mti na alikuwa akiwakimbilia wakina Angelo walipokuwa wameelekea ....
"Angelo anakuja huyooo" ... Poshie alipiga kelele, baada ya kumuona Jonas akija mbio huku akiwa amelenga kumpiga Angelo na ule mti ... Angelo aligeuka nyuma na kumkwepa Jonas ambaye alikuwa ameshanyanyua juu mti ili ampige Angelo lakini kwa bahati mbaya baada ya Angelo kumkwepa, ule mti ulitua kichwani kwa Poshie .... "Buuuuuuu!!" ... Poshie alikuwa akiyumba nakwenda kuliangukia tumbo. Robby alimuwahi na kumdaka lakini akatereza na Poshie akamuangukia Robby mpaka chini Pwaaaaaa!! ...."Poshieeeeeeeeeeeee" .... Angelo alipiga kelele na kumkimbilia mpenzi wake ili kwenda kumtazama kama bado alikuwa mzima ...... "Poshie amka mpenzi wangu, tafadhali Poshie usife bado nakuitaji amka" .... Angelo alimtikisa huku akimuamsha Poshie lakini wapi Poshie hakuwa hana kauli hata kidogo.
Damu zilikuwa zikimmwagika kwa wingi Poshie kiasi ambacho Roby alianza kupatwa na wasiwasi akihisi labda Poshie atakuwa amekufa.
Hakuna kitu kibaya kama kuona damu ya mtu aswa unapohisi kuwa utakuwa umemuua mwenzako bila ya kukusudia, Jonas alikuwa ameshikwa na butwaaa na kujikuta akitetemea akiamini lazima Poshie atakuwa amekufa ... "Unaona umeua, Jonas unaona umeua" ... Robby alimwambia Jonas huku akimfuata alipo. Jonas alistuka na kuzidi kuogopa, hakutaka kuendelea kusubiri alikurupuka na kukimbia eneo lile
****
Walipata msaada kwa wasamalia wema na wakamkimbiza Poshie Hospital na akapata kitanda ..."Angelo wewe ni mtu mkubwa sasa na karibuni unatarijia kuitwa Baba, hivyo unatakiwa ubadirike sana kutoka katika maisha yako ya zamani ili kuingia katika maisha mapya. Kwasasa wewe hautakiwi uishi kwa kujifikiria wewe mwenyewe bali unatakiwa uishi kwa kuifikiria familia yako yani wewe, mkeo na mtoto wako. Kosa moja ambalo utakalolifanya basi kaa ukijua unaweza kuigharimu familia yako kwa kosa lolote unaloweza kulifanya. Nafikiri mfano umeuona leo" ...
Usiku huo Hawakulala hata lepe moja la usingizi badala yake Robby aliutumia usiku huo kumpa kichen party bila vyombo Angelo {Kumfunda bila sherehe} ... Angelo alimuomba sana msamaha rafiki yake na kumuakikishia kwamba jambo hilo halitokuja kujirudia tena katika maisha yake.
*****
Asubuhi kulipokucha waliandaa chai chumbani kwa Robby ili wampelekee mgonjwa wao. Robby alitoka nje ili kumvizia Mama yake ili hasimuone Angelo na wakafanikiwa kutoka salama katika chumba cha Robby na wakaelekea Hospital.
Baada ya kufika Hospital walistuka baada ya kumkuta Jonas akiwa na Poshie huku Poshie akiwa amepata faham na wakiongea na akiwa amemletea Poshie mtoli na alikuwa akila.
