MZIMU UMERUDI TENA EPISODE:29



MZIMU UMERUDI TENA.

EPISODE:29

MTUNZI;HAMIDU MCHAKO

....................TULIPOISHIA..............
Nikiwa nahangaika kumpokonya niliwaona watu wawili wamemshika baba na wamemnyooshea bastola waliniambia tulia na achia hilo begi laa sivyo tunamwaga ubongo...........

..........ENDELEA..........

Niliduwaa kidogo na nikagundua tumetekwa bali hatukupelekwa gest.

Nilimtazama kwa hasira yule dereva halafu ch kustaajabisha hakuwa na wasi wasi wowote.
Nilianza kufikiria baba na begi la pesa kipi nipoteze?
Niligundua baba anadhamani kuliko pesa hivyo sikua na jinsi niliamua niwakabidhi lile begi la fedha ila kabla sikuwakabidhi niliwauliza.
➡Jeee tukisha wakabidhi hili begi mtatuacha huru?

Walijibu ndio tutawaachia huru.

Moyo wangu ulifarijika kuwa watatuacha huru na wakituacha huru tutarudi kuja kupambana ili waturudishie pesa zetu.

Niliwakabidhi lile begi na baada ya kutusachi na kugundua kuwa hatuna silaha yeyote walituachia.

Lile begi Alipewa mtu mmoja na alionekana ndio kiongozi wa kikundi kile cha kigaidi.
Baada ya kupewa alilifungua kisha akakagua hakuamini kile kiasi cha fedha alichokiona kwani zile fedha zilikua ni nyingi sana.

Nilianza kuwaza mengi huku nikijiuliza ni kwanini mimi kilasiku ni wamatatizo?
Nilizani matatizo yatakua yameisha baada ya kukutana na babaangu mzazi lakini sivyo.
Na ninaona kama vile ndio yameongezeka.
Yaani bado twatafutwa na Askari polisi na huku twatekwa tena na kikosi cha magaidi.
Nilini na mimi nitakuja kuwa na furaha?
Au ni kwa sababu sisi sio watu wa kawaida na hatufahi kuishi karibu na wanaadam?
Nilijiuliza maswali kadha wa kadha Ambayo sikuyapatia majibu.

Nilikuja shituka na kutoka kwenyedimbwi la mawazo baada ya kusikia bunduki zikikokiwa na kuwekwa sawa.
Tulinyooshewa zile bunduki na moja kwa moja nilihisi kuwa huwenda ndio siku ya mwisho kuiona dunia.

Nilimtazama Baba na baba nae alinitazama mimi.
Niligundua macho ya baba yako tofauti yaani alishaanza kubadirika na alikua yuko makini Na alijiandaa kukabiliana na chochote kitakachotokea.

Lakini kabla hawakufyatua risasi ilisikika sauti ikisema.
➡Eneo hili ni salama na twahara.Hivyo basi sitopenda kuona eneo hili linamwagika dam.
Ninachohitaji wachukueni na mkawamalize ndani ya msitu.

Waliamua kuacha walikuja watu wawili walitushika na walitunyanyua.
Hakika watuwale walikua na nguvu sana tena sana.
Nilianza kukokotwa na kusukumwa kama vile ninamakosa ya mauwaji.

Tulizunguuka nyuma ya lile jengo na tulitembea kama hatua sabini tulianza kukuta msitu mkubwa ambao ulifungamana vizuri mitiyake.
Moyo wangu ulianza kufarijika huku nikijisemea moyoni.
➡Nitamrarua ntuhuyu na dam yake nitainywa.

Wakiwa hawana hili wala lile.
Walizani wamewabeba watu wa kawaida kumbe sivyo walibeba mauti.

Kabla hatukufika eneo walilokua wanatupeleka niligoma kwenda.
Nilipogoma kwenda alinipiga kichwa.

Nilihisi maumivu ya ajabu na pale pale macho yali change na kucha zilianza kutokeza.
Baba alinitazama na alipandwa na hasira pale alipoona mimi nimepigwa.

Kabla hawakujipanga na lolote Mimi na baba kilamtu aliudaka mkono uliokua na bunduku.

Na kwa nguvu tulizokua nazo tulifanikiwa kuwanyag'anya zile bunduki na tulizitupa mbali kidogo na eneo lile.

Nilijikuta sikuile nimebadirika ghafla tena huku nikiwa na nguvu za ajabu Misuli ilitanuka huku nikiwa napumua kwa hasira kwa nguvu nilizokua nazo nilianza kuunguruma kama simba dume.
Yule mtu aliokua na kifua kama ukuta alianza kutetemeka na aliangalia vizuri njia ili anitoroke.

