MCHORA KUCHA PART 07
MCHORA KUCHA
MTUNZI:McLAURIAN
PART:07
ILIPOISHIA,
Noel akiwa amejawa na hasira,anazama
chumbani na kumkuta mrembo mkali
kweli kweli akiwa anamsuka mkewake...
SONGANAYO...
Mr.Kucha ambaye alikuwa amerembwa
kweli kweli,alilegeza shingo na macho yake hali
iliyomfanya aonekane pisi kali ya hatari japo
mapigo ya moyo wake yalianza kwenda kasi
sana.
"Shemu karibu...." Mr.Kucha kwa sauti ya kirembo alimwambia Noel huku akitaka kunyanyuka kitandani hapo.
"Kaa tu wala haina shida.Waitwa nani?"
Alimuuliza.
Kabla ya kujibu,Lisa alidakia,
"'Anaitwa Mwajuma ni ndugu yangu wa mama
mdogo ambaye amekuja kunipaka kampani
maana naogopa kulala peke yangu.."Lisa
aliongea.
Baada ya kuambiwa hivo,Noel alijifanya
anafungu akabati kisha akazama chooni lakini
hakuweza kuona chochote.
Aliinama mpaka uvunguni mwa kitanda ndipo Lisaa lipomuuliza,
"'Mme wangu unaangalia nini?"
"'Kuna kiatu changu kimoja sikioni sijui kiko wapi?,..alimjibu.
Wakati mazungumzo yanaendelea,Mr.Kucha
aliendelea kurembua kwelikweli huku akiwa
hajui kama kashagundulika au laa.
"Habari ya huko nyumbani"..Noela alimuambia Mr.Kucha huku akiwa anamuangalia kwa jicho
la chongo.
"'Ni nzuri shemu pole na majukumu.."akiwa
amebinua midomo, Mr.Kucha(Mwajuma)aliitikia
"'Asante hapa una muda gani toka umefika.?"
Alimuuliza.
Baada ya kuulizwa hivo,Mr.Kucha alihisi kama
roho yake inachomolewa mara baada ya kuhisi
siri kufichuka.
"Nina kama siku 4 hivi..'"alijibu kwa wasiwasi
"'Kweli shemu au unanidanganya...:"
"'Ni kweli..."Mr.Kucha alijibu kwa tabasamu ya
uongo.
"'Kwanini unamuuliza hivo na wewe mme wangu?,"Lisa alidakia huku akiomba sana.
"'Kwani kuna ubaya gani?"
"'Ayaa bwana..."
Baada ya muda mfupi, Noel alitoka chumbani
humo huku akiwa haamini mpaka nje ya
nyumba nakuendelea na msako.
Alisaka kila sehemu lakini wapi ndipo
alipojisemea,
"'Huyu Fetty popote pale nitakapokutana naye
atanilipa gharama za muda wangu.Yaani kaniamsha usiku wa manane kumbe hamna
kitu!,labda nisimuone.."
Wakati anaongea peke yake kwa nje, Mr.Kucha
alichungulia huku na kule kishaa kamwambia
Lisa,
"'Naomba unisaidie maana tayari kashanigundua hivo ataniua...huuu..!"
"'We bado hajagundua na unataka ufanyeje sasa?"
"'Nataka nitoroke.."
"'Hapan autajitafutia matatizo lakini pia nami
utaniweka matatizoni.Ninavyomjua Noel
asingegundua afu akakaa kimya.
"Huo ni mtego kaniwekea nakwambia..."
"Tulia tena utakaa hata wiki nyumbani..."
Mr.Kuchaa lijikuta anakuwa mdogo gafla kama
piriton huku akiendelea na shughuli nzima ya
kumsuka Lisa.
Akiwa anaendelea, Noel aliingia chumbani
humo,Ndipo walipoinuka nakutaka kwenda
sebureni.
"Mnaenda wapi?"Noel aliwauliza
"Shemu tunanda sebuleni tukuache upumzike"
Mr.Kucha aliongea.
"Ohh sawa haina shida hata ukitaka kubaki
hapa."Alijibu Noel
Mr.Kucha kwa uangalifu mkubwa,aliinuka
taratibu huku Noel akiwa anashangaa wowowo
la Mr.Kucha lililokuwa kwenye dera huku kifua
chuchu saa sita zikichomoza.
Mwonekano wa Mwajuma(Mr.Kucha)
ulimuacha Noel njia panda mpaka akajukuta
anameza mate bila sababu.
Wawili hao hatimaye walifika sebuleni ndipo Mr. Kuchaa lipokimbilia mlangoni ilia kimbie lakini cha kushangaza alikuta mlango umefungwa..