Japokuwa Robby alimuhusia sana Angelo jana usiku lakini Angelo alichukia kumkuta Jonas akiwa na mkewe ..."Umefuata nini hapa" ... "Angelo lini utabadilika mpenzi wangu? Yani Badala ya kuniuliza mimi kwanza hali yangu wewe unashikiria maswala ya ugomvi tu, basi gombaneni tena mniue kabisa" .... Poshie aliongea kwa uchungu huku akilia na Angelo alimuomba sana msamaha Mpenzi wake ... "Jonas amekuja hapa kwa niaba yako na yangu pia amekuja kutuomba msamaha na amesema amejifunza kutokana na makosa, istoshe yupo tayari kutusaidia" .... Jonas aliwapigia magoti na kuwaomba msamaha kisha akawaambia .... "Kuna chumba kinapangishwa kule bondeni kwa Tsh 15,000 Mwenyewe alikuwa anataka kodi ya mwaka mzima ambayo ni 180,000. Mimi katika akiba yangu, nilikuwa na Tsh 1,00,000 nilikuwa nataka kuwasaidia je mtakuwa na hiyo ya kuongezea hili mlipie pale mpate kwa kujishikiza" ...
Angelo hakuamini hata kidogo kwa maneno ambayo ameyaongea Jonas alimshukuru sana kwa moyo wake wa huruma na kuombana msamaha ... Robby aliamua kutoa simu yake ili ikauzwe na wapate kiasi cha kuongezea ... Poshie pia aliamua kutoa simu yake ili nayo iuzwe na wapate pesa ya kuongezea katika kodi.
Robby, Jonas pomoja na Angelo walitoka hospital na kuelekea mtaani ili wakauze simu na wapate kiasi cha kuongeea pale katika kodi ...
Walifanikiwa kuiuza simu ya Robby kwa Tsh 50,000 na simu ya Poshie kwa Tsh 30,000 na wakaongzea na ile pesa aliyokuwa nayo Jonas na ikafikia Tsh 180,000 .... Haraka walitoka pale na kuelekea kule kwenye chumba na walikuta tayari kimeshapata mpangaji.... Nguvu ziliwaishia na wailikaa chini huku wakiwa wamechoka kabisaa.
Mchana ulipofika walitoka na kuelekea Hospital na kukuta Poshie akiwa ameruhusiwa lakini walikuwa wanadaiwa kiasi cha Tsh 50,000 pale Hospital na kuna dawa za kiasi cha Tsh 10,000 walitakiwa kununua....
Angelo alimtazama Robby na kushusha pumzi kisha akachoka kabisa.
Robyy alimtazama na kumfuata pale alipo kisha akamwambia ... "Mbona umechoka sana Kaka?" ..."Lazima nichoke Robby, yani tunapiga atua 5 kisha tunarudi nyuma atua 10. Sasa pesa yote tunalipa Hospital, nini atma yetu? Au ndio tutaendelea kulala katika viwanja vya mpira?" .... Angelo alimwambia Robby huku tayari macho yakiwa yameshaiva na machozi yalikuwa yakimtoka ....
Robby alikuwa ni kijana ambaye mara nyingi alikuwa hapendi kukurupuka pindi anapotaka kutoa maamuzi ... Alinyanyuka na kutafakari kisha akapiga atua kadhaa na kugeuka na kumtazama tena Angelo na kumwambia ... "Poshie amekaa siku 2, tayali inatakiwa zaidi ya Tsh 50,0000. Kama tukimuweka zaidi hapa, inamana tutatumia pesa zaidi na tutakuwa tumerudi nyuma zaidi. Lete hiyo pesa" .... Angelo alitoa pesa na kumpatia Robby.
Robby alichukua pesa na kwenda kulipia, kisha akachukua dawa kabisa na akarudi walipo. Walimchukua Poshie na kutoka pale Hospital.
Alipofika nje walichukua Tax na Wakaondoka kuelekea mitaa ya kwao .... "Tuache hapo mbele Dereva" ... Robby alimwambia Dereva ambaye naye aliegesha gari yake vyema na wakashuka.
Robby alitoa noti ya Tsh 10,000 na kumpatia yule Dereva tax. Japokuwa alilalamika sana, kuwa walipokuja ni mbali, lakini Robby alimuomba sana na akamuelewa na akaondoka zake."Bado sijaelewa hapa tumekuja kufuata nini?" ... Angelo alimuuliza Robby huku akimtazama .... "Muda mwengine Maswali yako hayana nafasi Angelo, ngoja tu utajua tumekuja kufanya nini?" ....
ITAENDELEA......
TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.
Maoni
Chapisha Maoni