Nililigundua lile nilimrukia na nikamlarua kifuani kicha nikamuangusha chini na nilipeleka mdomowangu shingoni kwake na nikayakita meno yangu bila huruma na nikaanza kufyonza dam yake.

Nilitulia pale kwenye shingo kama dakika nbili aliruka ruka mwishoni alitulia.
Na sikuelewa ni kwanini nikiwa katika hali ile dam ninaiona ni tam sana kama Ninavyoiona Asali tam nikiwa katika umbile la kibinaadam.

Niliutoa mdomowangu shingoni kwake na tayari alishakufa japokua alikua na minguvu ya kuonea watu ila haikumsaidia kitu.

Nilimtazama baba nae nilimuona bado kaig'ag'ania shingo ya yule mtu na alikua anaendelea kufyonza dam taratibu.

Nakiwa naendelea kumtazama baba Nilimuona mtu katoka msituni mbio sana huku anapiga kelele.
Nilitazama kwa umakini ni kitugani kinachomkimbiza na niligundua kunamnyama anamkimbiza.
Bila kujali ni mnyama gani niliamua niende nikatoe msaada.
Nilitoka eneo lile mbio Huku nikifata zile kelele.
Niliamua kupita njia ya mkato ili nimtokee kwa mbele yule mnyama.
Nilifanikiwa kufanya vile na nilimtokea yule myama kwa mbele na nikaanza kunguruma.
Nilimtazama kwa makini alikua ni mbwa mwitu hivyo ni jamii moja.
Mnyama yule nae pia alinguruma na mimi niliongeza mngurumo kumzidi yeye.
Alipoona mngurumo wangu ni mkubwa alikunja mkia kuonyesha kuwa hawezi kupambana na mimi.
Muda ule ule baba nae alifika eneo lile nae alinguruma kwa nguvu kuliko hata simba dume.
Mnyama yule alizidi kukunja mkia na aligeuza na akaondoka.
Hatukupenda kupambana nae kwani tulimuona ni kama jamii moja tu.

Baada ya kuondoka mnyama yule baba alianza kusema.
➡Twende kwenyeile kambi ya magaidi tukapambane hadi waturudishie pesa zetu ili tuendelee na safari yetu.

Nilimwambia baba.
➡Mimi sioni haja ya kurudi kule baba kwa sababu sisi sio watu wa kawaida.Wazolangu ninaomba tubaki tu huku huku msituni tuishi huku huku hadi mungu atakapochukua roho zetu.
Kwa sababu nimegundua dam zetu na zao ni tofauti hivyo basi tukikaa karibu nao matatizo hayataisha na tutaendelea kufanya mauwaji kila siku hivyo basi sioni haja ya kurudi kwenda kupambana na watu wale kwa sababu sisi hatuwezi kuishi nao karibu.
(Niliongea kwa sauti ya kunguruma na ya mkwaruzo huku nikionekana kukata tamaa)

Baba alinisogelea na akaanza kuonge kwa sauti ya mngurumo na yenye mikwaruzu.
➡Hamidu mwanangu usikate tamaa kumbuka maisha tuliyomuacha mamaako kijijini.
Na fikiria ni kitugani tulimuaga kipindi tukiondoka.
Na kumbuka wewe ni nani katika kijiji chako hivyo basi bado unahitajika urudi Kijijini.
Sasa ni lazima tukamilishe jambo lilikotutoa jijijini sawa.
Hivyo basi ninakuomba nyanyuka na twende tukapambane.

Sikuwa na jinsi na Aliponitajia mama ndio Alipo nimaliza.
Nilikumbuka kweli mama tumemuacha katika mazingira magumu sana.
Nilikumbuka sikuile naagana na YUSRA basi hapo zilinijia nguvu za ajabu.
Nilinyanyuka sehem ile na tuliaza kukimbia kwa kasi kuelekea Kwenyeile kambi ya magaidi ili wakatupatie pesa zetu.

Kwa mwendo na kasi tuliokua nayo tulifika eneo lile na hatukuingia kwa getini bali tuliiruka fensi na tukatua kwa ndani.
Mlinzi wa geti Alisikia kile kishindo hivyo basi alianza kusogea eneo lile lililotokea kishindo bila kujua anayafata mauti.

Sikutaka kupoteza muda nilimuashilia baba Aendelee kuingia ndani zaidi na aniachie yule mlinzi nimmalize Mimi.