"Looo!! MyGod,sina ujanja tena"aliongea kinyonge
"We mbona husikii!, unataka kuleta matatizo nyumbani!,nimekwambia tulia afu kuwa makini
na sauti yako pamoja na wigi.."Lisa
alimwambia Mr.Kucha.
Alikaa kwenye sofa kisha akaendele akumsuka,
Lisa.
Akiwa kitandani amejilaza,Noel aliona sisimizi
wakiwa wanaongozana kwa mstari kama
wakujiandikisha NIDA ndipo aliposhituka.
Aliamka gafla na kuangalia ndipo alipowakuta
wamejirundika sehemu moja kama nyuki
waliokosa mzinga huku wakiwa wanashambulia
vitu ambavyo vilikuwa vinafanana kama uji wa
mgando wa muhogo au kamasi zito lamtu
mwenye kikohozi kilichoanza kuoza.
"'Hee!, mambo gani haya!,inamaana walikuwa
wanaji.. wenyewe! Au ni kohozi tu.."
Noel alisogea karibu na kuwafukuza sisimizi
hao lakini alishindwa kutofautisha kwani vitu
hivyo vilikuwa vimeanza kukauka kwambali.
"'Asingekuwepo shemeji leo angeniambia huu
uchafu wa aina hii chanzo ni nini..."
Noel aliongea kishaa kachomoa shuka zima.
Baada ya kuchomoa shuka,alishangaa kuona
godoro likiwa limechorwa ramani ya Afrika
ndipo alipoinamana kunusa kwambali huku
akihisi ni mk**jo lakini harufu haikuwa hivo.
Alibaki na maswali mengi kichwani mwake
ambayo hayakuwa na majibu kwa wakati huo.
Alitupa shuka hilo chafu kwenye nguo za Lisa
kama adhabu ya kutofanya usafi kisha akajilaza.
Baada ya muda mfupi huku akiwaameanza
kupitiwa na usingizi,simu yake iliita ndipo
alipoipokea.
"'We nani?"Noel aliuliza kisha simu ikakatwa.
Baada ya muda mfupi meseji iliingia,
"Ni mimi Fetty nilikuwa nakuuliza kuwa
ushafika?"
"Unataka nini?!"Noel alimjibu huku akiwa
amekunjauso
"Jamani mbona unanijibu hivo?!"
"'Sitaki tena ujinga wako!,naomba
tuheshimiane!, yaani unaniharibia kazi zangu
kwa uongo na upuuzi wako..."
"Naapa tena Naapa Nimewaona na bado yumo
ndani maana tangu asubuhi nimekuwa
nikichungulia..."
"'Ebu katafute kazi ya kufanya.Nina hasira sana nawewe...acha kunichokoza na usirudie tena siku nyingine" Noel alituma meseji hiyo kisha
akazima simu kwa hasira.
Fetty baada ya kujibiwa hivo,alibaki na
mshangao mkubwa huku akiwa hajui nini
kinaendelea,
"'Hee! ina maana anadhani namdanganya au?,
ngoja niende tuone kama hatomuona"
alijisemeakisha akaanza kupiga hatua kuelekea
kwa Noel.
Baadaya kuukosa usingizi,Noel aliamkakisha
akamkuta Lisa akiwa anaangalia TV nashemeji
(Mr.Kucha).
"'Ohh shemu kumbe unajua kusuka vizuri hivi.."
"Najaribu shemu.."akiwa anarembua alimjibu
Noel.
"Ohh, unatumia kinywaji gani?"Alimuuliza.
"Natumia soda pepsi na maji"
"Ebu kamfatie mgeni soda pamoja na mboga.."
Noel alimpatia Lisa kiasi cha pesa kisha
akatoka nje kufata vitu hivyo.
Bila kuchelewa,Noel alifunga mlango kisha
akamsogelea Mwajuma(Mr.kucha).
"Shemu nimekuletea zawadi yako..." alimwambia huku akiwa amamsogelea
kwa ukaribu.
"'Iko wapi hiyo"kwa sauti laini sana,Mr.kucha
alijibu.
"Njoo chumbani nikuoneshe..."
"'Mhhh...naogopa dada asije nikutah uko"Mr. Kucha akiwa anatetemeka alijibu.
"Hapana ameenda mbali kidogo afu mlango
umefungwa. Kwani unaogopa nini"Noel
alimvuta Mr.Kucha naye akalazimika kuwa mlaini.
"'Shemu hapana niletee hapa..."
"Ebu njoo bwana..."alimvuta kisha akaingia
naye chumbani huku Mr.Kucha akiwa haamini
kabisa........
JE ILIKUWAJE?
ITAENDELEA..........
BAKI HAPA HAPA KWENYE APP YETU
Maoni
Chapisha Maoni