MCHORA KUCHA PART 06



 MCHORA KUCHA


MTUNZI: McLAURIAN


PART: 06


ILIPOISHIA


Lisa yu chumbani akiwa amekumbatiana na Mr. Kucha huku wakicheza mziki mnono wa bufa taratibu. Wakati wakiwa wanaendelea kuburudika, Noel akiwa ananyata, alifika mlangoni huku akiwa ameandaa kisu chake kwa maangamizi..


SONGA NAYO...


Baada ya kufika mlangoni, aliusukuma lakini bahati mbaya kwake haukuweza kufunguka hali iliyoashiria kama umefungiwa kwa ndani.


Alitikisa kichwa chake kwa hasira kisha akatupa kibegi chake chini .


Aliusukuma kwa mara nyingine tena lakini haukufunguka ndipo alipoamua kugonga kwa nguvu.


"'Ngo..ngo...ngoo..." sauti za mlango zilisikika.


Wakiwa wamekumbatiana walishutushwa na sauti hizo ndipo Mr. Kucha alipobaki amekodoa macho kodo huku Lisa naye akitega masikio yake mithiri ya panya aliyehisi harufu ya paka 


"'Nani anagonga tena?" Mr. Kucha aliuliza kwa wasiwasi mkubwan


"Watakuwa ni watoto wa jirani maana huwa wanapenda kuja kuangalia Tv" Lisa alimjibu Mr. Kucha.


Baada ya kumwambia hivo, Mr. Kucha alisikilizia tena ndipo mlango ulipogongwa kwa nguvu sana mpaka mwangi ukasikika chumbani.


"Hee! Watoto gani mpaka wanatetemesha nyumba kiasi hiki!?, ebu kuwa serious hapa kuna jambo.." Mr. Kucha aliongea kwa hofu huku kwa mbali kijasho chembamba kikiwa kimeanza kujitokeza kwenye pua yaken


Kabla Lisa hajajibu chochote, Noel alitamka kwa nguvu,


"Fungua mlango ...!, ina maana hunisikii au?!"


Bila kupepesa macho wala shaka yoyote ile, Lisa alijua moja kwa moja sauti ya Noel ndipo aliposhika kichwa kama mjane aliyefiwa na mwanaye.


"Mama yangu wee!? Aliongea kwa sauti ya chini..


"Hee. .!heee!. Kuna nini!..kuna nini?" Mr .kucha akiwa anahema kama jogoo waliotoshana nguvu, alimwambia Lisa 


"'Sorry mme wangu karudi !,  yooo...huuu!!" Lisa alijibu huku akiwa anahangaika kama kuku anayetafuta sehemu ya kutaga kwa mara ya kwanza.


"Hee! Mme tena!, si uliniambia huna mme?, umenileta humu kuniua?"'Mr. Kucha alilalamika mithiri ya mwanafunzi aliyepunjwa maksi zake.


"We ongea polepole..."Lisa alimwambia.


Baada ya kuambiwa hivo, Lisa alifungua kabati la nguo lililokuwa na milango mitatu kisha akamwambia Mr. Kucha aingie lakini baada ya kuingia, mlango ulishindwa kufungwa kabisa 


"'Hee!..hapa naonekana...." Mr. Kucha alijibu kwa sauti ya pole.


Alikimbilia chooni lakini badaye aliwaza kuwa akikitwa itakuwaje ndipo alipochomoka.


Wakati yote yanaendelea, Noel alikuwa bado mlangoni kwa hasira kali huku akijitahidi kuita kwa nguvu lakini mlango haukufunguliwa .


Baada ya mbinu za kujiokoa kuonekana kuwa ngumu kwelikweli kama tajiri kuuona ufalme wa mbingu, walikuja na mbinu moja ambayo ilibuniwa na lisa huku akidhani itafaa kwa asilimia mia moja kutokana na sura na mwonekano wa Mr.Kucha.


Alifungua kabati la nguo kisha akachomoa brauzia, gauni refu , wigi , lipshine, wanja,pamoja  viatu virefu 


Baada ya kuvitoa alimvalisha Mr. Kucha na kweli alibadilika kwa asilimia 1000 kabisa yaani alikuwa mrembo wa aina yake mpaka akamzidi Lisa.


"Hapa unatakiwa uongee kwa sauti ya kike" Lisa alimwambia Mr. Kucha.


"Naweza sana kuhusu hilo usijali.."Mr. Kucha kwa sauti ya kurembua alimjibu.


Mambo yalionekana kukamilika ndipo Lisa alipofumua nywele zake ili kuonekana alikuwa anasukwam


"'Akikuuliza jina mwambia unaitwa Mwajuma ."


"'Sawa .." Mr. Kucha aliitikia huku mapigo ya moyo wake yakiwa yanaenda kasi .


Hayawihayawi sasa yalianza kuwa huku wahenga wakisema asiye na macho avae miwani .


Lisa alipunguza sauti ya bufa ndipo aliposikia sauti ikiunguruma. 


"Nani unagonga mlango?" Aliuliza


"Ina maana hujanisikia mda wote huo hee!"Noel alifoka kwa sauti ya ukali kwelikweli.


"Samahani mme wangu sauti ya redio ilikuwa juu afu nilikuwa nasuka.." 

Lisa aliongea kisha akafungua mlango.


Noel aliingia ndani akiwa kama amenuna kisha akafunga mlango na kuondoka na funguo .


"'Mbona unafunga mlango mchana huu?, ina maana hatutoki ndani?" Lisa alimuuliza mme wake.


Noel hakujibu chochote na badala yake alikwenda moja kwa moja kwenye vyumba vya wageni na kuanza kufanya msako wa aina yake mpaka akawa anazama uvunguni lakini hakuona chochote.

Wakati anaendelea na msako, Lisa aliketi chini ya kitanda na Mr. Kucha aķakaa kwenye kitanda kisha akaanza kumsuka huku akiwa amerembua macho kwelikweli.


Noel aliendelea kukagua kila sehemu lakini wapi ndipo alipojishika kwenye nyonga zake,


"Huyu Fetty hajanidanganya kweli!, kwanza yeye alikuwa wapi mpaka akawaona?, kama amenidanganya  mimi na yeye kitaeleweka. Haiwezekani niache kazi zangu kwa ajili yake ila ngoja niende chumba changu huenda atakuwa humo..." Noel aliongea kwa hasira 


Mr. Kucha akiwa anaendelea kumsuka Lisa chumbani humo huku akiwa amedamshi kama mrembo kweli, gafla mlango ulifunguliwa na Noel akaingia ndani.. . 


JE ILIKUWAJE?


ATAPONA MTU KWELI HAPO?


ITAENDELEA......

       BAKI HAPA HAPA KWENYE APP YETU

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: BINAMU 🔞 SEHEMU YA 11

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 1-5

CHOMBEZO: MASSAGE ROOM🔞 SEHEMU YA 21