Baba bila kujali aliendelea kuingia ndani kwa kunyata sata na mimi nilibaki na yule mlinzi eneo lile.

Mlinzi aliendelea kusogea.
Nikamuweka tageti vyema na nikawa namtazama kwa umakini wa hali ya juu.

Alipofika Mahali nilipohitaji Afike nilimrukia na nikaularua usowake kwa kuchazangu.

Alitaka atoe firimbi ili apulize ila kabla hajatoa niliushika mdomo waka na nikazitengua taya zake.

Na sikufanya kosa nililishika koolake kwa kuchazangu na nikalitoa koo lake nnje.

Alisikika akikoroma kwa sauti ya chini huku akirusha rusha mikono na miguu na dam nyingi zikimvuja.
Nilisimama nikamtazama na nikagundua hawezi kuinuka tena huyu ni wakufa.

Sikutaka kupoteza muda baada ya kummaliza mlinzi nilishika ile njia aliyoelekea baba.
Nilipopiga hatua kadhaa mbele nilikutana na mtu tena kalala chini lakini hakuwa na jeraha lolote wala sehem yeyote anapovuja dam.
Nilihisi labda ni mtego wa kunaswa mimi.
Nilimsogelea yule mtu kwa umakini wa hali ya juuu.
Na nilipomkaribia nilimrukia na nikakaa juu ya kifua chake huku mikonoyangu yenyekucha kali niliipeleka kwenye shingo yake.

Lakini nilipomtazama yule mtu kwa umakini nilimuona anatokwa na dam puani.
Na nilipomgeuza kichwa niligundua ameshaa kufa.
Niliistaajabu style ile ya mauwaji na niligundua style ile kaitumia baba kumuua yule mtu.
Niliikagua Ile style kwa umakini niligundua Alitumia kumnyonga au kuitengua shingo.
Niliona ni style moja nzuri hivyo basi na mimi nilihitaji kuitumia katika mashambulizi yale kwani ni style ya mkato.

Niliendelea kwenda mbele nilikuta kila kono kunawatu wamepigwa chini tena muda sana.
Ni jeshi la watu wawili Hamidu na Babaake lakini ni kama vile jeshi la watu mia mbili katika mashambulizi.

Niliendelea kusonga mbele pia nilikuta watu zaidi na zaidi wamelala chini hadi nikamkuta baba kwenyekona moja ya kuingia kwenye jengo kuu la Mkuu wa kikosi kile.

Ghafla nilimuona baba ameangalia juu kisha akanivuta upande wa pili.
Kumbe kikosi kile kilikua na maninja na baada ya kunivuta upande wa pili mshale wenye kitambaa chekundu ulikita ukutani na laiti nisinge sogezwa na baba ungenikita kooni.

Hakika ile ilikua ni kazi nyingine mpyaaa tena inahitaji ujuzi wa hali ya juuu.

Tulijibanza sehem ambayo ilikua na usalama.
kisha baba akaniambia.
Mwanangu unaonekana ni mpambanaji mzuri lakini hukupitia mafunzo ya hisia.
Hivyo basi maninja sikuzote huwezi ukawaona kwa macho ya kawaida bali ni lazima upitie mafunzo ya hisia.
Sikufaham kama eneo hili kunamaninja na laiti ninge faham nisinge kuruhusu uingie kwa sababu ni hatari kwako.

Hivyo basi ni lazima tugawane majukumu.
wewe utapambana na hawa watu wa kawaida.
Na mimi nitapambana na hawa maninja kwa sababu mimi nishaa pitia mafunzo hayo na ninauwelewa mkubwa tu juu yao.

Sikuwa na neno juu ya maamuzi ya baba.
Baada ya kukubaliana.
Baba aliniambia niwe makini kisha nilistaajabu kwa kitu alicho kifanya.
Kwani alipaa juu kama ninja na kwenda kutua juu ya mti mkubwa.
kusema kweli baba alikua na uwezo mkubwa.

Baada ya kikosi kujigawa mimi nilianza kutekeleza kazi yangu.

Kulikua na walinzi wawili Kwenye mlango wa kuingia kwa mkuu wa kikosi.
Hivyo basi nilihitaji niwamalize.

Nikiwa napanga mbinu ya kuwafata nilimuona mmoja kati yao anakuja eneo nililokuwepo mimi.
Nilisogea nyuma nikajibanza huku nikimsubilia kwa ham.

Aliendelea kusogea hadi akanikaribia na mimi sikupoteza muda nilimrukia na nikakishika kichwa nikakizunguusha na nikaitengua shingo yake.

