ROHO YA KUZIMU SEHEMU YA 2

STORY:-ROHO YA KUZIMU PAGE YA :-2 MWANDISHI:-AMANI KUYELA Page iliyopita iliishia pale Hashiru akiwa anatafuta namna ya kupenyeza gari lake la kifahari kwenye njia mbovu za uswahilini katika mtaa wa mtakuja. Sasa kama ida twende mzigoni,,,,vanvouver, wispa zempempeeeee,,,, Hashiru akiwa anatizama jinsi ya kupita katika njia ile, akaajitahidi kadri anavyoweza hadi akalipitisha gari nakuzidi kusogea mkabala kabisa na nyumba alipokuwa akiishi zehera, walipofika nje ya nyumba kulikua na watoto wengi wakicheza cheza pia majirani wakike walikua wamekaa nje katika mifuko ya sandarusi wakiwa wanapiga rusaku kama kawaida yao. Lakini walipoiona ile gari kali namna ile imekuja mtaani kwao, wakawa wanaongea chini chini kila mmoja akionyesha kushangaa sana kwa kuwa hawajazoea mtaani kwao kuona gari za maboss zikija. Wakawa wanatizama kwa umakini huku macho yao yote yakiwa chonjo kuangalia ni nani haswa nyangongo kaja na hiyo gari. Baada ya sekunde kadhaa akaonekana zehera akishuka akaanza kutoa mif...