Mo Dewji Aachia Ngazi Simba

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba ambaye pia ni mwekezaji wa Klabu hiyo, Mohammed Dewji ‘Mo’ ametangaza kuachia ngazi wadhifa huo baada ya mashauriano na Bodi ya Simba kupitia kikao kilichofanyika Septemba 21, 2021. Akizungumza katika video clip ambayo ameipost kupitia akaunti yake ya Instagram, Mo Dewji ameanza kwa kusema; “Asalam akeikum, Bwana Asifiwe, naomba kutoa taarifa yangu kwa wanachama na mashabiki wa Simba. Kwanza nianze kwa kutoa shukrani zangu za dhati kwa wana-Simba, mmetuunga mkono kwa miaka minne kama mwenyekiti wa bodi. Ninatoa shukrani zangu kwenu nyote kwani bila nyinyi, mashabiki, wapenzi na wanachama wa Simba tusingezeza kufika hapa. “Napenda nichukue fursa hii kuwashukuru viongozi wote wa Simba Sc na Wajumbe wa Bodi kwa kunipa ushirikiano mkubwa, kwenye uongozi wangu kwa miaka minne. Kwenye hii miaka minne tumepata mafanikio makubwa, tumechukua mataji manne ya ligi na tumefika hatua nzuri kwenye Champions League. “Muda ...