Nilimuachia Akadondoka chini kama mzigo.

Nilijipanga upya ili niende nikamshambulie yule mlinzi mwingine alio baki.
Ile napiga hatua niliona kitambaa cheusi cha kininja kinadondoka chini.
Niliamini ni kazi nzuri anayoifanya baba.

Niliendelea kumsogelea yule mlinzi mwingine bila yeye kujijua.
Nae bila kupoteza muda nilimrukia na nikamtengua taya ili asije akapiga kelele.
Nikaupitisha mkono wangu chini ya mapaja yake mawili.
Nilianza kuziminya mbegu zake za kiume kwa nguvu hadi nikahisi zimepasuka kisha nikamtengua shingo nikamtupa chini.

Kabla ya kuingia ndani nilichungulia na nilimuona yule dereva wa tax na yule alonipokonya begi la pesa na watu wengine wawili warefu tena wanene waliotuna misuli sikufaham kama wale ndio wakuu wa kikosi au laaa.
Niliendelea kuchunguza kwa umakini na niligundua wanazihesabu zile fedha zetu.

Nilifungua mlango taratibu bila ya wao kujua na nikaanza kuingia ndani.

TURUDI UPANDE WA PILI KWA BABA AKE HAMIDU.

Mzee alionekana kupambana kininja.
Alikua anaruka kutoka mti mwingine kwenda mti mwingine na alikua anamfata ninja mmoja hatari sana kwani ninja wale walikua ni wawili na mmoja alishammaliza na ndio mwenye kile kitambaa kilicho dondoka chini.
Yule ninja kila akifatwa mti huu anaruka kwenye mti mwingine na Akifatwa kwenye ule mti mwingine anaruka kwenye mti mwingine.
Kumbe yule ninja alisha jua yule mzee sio mtu wa kawaida kwani macho yake yalikua tofauti na pia meno mawili yamejitokeza mbele na pia ana kucha ndefu hivyo basi alikua anamsogeza kwenye mitego yake ili atakapo naswa amshambulie kwa urahisi.

Mzee bila ya kufaham hili wala lile nae alikua anafata na walibakisha mti mmoja ili waukute ule mtego.

Yule ninja aliruka juu ya ule mti wenyemtego na ale sehem alioruka kwa pembeni kidogo tu ndio kunasehem ya kuufyatua ule mtego ili ukunase.
Hivyo basi hata yeye mwenyewe ninja akiyumba vibaya unamnasa.

Ninja alitoka kwenye ule mti ili yule mzee nae aruke.
Ninja aliruka mti wa pili na mzee alijiandaa kuruka kwenye ule mti aliotoka yule ninja na mtiule ndio unamtego,

Daaaaaah Amakweli kwa kilichotokea sikuweza kuamini na sikuzote ukimuamini mungu atakurinda na atafanya mepesi kwa kila jambo.
Kwani yule mzee kabla ya yeye kuruka.
mtiule ulikua na kima.Hivyo basi yule kima ndio aliruka ilesehem aliyotoka ninja na akaufyatua ule mtego akanaswa.
Hapo mzee ndio alipogundua kumbe humu kunamitego nasi alianza kupambana na yule ninja kwa tahazari.
Ninja baada ya kuona lengolake halikutimia.
Moja kwa moja aliamua Ashuke chini.
MZEE nae hakutaka kupoteza muda nae alimfata chini Ili akapambane nae.

Kwa mikwara na mbwembwe aliyokua nayo ninja yule.
Mzee asipokua Makini anaweza kupoteza maisha kwa misteki ndogo tu.
Ninja alitua chini na MZEE nae Alitua chini na walianza kuzipiga kavu kavu bila hata siraha.
Ninja Alitishwa Akajaa Alipewa za dabo mbili tena za uso na alikatwa wenge.
weee mzee sio mtu wa sport sport.

Ninja naada ya kukatwa wenge na ndonga mbili za uso Alipotea.
Daaaaah ilikua ni kazi nyingine hiyo ya kupambana na kiumbe kisichoonekana.
Hapo mzee baada ya kuona ninja kapotea Alishajua ni hatari kwake.
Na Hapo ndio aliona umuhimu wa kupambana kwa kutumia hisia.
(Ngoja tumcheki mzee tuone kama atashinda maana ni hatari kwake.)

MZEE alifumba macho na Akaikutanisha mikono yake kisha akaa style ya kupambana.
Kabla Hakijiandaa sawa sawa ninja alitupa mshale.
Ona matusi ya mzee.
Mzee aliudaka ule mshale huku kafumba macho na kwa dharau aliuvunja vipande viwili na akautupa chini.
Kile kitendo Cha kuvunja ule mshale kilimuuzi sana yule ninja na ni tusi kubwa kuvunja mshale wa ninja yaani umeonyesha dharau kubwa sana.
Ninja alichukia Aliutupa upinde uliokua mkononi mwake na aliamua ashuke aje apambane kiume.
Hakujua kuwa anayafata mauti.
Alishuka kwa kasi ili Aje ampige kikumbo mzee.
Mzee kwa hisia alizokua nazo na alizokua akizitumia vyema Aligundua na Aliamua kuchukua kipande cha mshale alichokitupa chini na akamchoma yule ninja kooni pindi alipokuja kumshambulia MZEE.

Ninja Alidondoka chini na kupoteza maisha.
Alimfungua usoni na kumtazama kama anamjua lakini hakumfaham.
MZEE alimaliza kazi kwa namna hiyo.

TURUDI UPANDE WA PILI
Mimi Baada ya kuchungulia na nilipowaona Wanizihesabu zile fedha nilifungua mlango taratibu na nikaanza kuingia bila ya wao kujua.
Niliingia ndani nikiwa niko full mbwa mwitu.
Lakini sikuile nilijihisi niko tofauti.
Kwani nilikua ninao uwezo wa kusimama kama binaadam na pia nilikua na uwezo wa kujikunja na kutembea pamoja na mikono kama mnyama.
Nilikua ninazo akili za kibinaadam yaani nilikua nakifaham ninacho kitenda.
Nilikua nazungumza japokua ni sauti ya besi na inamikwaruzo lakini ilikua inasikika na kueleweka.

Sikupenda nipoteze muda niliingia kisha nikaufunga mlango na funguo nilibakinayo mimi.
Ilikua ni hatari kwangu kuufunga ule mlango lakini pia ilikua ni hatari kwao.
Niliruka juu na nikatua kati kati ya meza.
kilamtu Hakuamini kwa alichokiona Hivyo basi walichanguka na walisahau silaha zao mezani na kila mtu alikimbilia mlangoni lakini waliukuta mlango umefungwa.
Nilizikusanya zile silaha na kwa nguvu nilizokua nazo nilianza kuzivunja kama vijiti na zote nilifanikiwa kuzivunja.

Nilitoka pale juu ya meza na nikaanza kuwafata niliwakuta wamejikusanya sehem moja kamavile wanahisi balidi.
Nilimuangalia kwa hasira sana yule alietuuza na kutuleta eneo lile Dereva wa Tax kisha niliwasogelea na nikamrukia yule dereva na nikaanza kumgalagaza chini lakini kabla sikumchoma kucha wala kumg'ata alipoteza faham.

Kunammoja Alionekana Anamwili mkubwa na Anamacho yanawaka waka kwa mtazamo wangu niligundua yule sio mtu wa kawaida.
Na yeye hakukurupuka kupambana na mimi bali alianza kuwatuma wenzake ndio wapambane na mimi yeye ali kaa pembeni.
Alikuja jamaa mmoja mrefu tena mnene na ametuna misuli na alianza kupambana na mimi.
Nilimtazama ujio wake na kabla hakuanza kunishambulia nilimrukia kifuani na nikaishika shingo na nikaitengua au nikainyonga alidondoka chini na kupoteza maisha.
Alimtuma mwingine Ambae Alionekana ni mwanaadam wa kawaida nae pia sikumchelewesha nilimnyonga shingo.
Pambano sasa lilianza kwake na alionekana yuko vizuri maana Alikua anaruka ruka hakukubali nimshike hata kidogo.
Niliendelea kupambana nae lakini Alikua hashikiki na mwisho wa yote tulikuja shikana yaani kila mmoja kamshika mwenzake kwa nguvu na tulianza kusukumana kama vile myeleka na lengo langu nim'bane ili nimkite jino hata la koo.

Tuliendelea kusukumama na kila mmoja aligoma tukawa hatuendi kulia wala kushoto.
Yule Dereva Alizinduka pale chini na Alipoona wote tumeshikana na hakuna hata dalili ya mimi kuachiwa au kuachiana Aliangalia nyundo na aliiona Aliifata na Akaichukua na alianza kuja taratibu tena kwa kunyata ili aje anipigenayo kichwani............

..................ITAENDELEA.................



TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: BINAMU 🔞 SEHEMU YA 11

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 1-5

CHOMBEZO: MASSAGE ROOM🔞 SEHEMU YA 21